Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee?

P. kwa nini siku zote umekuwa mtetezi sana wa Zitto? sijawahi kuona ukipingana na hoja ya Zitto hata za kizushi kama zile za watu mia kuuawa, hata zile za kusena serikali haina chakula na watu wataanza kufa kwa njas, tulishasubiri hadi leo hatujaona hayo aliyo yasema, lkn nikuulize swali, Zitto mkoje naye mkuu na huwa anakupa nini hadi usimuone kuwa anachotaka muda wote ni political attention, leo unamtaja mbunge makini? jana kasema wanataka kumweka ndani kabla ya uchaguzi, ana nguvu gani hadi magu amuogope, wakati uchaguzi uliopita chama chake kilipata asilimia ambazo hazitajiki, je, Lissu atasemaje kama hata Zitto ni threat kwa uchaguzi ujao? hebu leo tuweke wazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Jiforopolitiki, karibu mitaa hii uone jinsi nimavyomsifu Zitto na kumfagilia.
P
 
Mkuu Jiforopolitiki, karibu mitaa hii uone jinsi nimavyomsifu Zitto na kumfagilia.
P
Mkuu Pasco,ukiona watu tunalalamikia huduma yako ujue kuna shida,kama tulikuzoea kutoa nondo halafu ukabadilika ghfla ni lazima tutalalamika tu,wewe ni mtu maarufu ndani ya JF na nje ya JF,sisi tuliokua tunakufahamu toka zama za DTV tunaumia sana kuona unayumba Mkuu,hata wewe ukubali ukatae umenyimwa uhuru wako,kwani ninaamini sana ulitamani ufunguke zaidi ya hivi lakini hauko huru,na kibaya zaidi ni tangu uitwe bungeni, au kitendo tu cha wewe kuitwa kuhojiwa bungeni ni kilikua cha kukutishia na kukuondolea uhuru wako kama mwandishi wa habari,hivyo kubali kuwa kitendo hicho kilikua ni cha kukuondolea uhuru wako wa kiuandishi kiaina,na hiyo ni ya moja kwa moja,sasa je mbinyo gani unaupata nyuma ya pazia unaokuondolea uhuru wako halisi kama tulivyokua tumekuzoea? Hiyo ni siri yako,kwa kifupi hata wewe huko huru kama vile wasivyokua huru wapinzani.
Ushauri wangu kama unataka kutupa nondo kama zamani anzisha ID isiyofahamika humu JF ili tuwe tunapata madini orijino,acha kuonge kwa mafumbomafumbo na ujanjaujanja.sisi tunaolalalmika tunakuona hauko kwenye viwango vyako vya zamani
 
2020 Zito ndiyo atakuwa Kub bungeni..kule zanzibar atapata wabunge wengi plus yeye huku bara
Huu ndio ukweli wenyewe wa 2020!.

Tukubali tukatae, JPM ni JIWE la ukweli, ni Mwamba, ni Jabali, hivyo kwa upinzani wa Tanzania huku Bara, kuna watu wawili tuu ndio wanaweza kupambana na JPM kwenye urais na JPM akapata angalau joto joto la uchaguzi, hawa ni Tundu Lissu na Zitto Zuberi Kabwe.

Kwa vile mpaka sasa hakuna uhakika wa Tundu Lissu kurejea nchini kuja kumkabili JPM kwenye urais, hivyo Zitto ndie mgombea pekee aliyebakia anayeweza kuleta impact kwenye urais.

ZZK asipokuwa mgombea wa upinzani kwa mwaka huu kumkabili JPM wa CCM, then ZZK ndie Mbunge pekee atakaye penya kwenye kasi ya JPM na kurejea Bungeni.

Kwa huku bara, tunakwenda kwenye Bunge la chama kimoja, ZZK ndie KUB, kupitia wabunge wa ACT watakao penyea Zanzibar, haswa kutoka Pemba na yale majimbo yao wawili ya Zanzibar.

Kwa huku Tanzania Bara, ZZK ndie mpinzani pekee atakayevuka kisulisuli cha CCM 2020
Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya... - JamiiForums

Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza - JamiiForums

P
 
Pascal Mayalla
Wanabodi,
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.
Mhe Zitto, kunapotokea uvunjwaji wa katiba, hatua ya kwanza ni kuomba tafsiri ya sheria kutoka mahakama kuu kama katiba imevunjwa au laa. Hili halikuihitaji kumshawishi mtu yoyote. Mtanzania yoyote anaweza.
P
 
Zitto aibua mazito ripoti ya CAG

SERIKALI ya Tanzania imevunja Katiba kwa kutumia kiasi cha shilingi trilioni 1.7 bila ya kupitia Mfuko Mkuu ambao hukaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amewaambia waandishi wa habari jana.

Katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya jijini Dar es Salaam jana kuhusu uchambuzi wa chama chake kwenye Ripoti ya CAG ya mwaka 2018/2019, iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita, Zitto alisema jambo hilo ni baya kwa sababu linaruhusu fedha za Watanzania kutumika pasipo kukaguliwa.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kulinda fedha za umma, Katiba iliweka ofisi ya CAG iwe inakagua mapato na matumizi yote ya serikali lakini uchambuzi wao umebaini matumizi ya shilingi trilioni 1.7 ambayo hayajakaguliwa na ofisi hiyo.
“Katika mwaka wa fedha wa 2018/2019, serikali ilitumia shilingi trilioni 1.7 bila kwanza kupitia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Baadhi ya fedha hizi zinatokana na mikopo kutoka nje.
“Hizi shilingi trilioni 1.7 zinazotokana na mikopo kutoka nje zimelipwa hukohuko; kwa mfano kununua ndege za ATCL na zinaweza pia kuwa zimetumika kuwekwa kwenye akaunti za watu binafsi huko nje. Utaratibu huu ni kichaka cha kukwepa kukaguliwa na CAG ili kufanya ubadhirifu,” alisema Zitto.

Janeth Joel Rithe @JaneRithe
Naibu Katibu Uenezi @actwazalendo

Simu: 0713556704
Email:riterite20@gmail
Mkuu Zitto, kwanza asante kwa taarifa hii, kwa vile umeihushisha na kuvunjwa kwa katiba, na taratibu za kushughulikia kuvujwa kwa katiba unazijua, nakuomba sasa, taarifa hii isiishie kwenye press conference na press release.
Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee? - JamiiForums
Du the needful
Usipochukua, then huu nao utakuwa ni uchozezi hivyo nashauri
Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa Uchochezi, Adai Rais Magufuli ni... - JamiiForums

Mahakama zenyewe ziko wapi? Kwa issues zinazomhusu Jiwe mwenyewe na kusigina Katiba, hakuna Jaji atakaye toa maamuzi in favour of upinzania/ Applicant . Kama ikitokea Mahakama Kuu Jaji aka award in favour of Applicant , ujue watakata Rufaa Court of Appeal na kule wataweka Majaji wao wa "kuchonga" Rejea kesi ya Bob Wangwe dhidi ya AG juu ya ma DED kusimamia uchaguzi.

Baada ya hapo ndiyo mwisho wa mchakato kwa kuwa ile Mahakama ya Afrika sisi tumejitoa kwa hisia na amri ya mtu mmoja, Jiwe.
 
Mahakama zenyewe ziko wapi? Kwa issues zinazomhusu Jiwe mwenyewe na kusigina Katiba, hakuna Jaji atakaye toa maamuzi in favour of upinzania/ Applicant . Kama ikitokea Mahakama Kuu Jaji aka award in favour of Applicant , ujue watakata Rufaa Court of Appeal na kule wataweka Mauaji wao wa "kuchonga" Rejea kesi ya Bob Wangwe dhidi ya AG juu ya ma DED kusimamia uchaguzi.
Baada ya hapo ndiyo mwisho wa mchakato kwa kuwa ile Mahakama ya Afrika sisi tumejitoa kwa hisia na amri ya mtu mmoja, Jiwe.
Mkuu Stuxnet, kazi ya mahakama sio tuu kuendesha kesi au mashauri mbalimbali bali pia kutafsiri sheria.

Eneo hili la kuitumia mahakama kutafsiri sheria sisi Tanzania tumekuwa hatulitumii kabisa eneo hili, katika kutafsiri sheria, mahakama inafuata utaratibu rasmi wa kutafsiri sheria unaitwa legal interpretation, ambao unaangalia mtunga katiba alidhamiria nini.

Mfano kwenye kuzuia mikutano ya siasa, mahakama ingeangalia katiba ilidhamiria ninj,
Jee katazo la rais limekiuka katiba
Wakijiridhisha yes limekiuka katiba
Baada ya kutolewa tafsiri ya mahakama ndipo sasa
wanafungua shauri kupitia Judicial Review, kuiomba mahakama itengengue kauli ya rais kwa rais kupewa amri za kimahakama kwa mihimili zinaitwa Prerogative orders au writs ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment
inayoitwa certiorari na kulazimishwa kufuta kauli yake, akigoma, ndipo ngoma inashuka bungeni.

Niliwahi kushauri Certiorari, Mandamus na Prohibition Kutumika Kuyafungulia Magazeti Yaliyofungiwa! Hadi Mwanahalisi!. - JamiiForums

Well put bro!! Na hivyo ndivyo inapaswa kufanyika. Ila mazingira ya Awamu ya 5 hayaruhusu. Judiciary wako highly intimidated and interfered na Executive. Yaani niseme hakuna Rule of Law. Zile hukumu zote za wanasiasa zinazifanyika Kisutu kama ile ya viongozi 9 as CDM au hiyo ya Maxene Melo, zote zinaandikiwa kwa Jaji Kiongozi na wale magistrates wanasoma tu. I hope you agree with me ila siyo lazima useme.
 
Zito anakuwa amekosa uzalendo kabisa. Mh Rais ni msema ukweli daima, na siku zote anasisitiza kwamba Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Iwaje ZITO Amsingizie kama ni kweli basi awaombe msama watanzania kwa kumshushia heshima Rais wetu mpendwa
 
Pascal Mayalla

Wanabodi,
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.
Kwa mantiki hii wapinzani wasipige kelele kuwa zuio la mikutano ya kisiasa kwa vyama vya upinzani ni udikteta. Bali rais alizuia hii mikutano kwa manufaa ya umma ili atekeleze yale aliowaahidi waTz. Ndio maana akaruhusu wabunge wafanye mikutano ndani ya majimbo yao ili kutoleta migongano. Ibara ya 30(1) The human rights and freedoms, the principles of which are set out in this Constitution, shall not be exercised by a person in a manner that causes interference with or curtailment of the rights and freedoms of other persons or of the public interest.
Kama alivyosema mkuu wa nchi for public interest sio wakati wa siasa bali wakati wa kupiga kazi,na ndani ya miaka minne watu wameona.
 
Of recent we have leaders who just follow their followers, they don't lead by showing the way or next move, wanataka tuwaongoze wakati wanatuongoza; Zitto in specific alivunja move wakati window of opportunity ilipotokea 2015, hii ni dhambi ambayo itatafuna hadi kucha zake, maana haisameheki, sasa yuko serious na lipi? tumbo lake ama mabadiliko aliyoyakinza 2015? Will the window of opportunity open wide again when he claims to be serious, no way, the entire nation is where it is due to ZZK 2015 actions

Huu ndio ukweli wenyewe wa 2020!.

Tukubali tukatae, JPM ni JIWE la ukweli, ni Mwamba, ni Jabali, hivyo kwa upinzani wa Tanzania huku Bara, kuna watu wawili tuu ndio wanaweza kupambana na JPM kwenye urais na JPM akapata angalau joto joto la uchaguzi, hawa ni Tundu Lissu na Zitto Zuberi Kabwe.

Kwa vile mpaka sasa hakuna uhakika wa Tundu Lissu kurejea nchini kuja kumkabili JPM kwenye urais, hivyo Zitto ndie mgombea pekee aliyebakia anayeweza kuleta impact kwenye urais.

ZZK asipokuwa mgombea wa upinzani kwa mwaka huu kumkabili JPM wa CCM, then ZZK ndie Mbunge pekee atakaye penya kwenye kasi ya JPM na kurejea Bungeni.

Kwa huku bara, tunakwenda kwenye Bunge la chama kimoja, ZZK ndie KUB, kupitia wabunge wa ACT watakao penyea Zanzibar, haswa kutoka Pemba na yale majimbo yao wawili ya Zanzibar.

Kwa huku Tanzania Bara, ZZK ndie mpinzani pekee atakayevuka kisulisuli cha CCM 2020
Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini haya... - JamiiForums

Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza - JamiiForums

P
 
Wanabodi,
Japo bandiko hili liko addressed kwa Mhe. Zitto, lakini hoja zake ni kwa Wapinzani wote, namuelekezea Zitto Kabwe kwa sababu kwa maoni yangu ndio mpinzani pekee kwa sasa anayeweza kusimama na rais Magufuli 2020, na Magufuli akahisi kijoto joto japo kwa mbali.

Ni kwa muda mrefu kumekuwa kukitolewa hoja za udikiteta wa rais Magufuli. Kama watu wale wale, wanatoa hoja zile zile miaka nenda miaka rudi bila kuchukua hatua zozote, then kuendelea kutumia hoja hizo ni kupiga tuu kelele, na kiukweli kabisa kelele zikizidi, zinageika a nuisances.

Swali ni hili

Swali kwa Zitto Kabwe na Wapinzani Wengine: Hoja ya Udikiteta wa Rais Magufuli, Kwa Nini Wewe Zitto na Wapinzani Mnapiga Tuu Kelele Bila Kuchukia Hatua Yoyoye?. Kelele zikizidi Zinageuka Nuisances, Jee Kelele Hizi za Udikiteta wa Rais Magufuli hivi sasa Isn't it a Nuisance?. Kama Upinzani Wenyewe wa Tanzania Ndio Upinzani Huu Ambao Umeishiwa Kabisa Hoja za Msingi!, Jee Tukisema Uchaguzi wa 2020 ni CCM Pekee?, Tutakuwa Tunawakatisha Tamaa Wapinzani? au Tunawaandaa Watanzania kupokea Ukweli Mchungu kuwa Tanzania Hatuna Kabisa Upinzani wa Maana?.

Bandiko hili linafuatia hoja ya Zitto kwenye bandiko hili Tanzania imetimiza Hatua 8 za kujenga Utawala wa Kidikteta?

Mhe. Zitto, with due respect, kitendo cha kurudia rudia kauli hii ya Magufuli ni dikiteta bila kuchukua hatua zozote, nazo ni kelele tuu.

Watanzania wa sasa hawataki kelele, wanataka matendo. Kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa, mnatakiwa mje kwa wananchi mtuambie mmefanya nini au mtafanya nini ili mchaguliwe na sio hizi kelele za udikiteta!.

Naomba kukukumbusha siku ile tulipokutana pale Karimjee, nilikushauri nini kuhusu hii hoja ya Udikiteta ?. Jikumbushe.

Watu wa mwanzo kuupinga udikiteta ni Chadema kwa kuanzisha Ukuta, na mtu wa mwanzo very vocal kuhusu udikiteta, nilitoa ushauri muhimu kwa Lissu kuhusu huu udikiteta, hivyo nakushauri Mhe. Zitto, niliisha kushauri kitu cha kufanya, na hapa kwa faida ya wengi, nashauri tena.

Kwa msio jua, udikiteta sio hoja ya kisiasa, ni hoja ya kisheria, matatizo ya kisiasa, yanahitaji ufumbuzi wa kisiasa na matatizo ya kisheria, yanahitaji ufumbuzi wa kisheria.

Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele! - JamiiForums
Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, zikishindikana ndipo sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.

Tukisema Tanzania hatuna kabisa any serious and credible opposition, viongozi wote wa upinzani mliopo ni wababaishaji tuu, na vyama vyote vya upinzani ni vyama vya upinzani uchwala, itakuwa ni kuwaonea?.

Kwa mwendo huu, acha tuu CCM itutawale milele, na wapinzani wanaojitambua na kuamua politics ndio full professional yao, tusiwalaumu wakijiunga CCM, wanaona mbali.

Kama haya yote unayaona, kwa nini hizo hatua usianze nazo wewe au na wewe pia kwa vile ni mtu wa Ujiji, hivyo unafanya kile Watu wa Ujiji wanachoita Surat Zubaa?.

Paskali.
Cape Town.
RSA
Rejea kuhusu Udikiteta
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni ...
Udikiteta Tanzania: Je, Rais Magufuli kweli ni dikiteta au ...
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...
UDIKTETA: Hongera Sana TWAWEZA, TZ hakuna Udikteta! Ila ...
Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni ...
Fungia Fungia Magazeti: Ni Udikiteta wa Serikali Magufuli ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...

Leo umeandika point nzito sana tokea mwaka uanze ila hofu yangu ni kesi ya uchochezi maana tulipofikia sio!!!
 
Back
Top Bottom