Zitto Kabwe, wananchi wako tunanyanyaswa

rusesa

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
538
233
habari wana jf.
wakazi wa kigoma mjini tuliojiajiri kwa kuchota maji katika chemu chemu za lutare na kujakuyauza hapa mjini kigoma tumejikuta katika manyanyaso mno.

mkurugenzi kwa kushirikiana na madiwani, na mtendaji wa eneo tajwa wamekuwa wakitunyanyasa sisi wachota maji kwa kututoza kodi. miaka nenda rudi tumekuwa tukichota maji haya bila hiyo Kodi, maana chemu chemu hizi ni za asiri hazihudumiwi na serikali wala nini sasa kodi yanini?


kwa sasa dumu moja tunatozwa sh.500 kama kodi ya maji. hizi pesa sijui zinaenda wapi? zitto mbunge wetu uko wapi?

popote ulipo mbunge wetu uje kututetea.

Nawasilisha.
 
Zitto yupo dar anakula bata nyie lipeni hiyo kodi tu maana hakuna namna.
 
Kama mnafanya biashara ni wajibu wenu kulipa kodi, mkisha
lipa kodi ndo muulize pesa zenu
zinafanya kazi gani?
 
Yupo bize na IPTL na Mabilioni ya Uswizi. Mambo hayo madogo madogo mpelekeeni Diwani na Meya. Mtakoma kuipotezea CCM hapo ilikuwa rahisi tu unamtafuta mwnykt wa Ccm Kigoma Dr.Walid Amani Walid Kabourouh a.k.a Mwami kabuyuki aliekuwa Mbunge wa kwanza wa Upinzani Tanzania na Makamu Mwenyekt wa kwanza wa Chadema Taifa kabla ya kutubu na kurejea CCM angelimaliza lakin mkajifanya Wajanja kukataa CCM kila mchuma janga hula na wa kwao.
 
Kama mnafanya biashara ni wajibu wenu kulipa kodi, mkisha
lipa kodi ndo muulize pesa zenu
zinafanya kazi gani?


Kama kodi kwa dumu maana yake dumu moja ni 3000/=, swali ni je wanapewa risiti kuonyesha kuwa wamelipia kodi
 
Back
Top Bottom