Zitto Kabwe awasha moto Songea!

Zitto anawaambia ongea kwa uchungu sana na anasema hiv sasa hakuna mahali ambako mtoto wa tajir na maskini hawakutani sehemu yeyote ile wanayokutana.

Ndio sababu anasema "hajaitwa na wazee, ameitwa na changamoto na matatizo ya nchi kuutaka urais" huyu jamaa ni vile tu watu hawamuelewi, ana machungu sana na nchi hii
 
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe leo jioni alikuwa akiuunguruma Lizaboni Songea katika kampeni wa uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 1/4/2012. Katika hotuba yake mheshimiwa Zitto amewahakikishia wakazi wa Songea kuwa atahakikisha wafanyakazi wa TANESCO ambao wamekuwa na tabia ya kuiba mafuta ya jenereta za kuzalishia umeme wanachukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo ili kuondoa tatizo la umeme linaloukabili mji wa Songea na viunga vyake. Zitto amesema akiwa mwenyekiti hesabu za mashirika ya umma atashughulikia tatizo hilo kwa kufanya mambo mawili kwanza kwa kuwahoji kwanini umeme ukatike hovyo Songea? Pili matumizi ya mafuta yanatumikaje? Kisha baada ya hapo mtiti wake mtauona. Alisema kama ameweza kumshughulikia mkurugenzi wa TANESCO Tanzania, kwa Songea itakuwa ni kitu kidogo kwake.


Katika kuondoa kabisa tatizo la umeme katika mkoa wa Ruvuma amesema ujenzi wa mitambo mikubwa ya kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe inajengwa Mbinga yenye uwezo wakuzalisha megawati 120 na mji wa Songea utapata kilovoti 220 pia katika kufanya tatizo hili kuwa ndoto kabisa, mkoa wa Ruvuma utaunganishwa na gridi ya taifa kutoka Makambako mkoani Njombe.


Vilevile Zitto Kabwe ametoa onyo kali kwa IGP na RPC wa mkoa wa Ruvuma endapo wataendelea na mpango wao wa kutaka kumletea zengwe mgombea wa udiwani wa kata ya lizaboni kuwa anatuhuma zinazomkabili toka mwaka 1988, CHADEMA wameinasa barua waliyoandikiana wakuu hao wa jeshi la polisi. Zitto amehoji iweje tuhuma hizo zifumbiwe macho toka mwaka 1988 walikuwa wapi wakati mgombea huyo alivyokuwa kiongozi wa mtaa kwa vipindi viwili? Pia inasemekana katika barua hiyo diwani huyo anaundiwa zengwe linaloonesha kuwa yeye alikuwa anachochea waendesha pikipiki waandamane na kuleta fujo katika kipindi cha mauaji yaliyokea miezi michache iliyopita mjini hapa. Zitto amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji yaliyotokea na si kutishia raia. Katika kukomesha kabisa tabia hiyo inayotaka kufanywa na polisi Zitto ameahidi kuipeleka barua hiyo bungeni.


Ameongeza kusema kuwa jeshi la polisi linampango wa kuleta polisi wengine kutoka nje ya mkoa wa Ruvuma siku ya uchanguzi ili kuwadhibiti wananchi wa Lizaboni washindwe kupiga kura siku ya uchaguzi kwakuwa polisi wa Songea wengi ni CHADEMA.

picha za mkutanohuo zinapatikana songeayetu.blogspot.com
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Zitto awawashia Moto TANESCO Songea na Kutoa Onyo kwa IGP na RPC
Naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe leo jioni alikuwa akiuunguruma Lizaboni Songea katika kampeni wa uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 1/4/2012. Katika hotuba yake mheshimiwa Zitto amewahakikishia wakazi wa Songea kuwa atahakikisha wafanyakazi wa TANESCO ambao wamekuwa na tabia ya kuiba mafuta ya jenereta za kuzalishia umeme wanachukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo ili kuondoa tatizo la umeme linaloukabili mji wa Songea na viunga vyake. Zitto amesema akiwa mwenyekiti hesabu za mashirika ya umma atashughulikia tatizo hilo kwa kufanya mambo mawili kwanza kwa kuwahoji kwanini umeme ukatike hovyo Songea? Pili matumizi ya mafuta yanatumikaje? Kisha baada ya hapo mtiti wake mtauona. Alisema kama ameweza kumshughulikia mkurugenzi wa TANESCO Tanzania, kwa Songea itakuwa ni kitu kidogo kwake. Katika kuondoa kabisa tatizo la umeme katika mkoa wa Ruvuma amesema ujenzi wa mitambo mikubwa ya kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe inajengwa Mbinga yenye uwezo wakuzalisha megawati 120 na mji wa Songea utapata kilovoti 220 pia katika kufanya tatizo hili kuwa ndoto kabisa, mkoa wa Ruvuma utaunganishwa na gridi ya taifa kutoka Makambako mkoani Njombe. Vilevile Zitto Kabwe ametoa onyo kali kwa IGP na RPC wa mkoa wa Ruvuma endapo wataendelea na mpango wao wa kutaka kumletea zengwe mgombea wa udiwani wa kata ya lizaboni kuwa anatuhuma zinazomkabili toka mwaka 1988, CHADEMA wameinasa barua waliyoandikiana wakuu hao wa jeshi la polisi. Zitto amehoji iweje tuhuma hizo zifumbiwe macho toka mwaka 1988 walikuwa wapi wakati mgombea huyo alivyokuwa kiongozi wa mtaa kwa vipindi viwili? Pia inasemekana katika barua hiyo diwani huyo anaundiwa zengwe linaloonesha kuwa yeye alikuwa anachochea waendesha pikipiki waandamane na kuleta fujo katika kipindi cha mauaji yaliyokea miezi michache iliyopita mjini hapa. Zitto amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji yaliyotokea na si kutishia raia. Katika kukomesha kabisa tabia hiyo inayotaka kufanywa na polisi Zitto ameahidi kuipeleka barua hiyo bungeni. Ameongeza kusema kuwa jeshi la polisi linampango wa kuleta polisi wengine kutoka nje ya mkoa wa Ruvuma siku ya uchanguzi ili kuwadhibiti wananchi wa Lizaboni washindwe kupiga kura siku ya uchaguzi kwakuwa polisi wa Songea wengi ni CHADEMA.
 
Back
Top Bottom