Zitto Kabwe na Moses Machali wafunika Kigoma Mjini

Zitto Kabwe na Moses Machali wafunika Kigoma Mjini

Zitto Kabwe ana kazi kubwa ya kuhakikisha anahudhuria kila mkutano wa ACT.asipoonekana yeye na mkutano wa chama chake unakosa watu kabisa na kuishia kuzomewa tu.
 
Last edited by a moderator:
Chadema ni hatari sio wakuamini kabisa siasa zao majitaka walikalilisha watanzania kuwa zitto ni msaliti kumbe wao ndo wasaliti.
Act ndo mpango Wa mjinimjini kwa sasa.
 
Hii ndo picha halisi. ..
 

Attachments

  • 1438452154394.jpg
    1438452154394.jpg
    86.8 KB · Views: 896
Yuko wapi Mwigamba? Au kazi yake tayari?
 
ZZK ni level nyingine.. Wanafiki wataongea kwa unafiki wao yet ACT z keeping growing and moving day by day. Shikamoo Zitto
 
Mbona chama chao ni huko kigoma tu?
Ni kweli wana nguvu kigoma... Ila kuna hii kitu inaitwa "Niche Marketing strategy". Sioni tatizo kuwekeza nguvu zao kigoma
 
Kitabaki kuwa chama cha baadhi ya Waha tu aje kwetu Mby kyl to Tdm tumuonyeshe misimamo ujinga wake abaki nao hukohuko Kgm nyambafu
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-WAZALENDO Ndugu Zitto Kabwe na Mbunge Moses Machali wamefunika kwa umati Mkubwa wa watu katika mji wa Kigoma Mjini.

Mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Kahabwa Gungu.

Yaani namshangaa kafulila amekomaa na NCCR ,wakati ACT HUKU KIGOMA NDIO HABARI YA MJINI
 
Thread closed!
Zitto ni nani?
Unatujazia seva
zitto ni mpinzani mwenye msimamo kwa hoja na sera. hanunuliwi hata bei ikiwa shs bil 10. huyo mungu wa chadema mnamjua wenyewe atawabariki kwa kula matapishi yenu.
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-WAZALENDO Ndugu Zitto Kabwe na Mbunge Moses Machali wamefunika kwa umati Mkubwa wa watu katika mji wa Kigoma Mjini.

Mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Kahabwa Gungu.


Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mstakhabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na Makaburu kama mkakati wa kujinusuru na kutoa nafasi kukabiri janga kubwa kuliko zote wakati huo la kuondolewa serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na Makaburu. Wakomunisti wa Afrika ya Kusini waliingia ubia na ANC ya mabwanyenye weusi ili kutokomeza kwanza ukaburu na mapambano na ubepari yaje baadaye. Katika Vita Kuu ya Dunia ya Pili wakomunisti walishirikiana na mabwenyenye wa mrengo wa kulia na kati kutokomeza janga kubwa zaidi wakati huo la ufashisti, yaani ubepari wa mrengo wa wa kulia kupitiliza. Hivyo hivyo mapambano ya kuleta uhuru wa Tanganyika yalivyo unganisha nguvu za mabwenyenye wazungu na waasia pamoja na zile za wakulima na wafanyakazi wa rangi zote kwa azimio lile la mkutano mkuu wa Tanu wa 1958 pale Tabora. Hivyo hivyo Mandela na ANC waliingia "urafiki wa mashaka" na De Clerk kiongozi wa Makaburu ili kuondolewa ukaburu kuwe kwa amani ya "kula matapishi" ya kuwalaani huko nyuma kuwa ni wabaya wa Mwaafrika!!

Mabadiliko ya haraka haraka yanayoendelea hapa Tanzania yenye lengo la kuondoa CCM madarakani kama chama dola kinachodumaza na kudhoofisha ushindani wa kisiasa miongoni mwa mabwenyenye wa tabaka tawala Tanzania ni mabadiliko yatakayoleta neema kwa Watanzania wote. Ile tu CCM kudhoofishwa na kujiunga UKAWA kwa Lowassa ni kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu ya mchukuzi.....Nikuondoa kizingiti kikuu cha kushamiri kwa demokrasia pana na maendeleo endelevu Tanzania ambacho ni kuhodhiwa na ukiritimba wa chama dola cha CCM kinachojinadi kama chama cha mrengo wa kushoto wakati ni chama cha mrengo wa kulia kama vyama vyote vya siasa Tanzania kwa sasa.

Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi ka wana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005, ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakaochukua sura ya demokrasia zaidi ili kuwa na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia (tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo), sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Ghafla mwanasiasa mwenye nguvu nyingi ndani ya chama cha kifisadi cha CCM, mwanasiasa ambaye umaaarufu wake umetokana na kuongoza mtandao uliouweka utawala wa sasa wa CCM madarakani, Ndugu Edward Lowassa, amekasirishwa na kukatwa jina lake na aliodhani ni rafiki zake ndani ya CCM na kuamua kusema basi na lolote liwe kwa kujiunga na vuguvugu la kupigania katiba mpya!! Naye sasa kang'amua kuwa Katiba ya sasa na ile Pendekezwa ni za ovyo maana haziruhusu kuwepo mgombea huru bila mizengwe. Hasira za Lowassa zimezaa tunda zuri la kug'amua kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Hasira hizi za mkizi ni furaha ya kunguru na ni busara kwa viongozi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla kutoongopa "kula matapishi yao" kwa kumkaribisha Ndugu Lowassa...huyu huyu waliomwita fisadi... kujiunga na UKAWA na kugombea urais. Nafasi ya kihistoria imejitokeza ya kukiondoa CCM madarakani kwa amani!!

Sishangai wasaliti wa vuguvugu la kukiondoa CCM madarakani wanatushauri sisi Watanzania wenye shauku ya kuutumia upenyo huu wa mpasuko ndani ya CCM kukiondoa CCM madaraka!!! Eti tuombe radhi kwa" kula matapishi yetu" wote tulio wahi kumwita Lowassa fisadi! Wao wanataka tuendelee kuvumilia kutawaliwa na CCM labda kwa miaka mitano au zaidi hivi mpaka chama kipya cha watakatifu kiitwacho ACT-Wazalendo kitakapo kuwa tayari kututawala badala ya CCM!! Sishangai kusikia ushauri huu kutoka kwa wasaliti hawa ambao kazi yao hata huko nyuma imekuwa ni kuudhoofisha upinzani dhidi ya CCM na kukisaidia CCM kiendeleee kuwa madarakani!! Hawa jamaa ni wasomi sana na ni wajanja sana, ilo lazima kulikiri!!!

Sitashanga kama haya ninayoyasema yatapigwa madongo na wasaliti hawa!! Historia itakapoandikwa baada ya UKAWA kupata viti vingi zaidi Bunge lijalo au hata kuutwaa urais na kupata Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba, itawapa hukumu yao stahiki, wajanja na welevu hawa! Bila shaka wanaoomba UKAWA ishindwe kupata viti vingi Bunge lijalo na iukose urais na hivyo tuendelee kutawaliwa na CCM na wao wapate viti vya kutosha kuwa viongozi wakuu wa eti upinzani muruwa wenye maadili ya Azimio la Arusha Tanzania!! Ni haki yao ya binadamu kuendelea na matumaini haya kama na sisi tulivyo na haki ya kuendelea na matumani yetu ya uwezekano wa ushindi mnono chini ya UKAWA dhidi ya ukiritimba wa chama kimoja chama dola cha CCM!

By Mwl. Lwaitama
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-WAZALENDO Ndugu Zitto Kabwe na Mbunge Moses Machali wamefunika kwa umati Mkubwa wa watu katika mji wa Kigoma Mjini.

Mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Kahabwa Gungu.

Kila kukicha kigoma kigoma tu kwani Tanzania ina mikoa mingapi?act mnatia huruma,na kwa taarifa yenu hapo kigoma hamtaaambulia hata udiwani
 
Back
Top Bottom