Zitto Kabwe kutopenda ubalozi wa Israel

Sirhan Sirhan Mpalestina Mkiristo aliyekuwa akiishi marekani aliyempiga risasi Bobby Kennedy baada ya Bobby kusisitiza kwenye kampeni zake kuwa akiwa raisi ataisaidia Israel kwa kuipa silaha kali!.

Kule Palestina, Si mpalestina Muislam, Si mpalestina Mkristo wote wanapewa kibano na Myahudi.

Sasa cha ajabu Mkiristo wa Tanzania anadhani Israel ni Taifa la Kikiristo, elimu, elimu, elimu.

Iko hivi

Wayahudi ndani ya Israel ni 75%
Waislamu ndani ya Israel ni 20%
Na Wakiristo ndani ya Israel ni only 2%
Waliobaki ni around 3% nyinginezo
 
Kama rai tu mitazamo ndiyo hii,huwa nadhani hata hawa viongozi wetu nao watakuwa na mitazamo kama hii.
 
Siasa za wakati huu tunaangalia zaidi manufaa ya taifa letu,
na utekelezaji wa Sera zetu za Mambo ya kigeni kwa mafanikio.

Siasa za kufungamana na upande fulani kwa manufaa yao zimepitwa na wakati.
Kipaumbele cha sasa ni maslahi manufaa ya taifa letu na sio vinginevyo.

Jambo lingine ni kuwa nchi yetu kwa miaka mingi imekuwa msuluhishi wa migogoro ya majirani zetu wanaokwaluzana, ili kuwa wasuluhishi wa kimataifa tunahitaji siasa za kutoegemea upande wowote bali kuwa katikati ili kukubalika na pande zote kama msuluhishi.

Kwa sasa itakuwa rahisi kuwaita pamoja Balozi wa Israel na Palestina ambao wote tunao hapa nchini, na kukaa nao pamoja na kuangali namna ya kuupooza mgogogoro wao bila kuegemea upande wowote.

Kinachozingatiwa kwa sasa ni MASLAHI YA TAIFA LETU.
 
Kuna maswali mengi nimejiuliza, Zitto bungeni ameongea kulaumu kwanini Tz imefungua ubalozi Israel, lakini hajauliza maswali yafuatayo:-
1. Kwanini Watanzania wengi kila mwaka huwa wanatembelea Israel (kama vipi aiombe serikali ipige marufuku watz kuitembelea israel).

2. Hajajua kama karibia 50% ya watz wanaipenda na kuisapoti Israel hivyo wangependa kuwa na ubalozi. hiki kimekuwa kilio cha wakristo miaka mingi sana, na ni haki yao wakristo kuwa na uhusiano na Israel.

3. Hajajiuliza kama anatakiwa kuwa na balance kwenye dini, kama upo ubalozi wa saudia wanakoenda wao kuhiji maca, kwanini kwetu sisi wakristo hakuna ubalozi wa israel tunakoenda kuhiji. nchi hii si ya kwetu wote, wakristo wanaoisapoti israel na wengine kina zito wasioisapoti.

4.Nimeshindwa kuelewa na kuamini kama hajawa religious motivated, ikizingatia dini yake.

5. Kuna siku maneno hayo aliyoyasema yatamhukumu kama yalivyomhukumu Membe akakosa urais baada ya kujifanya anaiponda israel ili kuwafurahisha baadhi ya watu. Siku ukija kuhitaji kura za ubunge au urais etc toka kwa watu wanaoupenda uhusiano wa kibalozi na israel, utapata jibu tu.

6. Tanzania tumefungua ubalozi, lakini hatujafungulia Jerusalem panapogombaniwa, tumefungulia mji mwingine kabisa.

7. Nchi karibia zote duniani zina uhusiano wa kibalozi, sisi tz sio kisiwa kwamba tujifanye tunapigania maslahi ya wapalestina leo, haitaleta effect yeyote, ni bora tu kushirikiana ili kuchuma matunda toka kwao kuliko kuyakosa kabisa.

nimetoa yangu ya moyoni dhidi yako wewe zitto.
Tangu uhuru 1961 Israel iliweka ubalozi Tanzania kwahiyo Ni mshirika WA zamani Sana.
Naambiwa benki kuu ya zamani walijenga wao
Kilimanjaro hotel walijenga wao
Jengo la ubalozi WA zamani WA USA kabla ya kulipuliwa bomu lilikuwa la ubalozi WA Israel

hapo namba 6. I hope one day we will move to Jerusalem
Naipongeza serikali ya awamu ya 5 kwa kurudisha mahusiano
 
Siasa za wakati huu tunaangalia zaidi manufaa ya taifa letu,
na utekelezaji wa Sera zetu za Mambo ya kigeni kwa mafanikio.
Siasa za kufungamana na upande fulani kwa manufaa yao zimepitwa na wakati.
Kipaumbele cha sasa ni maslahi manufaa ya taifa letu na sio vinginevyo.
Jambo lingine ni kuwa nchi yetu kwa miaka mingi imekuwa msuluhishi wa migogoro ya majirani zetu wanaokwaluzana, ili kuwa wasuluhishi wa kimataifa tunahitaji siasa za kutoegemea upande wowote bali kuwa katikati ili kukubalika na pande zote kama msuluhishi.
Kwa sasa itakuwa rahisi kuwaita pamoja Balozi wa Israel na Palestina ambao wote tunao hapa nchini, na kukaa nao pamoja na kuangali namna ya kuupooza mgogogoro wao bila kuegemea upande wowote.
Kinachozingatiwa kwa sasa ni MASLAHI YA TAIFA LETU.
utamununiaje mtu ambaye hajakukosea ati sababu anampiga kijakazi wake ambaye hataki kumtii
 
Sirhan Sirhan Mpalestina Mkiristo aliyekuwa akiishi marekani aliyempiga risasi Bobby Kennedy baada ya Bobby kusisitiza kwenye kampeni zake kuwa akiwa raisi ataisaidia Israel kwa kuipa silaha kali!.

Kule Palestina, Si mpalestina Muislam, Si mpalestina Mkristo wote wanapewa kibano na Myahudi.

Sasa cha ajabu Mkiristo wa Tanzania anadhani Israel ni Taifa la Kikiristo, elimu, elimu, elimu.

Iko hivi

Wayahudi ndani ya Israel ni 75%
Waislamu ndani ya Israel ni 20%
Na Wakiristo ndani ya Israel ni only 2%
Waliobaki ni around 3% nyinginezo
Asante kwa kutuelimisha sasa kunawatu humu ukisema waisrael wanazani umeusema ukiristo wanadhani zito anapambana na ukiristo ukiuliza na magu kufungua ubalozi Israel anapambana na uislamu hapo matusi yanaanza nakujifanya wanajua kufunika kombe
 
Tangu uhuru 1961 Israel iliweka ubalozi Tanzania kwahiyo Ni mshirika WA zamani Sana.
Naambiwa benki kuu ya zamani walijenga wao
Kilimanjaro hotel walijenga wao
Jengo la ubalozi WA zamani WA USA kabla ya kulipuliwa bomu lilikuwa la ubalozi WA Israel

hapo namba 6. I hope one day we will move to Jerusalem
Naipongeza serikali ya awamu ya 5 kwa kurudisha mahusiano
hongera serikali kwa hilo pia kutekeleza uhamishaji wa makao makuu kwenda Dom ambayo ni Jerusalem ya Tz
 
Nyerere alikuwa Muislamu alipovunja uhusiano na Israel?
Nauliza tuu, au alikuwa na sababu nyingine?

Ni mtu mshamba tuu anahusisha kila jambo na udini?
Nani amepinga ubalozi wetu Vatican?
Mwisho mtoa post aelewe Wayahudi sio Wakristo na sehemu kubwa ya historia ya Bwana Yesu Kristu ipi Palestine sio Israel.
Yaani mtoa mada atakuwa na utando mzito kwenye ubongo.Mtanzania au Mbunge sasa asihoji maamuzi ya serikali yetu aidha atakuwa katumwa na mabeberu au ni mdini.....?
 
Hoja iliyopo mezani inahusu Morocco ama Israeli na Palestine?!
JF inaaminika members wake wameenda shule... angalau kwa kiwango cha kidato cha IV! Watu walioenda shule hawa-conclude mada bila kuwa na reference!

That having saidi, hoja hapa sio Morocco wala Israel bali hoja ni kwamba Zitto anapinga uhusiano wa kibalozi na Israel!

Mijadala kwa watu walioenda shule lazima wajiulize ni kwanini Zitto anapinga uhusiano na Israel.

WHY? HOW? ni miongoni mwa maswali ambayo watu wanatakiwa kujiuliza kabla ya kutoa conclusion!

WHY not Israel jibu tayari amelitoa wazi ni kwa sababu Israel inaikindamiza Palestine!

Watu wanaoendesha mijadala kama walioenda shule wasingetoa hukumu hapo hapo kama mlivyofanya nyinyi bali wangeendelea kujiuliza ikiwa huyu Zitto ana silika ya kupinga ukandamizaji kwa namna ile ile anayoipinga Israel!

Baada ya kujiuliza hayo ndipo mngekutana na hoja kama--

Zitto 01.png


Hiyo ni mwaka 2016! Hapo tunaona Zitto yule yule anayeambiwa anaipinga Israel kwa kusukumwa na udini, hapo tunaona alipinga ujio wa Mflame wa Morocco ambae wana-share dini!!

Hiyo ni mwaka 2016 lakini wiki iliyopita tu hapa, Gazeti la Mwananchi la May 24, 2018 limeripoti kwamba:
Kwa upande wake, Zitto alipinga Tanzania kufungua ubalozi Israel na kurudisha uhusiano na Morocco kwa maelezo kuwa nchi hizo zimekuwa zikikandamiza nchi zingine.
Kumbe, hata baada ya miezi 20 baadae, bado Zitto anapinga Tanzania kurejesha uhusiano na taifa la Kiislamu kama anavyiopinga Israel kwa sababu zile zile... UKANDAMIZAJI! Sababu ambazo zilimfanya hata Mwalimu na mataifa kadhaa duniani kuvunja uhusiano na Israel pamoja na Afrika Kusini bila kusahau hiyo Morocco!

Baada ya kujiuliza maswali kuhusu hoja ya Zitto na kupata majibu, mngefahamu kwamba issue hapa sio UDINI kama mnavyodai bali ni IDEOLOGY na kusimamia unachokiamini!

Mara kwa mara Zitto amekuwa akijitanabaisha kwamba ni Mjamaa! Pekua makarabrasha ya uhusiano wa kimataifa na utakuta mataifa kadhaa ya kijamaa ya Latin America na Asia uhusiano wao na Israel ni wa tahadhali zaidi!

North Korea kwa mfano, wenyewe ndo hawalitambui kabisa taifa la Israel! Nadhani mpaka kesho, bado Cuba hawana uhusiano wa kibalozi na Israel! Bolivia na Venezuela sidhani kama wamesharudisha uhusiano wao na Israel tangu waubvunje almost 10 years ago!

Kwa upande wangu! Mimi ni Mwislamu sawa na majority ya Wapalestina! Lakini kama ilivyo kwa mwanadamu mungwana yeyote kutopenda ukandamiza, mimi pia napinga ukandamizaji wa Israel huko Palestine! Napinga si kwa sababu mimi ni Mwislamu bali napinga kama wanavyopinga Wakristo wengine wote duniani ambao hawasukumwi na udini katika kufikia maamuzi yao!!

Hata hivyo, mimi nasukumwa zaidi na fikra za kibepari kuliko za kijamaa!! Tofauti na Mjamaa ambae yupo tayari kupoteza fursa ili kumpigania mnyonge kama walivyokuwa wanafanya akina Nyerere, akina sie hatupo tayari kupoteza fursa!!

Tukikutana kwenye viunga vya UN tutapiga kelele dhidi ya taifa lolote linaloendesha ukandamizaji lakini huku tukihakikisha hatuziachi fursa zilizopo kwa huyo dhalimu!

Ni kutokana na hilo, ndio maana ni juzi tu hapa hivi ndivyo nilisema kuhusu Israel:
Ukishazi-profile hizi nchi ndipo pia utaangalia ni mabalozi na maofisa wa aina gani unatakiwa kuwapeleka huko!

Kama Israel is more worth economically than SADC, then, for international cooperation/ushirikiano wa kimataifa unaweka pembeni u-monster wake (but with caution) na kutoa priority ya masuala ya kibalozi kwa Israel over our SADC brothers!

Tutaendelea ku-maintain our relation/uhusiano with our SADC brothers kwa sababu undugu haufi.

Kinyume chake, tutawekeza nguvu zetu za Kidiplomasia kwa global monsters like Israel provided tunafahamu they're worthy economically na kuangalia ni maafisa wa aina gani tunatakiwa kuwa nao kule!!
Hivyo ndivyo siasa za kimataifa zinavyoenda na sio akina nyie kwamba ili mradi aliyeongea ni Mwislamu au Mkristo ndo basi mnataka kumfunga minyororo hapo hapo kwa sababu tu ya dini yake bila kuangalia misingi anayoisimamia!
 
Yan humu Luna watu akili zao zimejawa na udini na ukabila....sasa Saudi Arabia na Israel vinahusiana vipi na uislam na uikristo?He hoja ya Zitto imejikita kwenye hayo mtoa mada unayoyazungumzia au Zitto amejikita katika Sera ya nchi ya kuungana na wanyonge?
Mbona Zitto Huyo Huyo anapinga urafiki wetu na Morocco ambayo in typical Islamic state,mbona hapo hupaongelei au na wewe mbaguzi wa kidini?

Mimi ni mkristo lakini pia sikubaliani na inachokifanya Israel....hapo utasemaje?

Muwe mnafikiria muda mwengine siyo kuleta ubaguzi wenu na ukada wenu katika hoja za msingi.

ya israel ni ya kwao ss hayatuhusu.huko nyuma tulikuwa na ubalozi huko israel na wananchi wetu walikuwa wanaenda kuchota mambo mengi israel.SS leo tujifanye ati tunawasapoti palestina ati unamwacha israel that is stupid thinking.israel kwetu watz inamanufaa zaidi kuliko palestina halafu hizo siasa za ujamaa ziliishapitwa na wakati.we have now to consider economic advantage but not political advantage.ss tunajenga uchumi na ili uchumi wetu upae ni lazima tuwawekeze wananchi katika teknolojia.Israel wako mbali kiuchumi pia kiteknojia.hatuwezi poteza muda wetu ktk mambo ya kisiasa tunataka sasa kupalishwa uchumi wetu ili wananchi waweze faidika na ukuaji wa uchumi huo.palestina tutafaidika na nini.Maslahi kwanza mengine baadaye.
 
zitto aombe radhi, aepuke agenda za kidini, awe makini wakristo na marekani wanasupport Israel achange vema karata zake za siasa
 
ya israel ni ya kwao ss hayatuhusu.huko nyuma tulikuwa na ubalozi huko israel na wananchi wetu walikuwa wanaenda kuchota mambo mengi israel.SS leo tujifanye ati tunawasapoti palestina ati unamwacha israel that is stupid thinking.israel kwetu watz inamanufaa zaidi kuliko palestina halafu hizo siasa za ujamaa ziliishapitwa na wakati.we have now to consider economic advantage but not political advantage.ss tunajenga uchumi na ili uchumi wetu upae ni lazima tuwawekeze wananchi katika teknolojia.Israel wako mbali kiuchumi pia kiteknojia.hatuwezi poteza muda wetu ktk mambo ya kisiasa tunataka sasa kupalishwa uchumi wetu ili wananchi waweze faidika na ukuaji wa uchumi huo.palestina tutafaidika na nini.Maslahi kwanza mengine baadaye.
Agenda ni UKANDAMIZAJI....sio uchumi,sio ujamaa wala ubepari.Je tuuache ubinadamu wetu,utu wetu sababu uchumi?
 
Nyie watu mnatia aibu kishenzi kitu ambacho kinaonesha nyie ndio wadini wenyewe! Hoja za hovyo kabisa as if hamkwenda shule!

Zitto anaipinga Israel kwa sababu ya kuikalia Palestine!

Na sio Israel tu, pia anaipinga Morocco kwa sababu ya kuikalia Sahara Magharibi! Au Morocco nao ni Wakristo au Wayahudi?

Na hao Burundi wameikalia nchi gani?

Hiyo biashara ya utumwa huko Libya inafanywa na serikali au na magenge ya wahuni?!

Hivi ulishawahi kujishughulisha kufahamu hoja ya Zitto imetokea wapi au kwavile Zitto ni Mwislam ndo basi ukaamua kumhukumu kwa dini yake?!
Hapo sasa unachanganya kila kitu.ninachojua ni kua zito kalalamika kwamba sisi kama taifa tumeiacha sera ya kutetea wanyonge.ndio maana namshangaa hao wanyonge wapo israel tuu? Wapo hio moroco tu? Burundi hawapo? Syria ambako serikali inanyanyasa raia hakuna wanyonge? Kwanini achague wanyonge wakuwatetea? Jibu ni udini na unafiki.burundi kuna wanyonge; tanzania wapo wengi tuu.lakini zito ataacha kutetea waafrika wenzao anaenda kuitetea jerusalem ambayo ina jina la kiyahudi
 
Israel sio taifa la Kikristo, ni taifa la Kiyahudi, isipokuwa kwa wakristo ni kitu sensitive kupita unavyoelewa hivyo hata kulikabili unatakiwa kulikabili kwa uangalifu kwasababu linakwaza ukilihendo bila kuangalia hisia za wengine. Hata kama Israel sio wakristo, ujue wayahudi wanatumia Tora ambayo ni agano la kale kwenye biblia tunayotumia sisi wakristo, na zaidi sana, bila kuficha, sisi tunaamini mipaka ya ardhi ambayo Mungu alimpa Ibrahim ili Isaka na Yakobo(Israel) aje amiliki hadi ramani imechorwa kweney biblia kua hio ardhi wanayogombania ni ya wayahudi, Yesu alikuwa myahudi pamoja na kwamba baadaye wafuasi wake ambao ndio sisi tulikuja kujiita wakristo (wayesu) lakini ukweli ni kwamba dini yetu na ya wayahudi havitofautiani kabisa isipokuwa tu kwenye suala la Yesu(kristo). unachotakiwa kuelewa ni kwamba, wakristo wanamuamini Mungu wa Wayahudi/Mungu wa Israel, na Israel ndio ile pale unayotaka ubalozi usiwepo.

Yesu alikuwa Myahudi au Mkiristo?.
 
Nyerere alikuwa Muislamu alipovunja uhusiano na Israel?
Nauliza tuu, au alikuwa na sababu nyingine?

Ni mtu mshamba tuu anahusisha kila jambo na udini?
Nani amepinga ubalozi wetu Vatican?
Mwisho mtoa post aelewe Wayahudi sio Wakristo na sehemu kubwa ya historia ya Bwana Yesu Kristu ipi Palestine sio Israel.
Zitto na Mtoa mada wote ni wanazi wa madhahebu yao. Kwa msimamo wa Tanzania ya Nyerere kufungua ubalozi Israel na Morroco ni makosa.
 
Kama wakina Netanyahu sio wayahudi embu niambie wayahudi ni akina nani pale Middle East. Usikurupuke tu kama kimba la asubuhi mkuu
Hatimae nimegundua kumbe hapa mdini ni wewe na sio Zitto! Kumbe povu lote hili wala si kwa sababu ya maslahi ya Tanzania bali kwa sababu tu unaamini Israel ni taifa la Mungu!

Ngoja nikupe ilmu haidhuru hata kama utaendelea kuukumbatia ujinga kama ulivyofanya awali!

Mosi, kama nilivyosema kwenye post yangu hapo juu, binafsi naunga mkono uhusiano na Israel kwa sababu mimi ni bepari mnusa fursa!

Hata hivyo, kwa Mkristo kuiunga mkono Israel kwa sababu tu ya Ukristo wake ni jambo la aibu kwa sababu anaonesha wazi wala hafahamu anachokiunga mkono ni nini! Hawa ni wale Wakristo wasoma Bible huku wakiwa na uelewa finyu wa elimu ya dini/theology pamoja na elimu ya dunia

WHY?

KIIMANI, Israel ni taifa la KIYAHUDI kama ilivyo Saud Arabia kuwa taifa la Kiislamu!! Kwa imani/dini ya Kiyahudi

Ukristo ni dini ya Kishetani

Yesu Kristo ni Shetani!!!

Kwa kifupi, Ukristo unavyouchukulia Uislamu na watu wake ndivyo hivyo hivyo Uyahudi unavyouchukulia Ukristo na watu wake!!

On top of that, Uyahudi ni IMANI/Dini na pia ni ASILI/JAMII! Uhusiano wa Yesu Kristo na Israel ya sasa ni wa kijamii/kiasili na sio wa kiimani!

Wewe na Wakristo wote duniani ambao sio wa-Israel hawana uhusiano wowote wa kiimani na Israel kwa sababu, uhusiano wa Israel na Yesu Kristo sio wa kiimani bali ni wa kiasili! Wote ni wa asili ya Kiyahudi....

Wewe leo hii hata kama utakuwa ndio kiongozi wa Wakristo wote duniani bado asili yako haiwezi kuwa ya Kiyahudi sawa na Yesu na kinyume chake utabaki Mtanzania mwenye asili ya Afrika!!!

Kama lengo ni kuiunga mkono Israel Kiimani basi unatakiwa kubadili dini na kuwa Myahudi!

Hata hivyo, utakuwa Myahudi Kiimani tu na sio kiasili, kwa sababu, Kiasili, Myahudi ni yule ambae mama yake mzazni ni Myahudi!!

Kwa maana nyingine hautakuwa na uhusiano wowote na Yesu Kristo kwa sababu, kiimani, Yesu sio Myahudi na wewe hata kama imani yako itakuwa ni ya Kiyahudi, asili yako yako haiwezi kuwa ya Kiyahudi!

Yaani mnachokitolea povu hapa ni sawa na Saudi Arabia ingekuwa ni taifa la Kikristo halafu kila Saudi Arabia ikiguswa, Waislamu wawe wanatoa povu kwa sababu tu Muhammad alikuwa M-Saudi bila kujiuliza ikiwa uhusiano wao na Muhammad unatokana na u-Saudi Arabia wake au imani yake!!!
 
hakuna neno Palestina hata moja kwenye Bible, ila kuna Israel tangu kipindi cha Ibrahim hadi leo. ukweli huo hauwezi kufutika. Nyerere alikuwa anawaridhisha tu baadhi ya watu, na hiyo ilitukosti sana. kama kuna ubalozi wa iran, saudia hapa, kwanini ubalozi wa israel usiwepo?

Halafu, hivi unajua saudia na israel wapo kapu moja dhidi ya iran? saudia ana uhusiano mzuri na israel, sembuse tz ambayo ni masikini hata ikijifanya kuigomea israel hakuna madhara yoyote israel atapata?

Zitto siamini kama hakuna na element za kidini alipoongea ile hoja, amesahau kuwa kuna kundi kubwa sana la watz wanaisapoti israel na hao ndio atawaomba kura siku moja.

Israel wamefungua ubalozi hapa na sisi tukafungua kule, wamesema wanataka kurahisisha huduma, huduma gani? sisi wakristo huwa tunaenda kule kuhiji kama ninyi mnavyoenda meca....huduma hiyo na uhusiano huo ni wa muhimu sana kwetu.
Wewe ndio una upungafu wa kidini, kwani tulivyokuwa hatuna ubalozi Israel, wakristo wa kitanzania hawakuwa wanakwenda kuhiji huko? Na Je unaelewa yakuwa Waisrael sio Wakristo na Sio Waislamu? Je unatambua kuwa Wapalestina kuna Wakristo pia? Na je Unajua wakristo wakipalestina pia wanateswa na kuchukiwa na hao Waisrael ? Je unatambua kuwa mke wa marehemu Yasin Arafat aliyokuwa kiongozi wa wapalestina alikuwa ni mkristo ? Zito kasimamia haki za kisisa na si Udini, bali mambumbu kama nyie ndio mnatuletea udini hapa nchini, wewe ni shoga kabisa, mimi binafsi ni mkristo lakini sipendi na siwapendi baadhi ya Waisrael kwa ubaguzi na utesaji wanaoufanya.
 
Well.....hivi lakini,kwanini kila anayesimama anaitetea tu Palestine na siyo nchi nyengine ambazo uvunjivu wa haki nao upo kwa kiwango cha kutisha?{sina maana kutetea uovu naomba nieleweke}

Kuna nchi kama Somalia tena Waafrika wenzetu daily wanauwana,dini moja kabila sijui ni moja wale maana hawatofautiani but hakuna hata mmoja akasimama siku kutetea damu zinazomwagika kule,ningetegemea kuona watu wakipaza sauti kwamba balozi yao ifungwe hapa kwetu maana wameshindwa kusimamia haki lakini wapi!!!

Tuache kuwa biased ktk hili tuonyeshe utu wetu pale inapobidi.
Wewe umesikia wapi kuwa sisi Tanzania tuna ubalozi wa Somalia?
 
Back
Top Bottom