Zitto Kabwe si mkweli

Rafa kilenza

Member
Jan 23, 2017
32
30
ZITTO KABWE AWAAMBIE UKWELI WANANCHI WA KIGOMA MJINI KUHUSU MAMBO HAYA

Jana mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha act wazalendo ndugu zitto z kabwe alifanya mkutano wa hadhara katika kata ya Gungu

Na katika mkutano huo zitto alilamika sana kuhusu serikali kuu kushindwa kupeleka fedha za maendeleo pamoja na raisi wa nchi kushindwa kusaini vyanzo vipo vya mapato vya manispaa

Kabla zitto hajataka serikali iwaambie wananchi wa kigoma kwanza naomba zitto kabwe kama kweli ni mzalendo wa kweli hawaeleze wananchi wa kigoma mambo yafuatayo

A..MAPATO YA BAJAJI
Baraza la madiwan la kigoma mjini linaloongozwa na chama cha act wazalendo kilipitisha tozo kwa kila bajaji iliyopo ndani ya manispaa ya kigoma kwa kutoza tsh 500 kwa siku na jumla ya bajaji katika manispaa ni bajaji 1000 kwa hiyo kwa siku moja wanakusanya tsh 500,000/=
Kwa siku kamilifu za mwezi wenye siku 30 wanakusanya tsh 15, 000,000/=Tsh
Sasa tunaomba mbunge zitto awaeleze wananchi wa kigoma mjini na watanzania wote kuwa hizi fedha wanazipeleka wapi?
Mbona kwenye vitabu vya manispaa hizi fedha hazionekani?
Zitto tunaomba jibu kuhusu hilo jambo

B. MAPATO YA KATOSHO
Manispaa ya Kigoma mjini ililikodisha bwawa la katosho ambalo lilikuwa ndio msingi mkuu wa chanzo cha maji kwa wananchi wa kata ya gungu
Kutokana na shida ya maji ndani ya manispaa ya kigoma mjini manispaa ya zitto iliamua kukodisha bwawa hilo kwa mtu ambaye ni rafiki mkubwa sana wa zitto kabwe na kuzuia wananchi kutumia bwawa hilo
Hakuna anayejua adi sasa ni kiasi gani kilicholipwa kutokana na kukodisha bwawa la katosho na imebaki siri ya mbunge na madiwani wake
Mtu aliyepewa katosho ni rafiki mkubwa sana wa zitto pamoja na bahadhi ya madiwani wake
Ukiwa kama mzalendo wa kweli tunaomba kwa dhati uelezee mapato yaliyotokana na kukodishwa kwa katosho na kwanini umeamua kuzuia wananchi wasichote maji hapo
Mh zitto tunaomba majibu ya hilo swala

C..UJENZI WA VIBANDA VYA STENDI

Madiwan wa act walipitisha mradi wa kifisadi zaidi wa mradi wa ujenzi wa ukuta na vibanda 37 vya stendi kuu ya Masanga kwa gharama za tsh 840,000,000/= yani milion mia nane na arobaini

Huu ni wizi mkubwa sana haiwezekani ujenzi wa vibanda 37 ugharimu kiasi chote hicho cha fedha
Tunaomba zzk uwaeleze wananchi wako gharama halali za ujenzi huo na sio hizi za kifisadi

D. KUVULIWA UANACHAMA KWA DIWANI BABA LEVO

Kipindi cha kampeni za ubunge msemaji mkuu katika kampeni za act alikuwa baba levo lakini baada ya baba levo kupinga hadharani ufisadi unaofanywa na chama chake hasa katika mirada ya ujenzi baba levo ameanza kutengwa na kutopewa nafasi tena katika mikutano na kuambiwa ana tumiwa na ccm
Hili ni jambo la kawaida sana katika vyama vya upinzan pindi anapojitokeza mtu anayepinga ujinga ndani ya chama lazima abatizwe jina la msaliti
Tunaomba kujua kwanini baba levo anatengwa sasa hivi?
NDIMI
RAPHAEL LUKINDO
 
Back
Top Bottom