Ni faida gani Tanzania imepata tangu ianzishe uhusiano wa kidiplomasia na Israel?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Wakati kukiwa na suala la kuanzisha uhusiano na taifa la Israel, wengi walitoa maoni kwamba msimamo wa kiitikadi wa Tanzania ni kutoshirikiana na mataifa ambayo yanakandamiza jamii fulani ya watu na kukiuka haki zao za binadamu. Na hata tulisema kiitikadi tunaunga mkono jitihada za Wapalestina kuwa huru katika eneo lao, sambamba na azimio la Umoja wa Mataifa la kuwa na mataifa mawili katika lile eneo (two states solution).

Na watu walisema wazi kwamba linalofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina ni sawa na ilichofanya serikali ya makaburu dhidi ya wazalendo wa Afrika Kusini, na hivyo kama hatukukubali kuwa na uhusiano na serikali ya makaburu hatupaswi kuwa na uhusiano na serikali ya Israel ili kuwashinikiza kuwatendea haki Wapalestina.

Serikali ilibisha kwamba kulikuwa na sababu nzuri za kiuchumi kwa Tanzania kuwa na uhusiano wa kibalozi na Israel, na kwamba itakuwa rahisi kwetu hata kuchangia na kusisitiza juu ya haki za kibinadamu za Wapalestina ikiwa Israel watakuwa na ubalozi wao hapa nchini.

Sasa ningependa kujua, hadi sasa karibu miaka miwili baada ya kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Israel, ni faida zipi za kiuchumi tumepata? Na pili, wakati Wapalestina wakirusha makombora kwenda Israel na kuua watu 12, na Israel wakiwatwanga Wapelestina na kuuaa watu karibu 220 kutia ndani watoto 65 hivi, tulitumiaje kuwapo kwa ofisi za ubalozi za Israel nchini kusisitiza juu ya haki za kibinadamu na kukemea mauaji ya watoto na wanawake yaliyofanyika?
 
Nyerere aliwatetea wapalestina mpaka kuvunja uhusiano na Israel lakini bado mnamuita Laanatul Mchonga, kwahiyo sasa hivi hakuna anayejali.

Maana hakuna mwenye shukhrani.
 
Uhusiano na Wapalestina una manufaa gani kuanzia hapo.
Uhusiano na Palestina ni katika suala la sisi kuwa watu tunaojali utu wa mwanadamu, kama ilivyokuwa kwa Msumbiji, Namibia, Zimbabwe, Angola, South
 
Nyerere aliwatetea wapalestina mpaka kuvunja uhusiano na Israel lakini bado mnamuita Laanatul Mchonga, kwahiyo sasa hivi hakuna anayejali.

Maana hakuna mwenye shukhrani.
Tenda wema uende zako usingoje shukurani
 
Back
Top Bottom