Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

Makutano Show

Member
Aug 3, 2012
21
65
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe leo kuanzia saa tisa mchana atakuwa katika kipindi cha Makutano Magic FM kinachoendeshwa na Fina Mango ambapo atazungumzia na kutoa ufafanuzi kuhusu shutma za rushwa zilizolitikisa Bunge hivi karibuni ikiwa ni pamoja na yeye kudaiwa kuwa mmoja wa wabunge waliohongwa ili kutetea madudu ya Tanesco.

Pia atazungumzia suala la mbio za Urais 2015 na posho kwa wabunge.

Wana-JF mnaruhusiwa kuuliza maswali na kutoa maoni ambayo yatasomwa katika kipindi.

Karibu.
Amejibu ifuatavyo, kwa baadhi nitakayokumbuka

- Urais, ni kweli ana nia ya kugombea pamoja na kwamba hajasema atagombea 2015,
- Anashangaa katiba yetu kuweka umri wa mgombea urais uwe 40, wakati baadhi ya nchi jirani ni 35
- Anapigania nyimbo za wasanii kwenye milio ya simu wapate 50% sasa hivi wanapata kiduchu - 7%?
- Amekataa kujibu swali la posho na mishahara ya wabunge - kasema aulizwe spika
- Kwa nini hayupo na wenzie kwenye operation sangara, kasemawamepeana ratiba na pia alikuwa ana ahadi ya kuhudhuria hicho kipindi cha Fina
- Mwanasiasa ampendaye amesema Halima Mdee, Spokesperson - Bibi Titi Mohamed,

Hayo ndio baadhi ya niyakumbukayo
JUMAPILI, AGOSTI 05, 2012 | EVANS MAGEGE

*Asema hajawahi kutangaza mwaka
*Akiri ni vigumu bila baraka za chama
*Aahidi kumuunga mkono atakayeteuliwa
*Masha naye aibuka, autolea macho ubunge


JINAMIZI la urais linaendelea kumwandama Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA).

Hali hiyo imetokana na mwanasiasa huyo machachari kushindwa kuweka wazi mwaka wa uchaguzi ambao atagombea urais kama ambavyo amekwisha kutangaza.

Zitto alipatwa na kigugumizi hicho jana alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Makutano kinachorushwa na radio ya Magic FM ya Dar es Salaam.

Zitto alihojiwa kuhusu masuala mbalimbali na katika suala la urais aliendelea kusisitiza kuwa anautaka ingawa alishindwa kutaja mwaka ambao atatekeleza azma yake.

Zitto alisema suala la kugombea urais ni azma yake kutoka moyoni na kueleza kuwa yeye ni tofauti na wanasiasa wengine ambao hulitaka jambo kwa kisingizio cha kutumwa na watu wengine.

"Ni kweli nautaka urais jambo ambalo nataka Watanzania wajue, mimi sikusema ni lini lakini nia yangu ipo…iwe mwaka 2015, 2020 au 2025.

"Dhamira yangu nataka siku moja kuliongoza taifa langu, kama mwanasiasa mkomavu huu ni uamuzi wangu kutoka moyoni, sijatumwa wala kuagizwa na mtu yeyote.

"Siamini katika kauli za kutumwa, kuombwa wala kuagizwa ila kwa mwanasiasa anayejiamini katika uongozi lazima athubutu kuweka dhamira ya kweli katika kuongoza wananchi,"alisema Zitto.

Hata hivyo, Zitto alisema pamoja na dhamira yake hiyo, ataendelea kufuata sheria na taratibu ambazo ni pamoja na kupata ridhaa ya chama chake cha CHADEMA.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema hadi hivi sasa chama chake hakina mgombea urais na kueleza kuwa muda ukifika suala hilo litakuwa bayana.

Zitto alisisitiza kuwa hana ubinafsi juu ya hoja hiyo na kusema kuwa mwanachama yeyote atakayeteuliwa kupeperusha bendera katika wadhifa huo yuko tayari kumuunga mkono.

Akizungumzia suala la tuhuma za rushwa linalohusisha wabunge kuhongwa na kampuni na baadhi ya makampuni ya mafuta, Zitto alirejea msimamo wake wa kupinga kuhusika katika rushwa.

Zitto alisema binafsi yake anaiamini tume iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika kushughulikia sakata hilo kwa kusema kuwa ripoti ya tume hiyo itabainisha ukweli iwapo anahusika au laa.

"Kwa sasa tumekuwa katika taifa la majungu, uwongo, fitna na tuhuma zisizokuwa na maana na haya yamekuwa kama maisha ya kawaida ya wananchi.

"Nadhani kwa hili tusiliongelee sana na tuiachie tume iliyoundwa kuchunguza jambo hili ifanye kazi kwa uhuru mkubwa..kwani inatakiwa kutoa majibu yake ndani ya siku 14…msihofu majibu yatatoka tu hivu karibuni,"alisema Zitto.

Zitto pia alisisitiza kuwa yeye siyo mla rushwa na wala hajawahi kula rushwa.

Mwanasiasa huyo kijana anadaiwa kuwa na utajiri mkubwa na baadhi ya mali anazodaiwa kuwa nazo ni pamoja na ujenzi wa kasri unaoendelea Mbezi Dar es Salaam na magari ya kifahari.

Katika mahojiano hayo, Zitto alikanusha madai hayo akisema maneno yote hayo yaliyoibuka ni fikra hasi juu ya nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

"Dhamana niliyonayo katika POAC inawajenge watu sura tofauti ya labda najinufaisha na madaraka yangu katika kamati hiyo…nasimamia mashirika zaidi ya 290, kwa hiyo wanafikiri Zitto ni tajiri.

"Na kama vile haitoshi ule msimamo wangu kupinga posho za ubunge nayo ilifanya wengi wachukie …lakini nitaendelea na msimamo wangu ule ule.

"Kuhusina na mali zangu ..mimi si tajiri kama wengi wanavyodhani, sina Range Rover, Hammer au jumba la fahari kama watu wanavyozusha.

"Mimi ninajenga Kigoma, Dar es Salaam sina nyumba, sina kiwanja achilia mbali kiwanja sijawahi kuomba kiwanja Dar es Salaam wala Dodoma, hilo kasri nitakuwanalo wapi?.

"Nakumbuka siku hiyo mambo haya yaliibuka ilikuwa siku ambayo bajeti ya Nishati na Madini ilikuwa inawasilishwa ….na katika wakati mwengine siku hiyo hiyo, mishahara na posho mpya kwa wabunge zilianza kutoka, hivyo basi wabunge wengi walichangia jambo hilo hadi wengine wasiopenda kuzungumuza siku hiyo walizungumza," alisema Zitto.

Alipohojiwa juu ya kiasi kipya cha posho na mshahara Zitto alikataa katu katu kuzungumzia hoja hiyo na kusema kuwa mtu wa kuulizwa ni Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Wakati huohuo, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha alisema bado anayo dhamira ya kuwania tena ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza.

Masha aliangushwa na mbunge wa sasa jimbo hilo, Ezekia Wenje wa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010 na hivyo kupoteza ubunge pamoja na uwaziri.

Masha ambaye alikuwa akihojiwa katika kipindi hicho alisema bado anayo dhamira ya kugombea tena kiti hicho cha ubunge wa Nyamagana lakini hajaamua atafanya hivyo lini.

Alisema kuwa hawezi kutangaza ni lini atafanya hivyo lakini iwapo wananchi wa jimbo hilo watamuhitaji kugombea uchaguzi ujao wa 2015 atafanya hivyo.

"Nikigomea tena sitashindwa …suala la kutaka kugombea ni lazima lakini kwa sasa nafanya biashara zangu binafsi…najipanga nitarudi tena katika siasa," alisema Masha.
 
Zitto amekuwa akijitenga na harakati nyingi za chama mfano ni M4C, wenzake wanahaha vijijini yeye yupo kwenye ziara binafsi.

Kwanini amekuwa hashiriki harakati za chama zaidi ya kujijenga binafsi? (Naomba asilete historia za kukitoa chama mbali, azungumze nafasi yake sasa katika chama)
 
Napenda umuulize maswali yafuatayo:

1) Kwa nini anamtetea Injinia Mhando wakati ameonyesha wazi mgongano wa kimaslahi (conflict of interest) kwa kuipa kampuni ya familia yake TANESCO bila kufanya full disclosure?
2) Kwanini yeye Zitto amekuwa akiandamwa sana na vyombo vya habari?
3) Nini vision yake juu ya Tanzania miaka 25 au 50 ijayo?
4) Tanzania ifanye nini ili kuepuka resource curse kama ilivyotokea Nigeria au DRC?
5) Katika 50 iliyopita kungekuwa na tuzo iitwayo "The Golden Tanzanian in 50 years" katika nyanja zifuatazo angempa nani awe hai au awe ametangulia mbele ya haki?
(a) Statesman -------------------------
(c) Economist -------------------------
(d) Chief Executive Officer -------------
(e) Entrepreneuer ---------------------
(f) Investigative Journalist -------------
(g) Most admired politician -------------
(h) The best diplomat ------------------
 
Swala la posho bungeni:

Mh. Zitto amefanya juhudi gani binafsi kama kiongozi wa juu wa CHADEMA kuhakikisha anawashawishi wabunge walau wa upande wake wa CHADEMA kumuunga mkono? Kwanini anashindwa kushawishi wabunge wenzake yeye akiwa kiongozi wa juu wa chama?
 
Haya ni maoni toka kwa wadau wengine ambao wameyatuma kwetu kupitia Facebook wall:

Francis Daudi Fanya kazi kaka, kama uchunguzi ufanyike na kuwajibika uwajibike kama ulihusika kweli, "huwezi kuona msitu ukiwa msituni" Mungu akipenda hata uwe rais kwani naamini umepikika kiutawala vya kutosha!
Isaac Shuaka Nikiwa jiji la Nairobi Kenya swali langu ni:

Nini mtazamo wake katika Afrika ya sasa ikiwa viongozi wake wanajihusisha na vitendo vya rushwa?
Killongo Ernest Zitto unakubalika sana kumbuka CHADEMA ni ya vijana, usihofu mwaka 2015 ni wetu kaza buti sisi tunakusikilizia
Gidion Kasekwa kaka Zitto keep it up, usiangalie watu wanasemeje lakini zaidi hakikisha malengo yako yanakamilishwa vyema. "stick to your dreams"
 
Mhe. Zitto,

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda jitihada zako na uzalendo wako lakini kuna sehemu umenitibua mpaka nahisi labda gazeti la Majira lilikuonea, hivi ni kweli uliandika ujumbe kwenda kwa Maswi wenye maneno haya?
“Maswi, sijawahi gombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana, tuhuma ambazo wewe na Waziri wako mnatoa dhidi yangu ni uwongo, uzushi na za kupikwa.

Mwambie Waziri wako na wewe binafsi, sijawahi kushindwa vita ya kulinda credibility yangu, sipendi ujinga hata kidogo, mimi nina uhuru wa kusema ninachoamini, sina bei tupambane tu tuone nani ataumia,

Ref: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...na-prof-muhongo-hauna-maadili-ya-uongozi.html

Kama uliyaandika wewe mwenyewe, uliyasoma kabla ya kuyatuma? Kama ni uzushi/uwongo, umelichukulia hatua gani gazeti hili?
 
Maswali:

1. Atueleze yale mawasiliano kati yake na Rostam Aziz yalioandikwa na gazeti la MwanaHalisi (toleo nimelisahau) yalikuwa ya kweli au la? Kama ni kweli atueleze sababu hasa za kutumia muda mrefu sana kuwasiliana na Rostam. Kama ni uongo, mbona tunafahamu na tuna ushahidi wa Rostam kwenda voda na kuchimba mkwara na kumtafuta aliyetoa data hizo?

2. Kwanini maudhui ya nje ya siasa yake yanaonyesha hamna ushirikiano na chama? Yaani team work?

3. Kwanini hakuwanadi wagombea wa CHADEMA Kigoma wala Dr. Slaa kule Kigoma kipindi cha uchaguzi mkuu 2010 Kiasi cha kusababisha chama kupoteza kura nyingi za ubunge na urais? Ikumbukwe hata Dr. hakufanya kampeni Kigoma kwa sababu hiyo.

4. Je, tukisema kwamba ulipoteza mwelekeo wa kisiasa pale ulipoteuliwa na Kikwete kwenye kamati ya madini tutakuwa tumekosea?
 
Hivi anaruhusiwa kulizungumzia wakati lipo kwenye kamati (Mahakama ya bunge)???.. Manake tumezoea hili neno 'Hilo lipo mahakamani haliwezi kujadiliwa'
 
Naomba athibitishe/afafanue kwa kina haya madai/matamshi yake yaliyopo kwenye tamko lake:

"Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali [KINA NANI?MUHONGO NA MASWI?KUNA UTHIBITISHO THABITI KUWA WAMETOA KAULI HIZI?] ambao wamekuwa wakizieneza [LINI?WAPI?] na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa"

"Baada ya tukio hilo, nikiwa hapa Dodoma, mwandishi wa habari wa gazeti moja alinifuata akiniambia kuwa wamekutana na Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake, Nd. Eliachim Maswi hapa hapa Bungeni na wamewaambia kuwa mimi nimepewa rushwa[MWANDISHI ALIWAREKODI?]. Hakutaja nimepewa rushwa na nani, kiasi gani na wala kwa lengo gani!Nimejaribu kumtafuta kwa simu Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake ili wanipe ufafanuzi juu ya mimi na Kamati ya POAC kuhusishwa na tuhuma hizi bila mafanikio, hali ambayo inaniondolea mashaka juu ya ushiriki wao katika kueneza au kuthibitisha uvumi huo [UNA MASHAKA AU HAUNA MASHAKA?]"

"Najaribu sana kujizuia kutokuwa na mashaka na ushiriki wao [MUHONGO NA MASWI] huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti"[WAMESHINDWA VIPI KAMA HAMKUWASILIANA?]

"Kote huko [CHC, KIWIRA N.K.] uadilifu na uzalendo wa Kamati hii [POAC] haujawahi kuhojiwa"[HII NDIO MARA KWA KWANZA KUHOJIWA? MKULO NA WENZAKE HAWAKUHOJI?]

"Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa [UNAWAJUA? UMEWARIPOTI PCCB/DPP/POLISI/KAMATI YA MAADILI YA BUNGE?] wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa"

"Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu [KINA NANI?] kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa Kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao [MBONA HUWATAJI NA KUIBAINISHA HII MIKAKATI?] ya kifisadi"

"Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani [KAMA UNAWAFAHAMU MBONA HUWATAJI?] ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha"


CHANZO: MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI « Zitto na Demokrasia
 
Mosi; Viongozi wote wa chama wako kanda ya Kati kuongoza operesheni Sangara. Yeye amesusia kushiriki na wenzake, Kwa hilo tu yeye hajioni ana agenda ya siri dhidi ya chama?

Pili anasemaje kuhusu yeye kuwashambulia wabunge wa chama chake Nassari na Mdee pale walipokana habari za uongo za gazeti Mwananchi kwamba wamemtangaza yeye ni mgombea urais wa CHADEMA? Alikuwa na maslahi gani na habari ile?
 
Hakuna jambo rahisi kaka yangu Zitto, hata wajumbe wa Mungu walipata vikwazo vingi, imani yangu kwako ni kubwa na nafahamu fika kwamba una malengo thabiti kwa watanzania wote na hasa wana Kigoma na wanajamii wa Kigoma Kaskazini, Usichoke
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Dada Fina kwa kutuwezesha nasi kujiunga nawe.

Swali kwa mheshimiwa: Ni kwanini kama ambvyo wadau wengi wanavyodai, anajitenga na wenzie kwenye kujenga chama na anategemea nani wampe kura za urais iwapo haendi kwa wanachama kama ambavyo viongozi wengine wa CHADEMA wanafanya?
 
Kwenye kura za maoni za JF kati ya Zitto na Slaa, asilimia 85 ya wapiga kura wanapendelea Slaa awe mgombea, asilimia 15 ndio wanataka Zitto. Je, Zitto haoni kuwa hiyo ni dalili ya kutokuungwa mkono katika harakati za urais na kwamba ana-'swim against the current'?

Je, ameshawahi kujaribu kuongea na Slaa ili kujua kama Slaa ana mpango wa kugombea urais 2015?
 
Nina maswali mawili yanayohusiana na wazo moja kuhusu CHADEMA

Maswali:

  • Nini msimamo wa chama kuhusu mafao ya wafanyakazi wanaojitoa?
  • CHADEMA kilichukua/kinachukua hatua gani ndani na nje ya bunge kuwatetea wafanyakazi kwa hili?

Wazo:
Nahisi iko haja kwa CHADEMA kuwa na msemaji wa chama ili misimamo na kauli muhimu za chama zitolewe kama kauli rasmi ya chama; tofauti na sasa ambapo mara nyingi chama hulazimika ama kumtetea mtu anapobanwa au kumkana pale anapotoa kauli kinyume na msimamo wa chama.
 
Mh. Zitto jamii imeshtushwa na utajiri wako wa ghafla ambapo inasemekana unajenga kasri Mbezi, pia unamiliki Range Rover 'Vogue' na hammer (magari ya kifahari);

Swali 1: Je, Mh. Zitto upo tayari kupitia kipindi hiki cha radio kulitangazia taifa/kutaja MALI UNAZOMILIKI?

Swali 2: Je, ukwasi ulio nao kwa kipindi hiki kifupi tangu uwe kiongozi (ubunge+ POAC) unaakisi vipi tumaini la vijana ?
 
Nina maswali mawili yanayohusiana na wazo moja kuhusu CHADEMA

Maswali:

  • Nini msimamo wa chama kuhusu mafao ya wafanyakazi wanaojitoa?
  • CHADEMA kilichukua/kinachukua hatua gani ndani na nje ya bunge kuwatetea wafanyakazi kwa hili?

Wazo:
Nahisi iko haja kwa CHADEMA kuwa na msemaji wa chama ili misimamo na kauli muhimu za chama zitolewe kama kauli rasmi ya chama; tofauti na sasa ambapo mara nyingi chama hulazimika ama kumtetea mtu anapobanwa au kumkana pale anapotoa kauli kinyume na msimamo wa chama.

Mkuu msemaji wa chama ni John Mnyika,inavyoonyesha hufuatilii mambo kwa sababu hayo yote unayozungumzia Mnyika ametoa kauli.
 
Dada Fina Mango, karibu sana ndani ya JF....mapresenter kama wewe ndiyo tunaowahitaji hapa jamvini ili mtupe mijadala tutakayoichangia kwa hoja kwa faida ya Taifa letu....mshawishi na Masoud Kipanya nae ajoin ndani ya JF.

ANGALIZO:
Endesha hicho kipindi cha leo kama mtu mwenye fikra huru kwa kumuuliza huyo muheshimiwa maswali mazito na yenye msingi. Usimuulize maswali mepesi na yasiyo natija kama wafanyavyo wale ma-presenter wa 'Radio fulani'

Kwa mda huu sina swali, ila kipindi kikianza nitakurukia hewani na swali la pasua kichwa kwa muheshimiwa.
 
Kwanini ana papara sana ya urais? kwanini asishughulike zaidi kukijenga chama ili waweze kuiondoa CCM madarakani, alafu mambo ya nani awe nani yatafuata? Kwanini watu wasimtafsiri kama mnafiki fulani anayetumiwa kukivuruga chama?
 
Back
Top Bottom