ndo mkombozi mnayemfagilia kila kukicha, yaani hata akijisaidia njiani mtasema zoa kwa sababu anatoka kanda ya kasakzi. isitoshe Zitto ana busara hata ya kuyaendea mambo, watu wanaleta ushabiki tu wa kumusakama zitto eti kwa sababu ana dhamira ya kugombea urais hicho tu ndo kinachowatoa roho cdm na sio kingine, kwa sababu mnataka mchaga na familia yake yote watawale nchi ila sio kabila lingine kama zitto, kwa taarifa yenu kumjadili sana zito ndo mnampa chati zaid na nyie kujishushia hadhi.
Wakuu heshima mbele,
Hoja ya Zitto kuwakilisha Upinzani ina mashiko lakini hoja nyingine inaibuka ni nani amemtua kuwakilisha upinzani? Maana tunavyojua ki Protocal ilipaswa Ikulu iiombe ofisi ya Spika Mbunge mmoja kutoka kambi ya Upinzani ashiriki kwenye msiba kwa niaba ya upinzani. Hata hivyo, Spika nae asingekuwa na mandate ya kuteua Mwakilishi kutoka kambi ya Upinzani. Ilipaswa ashushe dokezi chini hadi kwenye Ofisi ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani ndiye ateue Mbunge wa Kuwakilisha.
Sasa kama Jina la Zitto limetoka moja kwa moja kutoka Ikulu lazima watu wahoji. Kunani Zitto? Kwa nini asiwe Lissu au Nassari au Silinde au Wenje nk? Je uteuzi wa Zitto kwenda Ethiopia ulikuwa na baraka za Ofisi ya Spika na Kiongozi wa Upinzani? Haya ndiyo maswali ya kujiuliza, Mimi, wewe na wengine.
TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams)
tumbiri@jamiiforums.com
Mkuu TUMBIRI, nashukuru kwa kutufahamisha protocols kuhusu uwakilishi wa upinzani.
Quote yangu hiyo hapo juu inahusu hiyo signecha yako; mbona hukuweka Form 4, na darasa la saba? Nimejaribu kuona ambavyo signecha yangu ingekuwa iwapo ningefuata format yako, nikaona watu wasingeweza kunielewa.
Kichuguu
Executive MBA (in progress, expected in May 2013); P.E; MIEEE; MIET: Ph.D (Physics); Ph.D.(Engineering); M.S. (Math), M.Eng.Sc; B.Sc(Eng); Certificate of Service (JKT); Advanced Certificate of Secondary Education (PCM-Form 6); Certificate of Secondary Education (Form 4); Primary School Leaving Certificate (Std 7);
Kimbunga,Mkuu TUMBIRI tutajuaje manake wote tunabashiri tu. Bahati mbaya Spika ama KUB hajajitokeza na kukanusha kumteua!
Hujui kama Mhe. Zitto ni waziri wa Serikali kivuli. Yuko kwenye msafara wa Mhe Raisi kwa baraka za wananchi kama mbunge na waziri kivuli kupitia mihimili ya nchi.
Tatizo ni kuwa, kila jambo mnafikilia siasa siasa tu.
WAKUU!
Namshangaa huyu Mh. Zitto Z. Kabwe. Wakati wa mkutano wa M4C Morogoro tuliambiwa angehudhuria. Baadae mawasiliano kati yake na Makamanda waliokuwa kwenye harakati za ukombozi yakapotea. Leo hii katia timu Addis na Mkulu.
Makamanda, hii ime kaa je? wakati Makamanda wengine wakiendeleza harakati za kuwakomboa waTanzania huyu Mh. mbona yupo beneti na Magogoni sana?
Ni kuuliza tu Makamanda.
Nakubaliana na wewe Radhia huyu jamaa ni MOLE [ Ndumila kuwili au kwa jina limgine KIKULACHO!!] wa ccm humo Chadema, the sooner he is flushed out the better!!
wana forum tuwe na tafakuri za kina. viongozi wa vyama vya kisiasa ni viongozi wa kitaifa. licha ya tofauti za kisiasa, wanafaa kuheshimiwa na wanasiasa wote.
siasa siyo uadui. miezi miwili iliopita, lissu alikwenda na msafara wa spika ktk nchi za korea, japan........
prof kahigi alisafiri na jk pia. zitto kaenda na jk kwa mwaliko kutoka ikulu wakiwaandikia chdm kutoa muwakilishi atakae ungana na msafari wa rais kwenda ethiopia kuhudhuria maziko ya zanawi. zitto hajadandia msafara. ana baraka zote za chdm. msidhani mtu hujiunga na msafara bila ya mawasiliano ya awali kutoka ikulu na chama husika.
ukiangalia hiyo picha, utaona yupo pia haroun suleiman kutoka serikali ya znz, yupo lusinde wa ccm nk........
tuwe waungwana. zitto ninaemjua na uzalendo wa hali ya juu. sera yake ni TANZANIA KWANZA VYAMA BAADAYE. KWA WENGINE chama kwanza tanzania baadaye. hii ndiyo sababu inayomfanya zitto watu wengi wasimuelewe.
tutumie bongo zetu kujenga hoja siyo kufuata mkumbo!!!!!!!!!!!
Mkuu Kichuguu big up Mkuu wangu. Kwa vyeti naona sikuwezi kabisa Kaka. Mimi Form Four nilimaliza Kibaha High School. Nilikuwa mwanafunzi wa tatu kitaifa kwenye matokeo ya Form Four ambayo yalinipeleka kusoma Mzumbe kidato cha tano na sita. Primary nilimaliza pale Mugabe, Sinza.
TUMBIRI (PhD, HULL University, HULL City - United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com
Zitto ni disaster na ninashangaa watu ambao mnatoa povu kumtetea huyu gaidi wa ukombozi, huyo jamaa ni puppet leader, mfatilieni kwa makini mambo yake ndio mtagundua, huyu jamaa kama aliweza kumpigia kampeni Jk badala ya Dr.slaa 2010, je anashindwa nn kukisaliti chama? THINK BIG magreat thinkers huyu jamaaa hafai na sisi hatutacha kumchana live hata siku 1.
Mkuu, ungekuwa na upeo mkubwa wa kuelewa siasa usingejibu kirahisi hivi. Ni waziri kivuli kwa serkali ipi kivuli? inayoongozwa na nani au chama gani?
kwa uelewa wako kama angekuwa waziri kamili wa serikali inayotawala angeweza kujiamulia msafara kama huo bila kibali cha wakuu wake?!!!
Soma tena swali hili na kisha uje na jibu lenye mantiki "amekwenda kwa baraka za nani? Bunge, Serikali, CDM, Jimbo lake au binafsi?"
Upinzani sio vita, tujaribu kubadilika! Bado hajaenda kwenye tukio baya kumbuka ni msiba huo.
Agenda zake za uharibifu mtazielewa baadaye kidogo.