Zitto Kabwe: Sitopoteza muda kuwajibu waliotunga email feki

Zitto Kabwe: Sitopoteza muda kuwajibu waliotunga email feki

Status
Not open for further replies.
sasa nimeamini ni za kweli. mbona ametoka kujibu mapema hivi??? et font zunatofautiana aoneshe font zilizotofautiana

Kashikwa Pabaya mkuu.Ogopa kukamatwa hivi ukifanya ukuwadi hakuna tofauti na kukamatwa ugoni.
 
Mnaodhani mna chama inabidi mfikirie upya.

Teeeeeh teeeeh teeeeh teeeh kumbe kina mwl kaijage ni watumishi tu akiamua anawatimua? Ni sawa na bakhresa akiamua kuiuza azam football club anauza!
 
Kwani watu wanaposema nchi yangu tanzania ina maana gani hii Jf imekuwa ya kishambenga sasa
 
attachment.php

Hiyo "Chama changu" mbona kama imeongrzwa na mtoa mada kama ukisoma kwa makini hii tweet!
 
Kama wapo mikumi ni vizuri watapokelewa na profesa j ili washindane kumwaga mistari na yule mzee anaye jiita msanii kioo cha jamii
 
maskini chadema wanahangaika poleni.

mchaga hamumuwezi muha mchumi mjenga hoja mzuri.
kuna muda kidogo kuna makada wa ccm walikuwa wanamzungumzia zito kuwa ni kijana anaeweza kujenga hoja vizuri sana
 
Maneno ya Zitto Kabwe
Nimepewa taarifa na kupata kuona email za kizushi zinazojaribu kunihusisha na mawasiliano feki na Mwigulu Nchemba.
Kwa mtu yeyote mwenye uelewa hata mdogo wa uhariri wa picha kwa kompyuta mfano Photoshop, anaweza kugundua kwa wepesi kuwa email hizi zimehaririwa kwani hata maandishi yaani fonts ni za kupishana.
Nawahakikishia watanzania wote kuwa email hizi ni feki na za kizushi.
Sitakubali kupoteza muda kujadili uongo na uzushi kwani hivi sasa niko katika ujenzi wa chama changu ACT - Wazalendo nchi nzima.
Nawashukuru wote walioonyesha imani kubwa kwangu na kutambua kuwa siwezi kujihusisha na mbinu yoyote chafu. Siku njema
Leo tupo Morogoro, kesho Dodoma
Kila siku jambo la kwanza huwasoma watu wangu mashuhuri nchini kama mitandao toka Slaa, Zitto, Mnyika, Maria Sarungi na #ChangeTanzania , Abdallah Mwinyi, January Makamba, Mohamed Mtoi, na wengineo wengi tu kupata habari zao mpya na mambo muhimu yanayowagusa.

Ni rahisi watu kutunga habari na wakaikuza wakati sio kweli. habari kama hizi zina malengo yake na wajinga pekee ndio huzipokea na kuziamini...lakini watakapo gundua Ukweli hawatakuamini tena kwa ujinga uleule..
 
Gazeti la Mawio la tarehe 16/04/2015 , limeandika mawasiliano yaliyonaswa kati ya Mwigulu Nchemba na Zitto,mawaslioano hayo ya email yameonyesha jinsi Zitto anavyotumika kudhppfisha upinzani.

Kwa tunavyomjua Zitto anavyopenda kukimbilia mahakamani, kwanini kwa hili hajaenda mahakamani kulishitaki MAWIO?

Kama tulivyotegemea atakanusha..amekanusha kwenye mitandao ya kijamii . Je, kukanusha tu inatosha kwa kashfa nzito kama hiii?? Je anahofia nini kwenda mahakamani?

Naamini anajua ushahid utakaowekwa wazi na MAWIO huko mahakamani , hautamuacha salama!! Hiii inatupa picha ya wazi kuwa Zitto anatumika kudhoofisha upinzani upo!!

Huu ni zaidi ya usaliti kwa watanzania..hii ni dhambi kuwa KIBARAKA wa kuua demokrasi anafanya kwa watanzania, na kama Mungu wanayemuomba watanzani yupo Hai Zitto hafiki mbali.Very soon atakutana na hukumu ya Mungu.

DSC01394.jpg
 
Hana muda wa kipuuzi huo, kazi iliyopo sasa ni kusambaza UZALENDO tu, hiyo singo ilishabuma na hilo gazeti linatafuta Kiki tu, kwanza ndio mara ya kwanza nasikia kuna gazeti hilo
 
Huu sio wakati wa siasa za majitaka. Ni mwendo wa kusambaza Itikadi ya Ujamaa wa Kidemokrasia na Uzalendo.

Siasa za kwenye mitaro tumewaachia Chadema na Taasisi zake. Hizo ndo hasara za Taasisi kuongozwa na watu wenye elimu ndogo.
Ni haki yenu kwani hiyo ndo kazi ya simple mind.
 
Hana muda wa kipuuzi huo, kazi iliyopo sasa ni kusambaza UZALENDO tu, hiyo singo ilishabuma na hilo gazeti linatafuta Kiki tu, kwanza ndio mara ya kwanza nasikia kuna gazeti hilo

Kama ndio kwanza unasikia uwepo wa gazeti hilo inamaana wewe ni mbumbumbu na hujui mambo mengi hivyo ulipaswa kukaa kimya. Ina maana hujui pia kwamba chama hicho kipya kinajihusishba na mambo ya KAFARA?
 
Ukikaa kujibizana na MAWIO na wewe utakuwa MWENDAWAZIMU.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom