English Learner,
Ni Imani yangu uko salama ndugu yangu na pole na majukumu. Ndugu yangu utaniwia radhi kwa kutaja jina lako hapa, lkn ni kwasababu nahitaji msaada wako hapa. Naamini kuna wengi pia watachangia lkn kamwe usisite kutia mchango wako hapa, kwani unahitajika sana.
English Learner,
I need your assisstance in constructing a theory based on the informationprovided below. I was really touched by the theory you constructed from what happened during the presentation of the Opposition Budget 2012-2013 made by Hon. Zitto Kabwe this month. You made something with a lot of valid information, and I congratulateyou for that my dear. Today I really need your help again on these issues by constructing a theory and tell us something about the hypotheses from the literatures provided below;
A: OLD NEWS ABOUTZITTO KABWE AND CHADEMA
Moto wawakaChadema, NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO
Sunday, 01 May 2011 22:56
By Ramadhan Semtawa
VITA vya makundi vimezidi kuviandamavyama vikubwa vya siasa nchini, ambapo sasa hali si shwari ndani Chadema,ambako kunadaiwa kuwepo mkakati wa kumng'oa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho,Zitto Kabwe.Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa KigomaKaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anadaiwa kuponzwa na msimamowake kupinga ununuzi wa magari mitumba yenye thamani ya Sh480 milioni yaChadema.
Zitto Kabwe boostsCCM will never defeat him
Thursday, 09 September 2010 08:34
By Ramadhan Semtawa
Former Kigoma North MP Zitto Kabwehas vowed to retain his seat in the coming General Election despite plans by ChamaCha Mapinduzi to oust him. Mr Kabwe made the statement after the CCM campaignmanager, Mr Abdulraham Kinana, announced plans to win all constituencies thatwere under opposition parties in the last five years.Mr Kinana was quoted as saying thatCCM planned to win all constituencies which were under opposition parties. Hesaid they were going to set camps in those constituencies, including KigomaNorth and Moshi Urban, in a bid to dislodge outgoing MPs.Mr Kinana was quoted to say thatthere was a need for the ruling party to strengthen its campaigns in someconstituencies which have been dominated by opposition parties for a long timenow.But in his response Mr Kabwe saidthe ruling party had no power to oust him. He said Kigoma North would alwaysremain an opposition party's constituency since voters were aware of thestrength and importance of electing him.
Zitto atembea nabarua ya kujiuzulu Chadema*
ASISITIZA ATAMUUNGA MKONO KAFULILAKIGOMA KUSINI
Na Ramadhan Semtawa
HALI ya kisiasa ndani ya Chadema,inazidi kuwa mbaya, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa chama, Kabwe Zitto kuandaabarua ya kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya chama ambayo anatarajiwa kuiwakilishawakati wowote atakaporejea nchini.
Zitto kupitia barua pepe aliyoitumia Mwananchi Jumapili, aliweka bayana msimamowake wa kuchukizwa na siasa chafu zinazoendelea ndani ya chama hicho na kwamba,sasa yupo tayari kujivua nyadhifa zote ndani ya chama hicho ukiwamo ubunge. "Ninayo barua ya kujiuzulu kilanafasi niliyonayo ndani ya chama ikiwamo ya ubunge, nataka kuendelea na maishayangu," aliweka bayana Zitto. Hatua hiyo ya Zitto ambayo inazidi kukiwekachama hicho njiapanda, inakuja wakati Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa,akieleza kwamba hali ni shwari ndani ya chama hicho.Wakati akizungumza na waandishi wahabari juzi, pamoja na kutetea uamuzi wake wa kuwatimua Ofisa Habari wa chamahicho, David Kafulila na Ofisa wa Bunge, Danda Juju, Katibu Mkuu huyoalilishambulia gazeti la Mwananchi kwa madai kuwa linaishambulia Chadema kwakuchapisha habari inayoeleza hali tete iliyopo ndani ya chama hicho. Akielezeakuhusu hatua yake hiyo, Zitto alisema: "Sitaki kugombana na mtu mimi.
Zitto Kabwe atangazakung'atuka
Published 03/1/2007
na Ramadhan Semtawa
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, ZittoKabwe, ametangaza kung'atuka katika wadhifa wake mwaka 2010. Kabwe alitangazaadhima yake hiyo jana, wakati akiongea na waandishi wa habari katika Hoteli yaGreenbeach mjini Maswa mkoani Shinyanga.Alisema amefikia uamuzi huo bila kushinikizwana mtu yeyote na ameamua kutangaza mapema ili kutoa nafasi kwa wanaotaka kugombeanafasi hiyo, ili wajiandae.Kabwe alisema anatamani kufanya kaziza kitaalamu, hasa zinazohusu taaluma yake baada ya kuwa mwakilishi wa wananchikwa kipindi cha miaka mitano."Tangu nimalize masomo yangu chuokikuu, ni kipindi cha mwaka mmoja tu niliofanya kazi kisha nikachaguliwa kuwambunge, hivyo nina hamu ya kufanya kazi nyingine mbali na hii ya uwakilishi,"alisema Kabwe.Alisema uamuzi wake wa kuachana naubunge hauhusuni na masuala ya siasa ambayo iko katika damu yake (Mwananchi, 2007).
B: CURRENT NEWS ABOUT ZITTO VS OTHER MPS
Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya(CCM) nae amekanusha kumpigia debe Zitto kwenye Urais. Kupitia ukurasa wake waFacebook, ameandika;
"Nasikitika sanakuambiwa kuwa nimempigia debe urais mh Zitto Kabwe. Huu ni uwongo wa kutubwatulienda Kigoma kuwaunga mkono wasanii wa Kigoma walioamuwa kwenda kuchangishafedha za ujenzi wa kituo cha vijana. Nilienda kama mbunge wa vijana kwa ajiliya kuunga mkono vijana wenzangu. Huu ni uzushi mkubwa. Natambua kila chama kinautaratibu wa kupata mgombea uraisi" (EstherBulaya, 24.07.2012).
Katika gazeti la Mwananchi la tarehe23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zittonjia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka nakusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na nduguJoshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema.
Napenda kusema masualayafuatayo.Moja, Waheshimiwa Wabunge HalimaMdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, RayaIbrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana waKigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.Wabunge wengine walialikwa lakinihawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamatana Peter Serukamba.
Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanyamazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumzaau hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.Waheshimiwa wote walipewa nafasi yakusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo nindugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwakwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile nakuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kamahabari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmojamaana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.
Kama mwandishikaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo.Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipikiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyoteile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hatamakanusho yao.Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.Suala la Urais lisitupotezee mudakwani kuna mambo mengi sanaya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.
Chama changu bado hakijatangazarasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Uraismpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuombakupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamiina wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo nahivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
Mzee Thabiti Kombo alituachia usiatunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akibaya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote (Zitto, 24.07.2012).
Nilikuwepo uwanjanipale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwahapa na zitathibitisha.Siwezi kuwaandikia mwananchi kwanimimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.Mimi ninaamini gazeti la Mwananchindio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambaloumiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaana hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasitikurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yotenchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. HivyoMwananchi linaaminika na umma.
Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchikama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe hukowalikochukiana.
Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepouwanjani tunajua nani alisema nini (Zitto,24.07.2012).
NB1: Kwa ajili ya kupata theory na hypotheses nzuri, pia unaweza ukaongezea na taarifa zozote ulizonazo kuhusiana na matukio ya namna hii ili tuweze kupata uhalisia wa mambo haya.
NB2: Mwana-JF yeyote anaruhusiwa kuchangia kwa kadri atakavyoona inafaa kwa ajili ya ukombozi sahihi wa nchi yetu na siyo kuwa na rangi nyingi na hatimaye watu washindwe kufahamu wapi mwelekeo wa Zitto Kabwe; Gazeti la Mwananchi na CHADEMA.
Ni mimi TELO.