zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Huelewi kuwa wakati wa Kikwete ni wakati wa utendaji? Usione hawa wapinzani wanawahi kukimbilia kuita waandishi wa habari na kubandika haya mambo kwenye mintandao, hayo yote ni mambo yanayotekelezwa kwa sasa hivi. Kuhusu Matrekta, mpaka sasa wameambiwa wakubwa wa mikoa na wilaya wao ndio wakasimamie wahakikishe kama si vikundi hata mtu mmoja mmoja anakopeshwa kwa dhamana ya hilohilo trekta na sehemu yake ya kulimia tu. Naona hujui kinachoendelea. Umeshindwa kuelewa kuwa kwa mara ya kwanza sasa na toka mpango wa Kilimo Kwanza na akiba ya chakula tuna akiba ya chakula ya miezi sita ujayo na inatuna kila mwaka, tunategemea mwaka huu itafikia akiba ya mwaka mzima kwa mahindi. Mwakani tunategemea kuona mchele kwa wingi sana kwa kuwa kuna mabonde ya kulima mpunga amabyo ni kipa umbele kwa sasa. Tatizo la Watanzania ni kuwa umeshapewa bi harusi, haitoshi unataka usaidiwe kuvuliwa na nguo zake, nayo haitoshi, unataka usaidiwe mpaka (ashaakum si matusi) kunyanyuliwa miguu yake, na hiyi mnaona haitoshi, mnataka mpaka msaidiwe kumshughulkia huyo bi harusi. Nyie kaeni na kudakia hoja na mipango ambayo inafanyiwa kazi, mnalalamika kufanyiwa, wenzenu wanatekeleza na wanafanya kweli. Of course, Rome was not built in a day, we are heavily under construction right now, way past the drawing room.Mipango tunayo mizuri huenda tatizo likawa ni utekelezaji wake,mie naamini muda tractor zilivyokaa pale SUMA JKT ungetumika kukopesha vikundi mbali mbali vya uzalishaji kupitia Saccos zao,Deni lingekuwa limelipika au kupungua kabisa na uzalishaji ungekuwa umeongezeka. Tumejenga kasumba ya kutoaminiana na kisha kulaumiana kuwa ni wavivu na wazembe bila kuwa na sababu za msingi.