.Just thinking aloud!!
Hivi kama baba mwenye nyumba akialika wageni (bila kujali rangi au asili yao) waje nyumbani kwake kisha akawaruhusu waingie ndani ya nyumba yake na wawe huru kuchukua au kufanya kitu chochote watakachoona kina manufaa kwao ni halafu wale wageni wakaiba pesa na kubaka watoto ni nani wa kulaumiwa? Ni baba mwenye nyumba au ni wale wageni aliowaalika na kuwapa ruksa ya kuingia popote wanapotaka na kufanya chochote wanachoona kinafaa?
Hivi baba au mama mwenye nyumba akichukua raslimali ya nyumbani kwake akaipeleka nje (iwe kwa nyumba ndogo, kidumu au popote anapojua yeye) na kuiacha familia yake ikiwa maskini haina msaada ni nani wa kulaumiwa? Ni mwenye nyumba au wale wanaopelekewa mali ili watumie na zinazobaki waendeleze majumbani kwao?
Nadhani imefika wakati waafrika tukaacha kutafuta mchawi nje ya nchi na kuelewa ule msemo wa wahenga kuwa kikulacho ki nguoni mwako.
Kila dola inayoondolewa afrika ama ina baraka ya waafrika walioteuliwa kuwawakilisha wenzao kusimamia raslimali za nchi zao au inatoroshwa na hawa wawakilishi wenyewe na kupelekwa kwa wazungu, waarabu, wachina, etc. Tuache kupoteza muda wetu kutafuta wachawi ulaya, amerika na bara hindi wachawi wetu wapo humu humu nchini.
Namsubiri Kiongozi wa Kwanza mwenye akili. Atakayehamasisha Watanzania wachange tusenti twao (wa alfu moja, mbili, tano, kumi, n.k) kuwa mtaji wa uwekazaji katika nyanja watakaichagua kuliko huu upumbafu wa kuandika kwenye karatasi/mitandao, kusoma kwenye Podium/iPad, kuwaponda wazungu majukwaani alafu ukishuka unakwenda kuwaomba misaada!
Tuliwahi kuchangishwa tukaanzisha NICO. Vihela vyetu vikaishiwa kuliwa na akina Mosha yule CTI & Co.
watanzania tuwe wazuri wa kumpa mtu sifa yake kama tulivyowazuri wa kubeza.alichokifanya zitto kabwe ni udhubutu ambao wengine tumeshindwa.jamani mnyonge ,mnyongeni lakini haki yake mpeni! Hongera zitto kabwe!
safi sana zito hakika hakuna kama zito ndani ya chadema yupo makini sana sana
MHIMBIMBILI nieneo baya sana na zuri sana,Kunawakati utakutana na watu wanalia sana,Kunawakati utakutana na nyuso za furaha.Uporaji? We Zitto acha unafiki! Ni nani mporaji kati ya viongozi wetu na wazungu? Mfano rafiki yako Idrisa alipopora fedha za rada mbona hukupiga kelele! Na huyo katibu wa chama chako cha magamba kinachokupa kichwa anapopora meno ya tembo mbona hupigi kelele? Na mtoto wa huyo rais wako anayekupa kichwa anapopora mbona hupigi kelele. By the way kwani wazungu hutushikia bunduki? Mikataba kama ile ya madini si nyie mliipitia?
If therein is anything to salute ZZK, you will then need to salute many ****** in town.
zitto ni mzalendo,mtiifu,mwelewwa,msomi,jasiri n.k kawa taifa hili anazungumza mambo kitaifa na si kwa misingi ya uchadema na ccm.zitto amekuwa jasiri kuwaeleza wazungu maovu na hila wanazotumia kuzipata raslimali za africa. Ni viongozi wangapi wenye ujasiri wa kufanya hivyo? Wengi wa viongozi wetu wamebaki ni vibaraka wa wazungu na husifia hata vile visivyikuwepo, na kusisitiza ushirikiano usio na tija, ushirikiano wakinyonyaji! Ushirikiano wa bwana na mtwana nuawezekana? Hongera zitto!
katika mijadala ya asubuhi ya kituo cha televisheni cha startv jumapili iliyopita, wageni waalikwa katika mjadala ule walimulalamikia mh.zitto kwa kukurupusha hoja ambazo anashindwa kuzisimamia.kudhibitisha hili ni kuwa katika bunge lililopita alisema atawataja walioficha pesa uswizi kama serikali haitawataja lakini wiki mbili zilizopita mh. Zitto amesikika kupitia startv hiyohiyo kuwa hatawataja.
Hatujakaa sawa anaibuka na habari za kuwalaumu wazungu kwa wizi. Njia bora ilikuwa mh. Zitto anahakikisha tunajisafisha sisi kwanza kwa kuwashughulikia wezi tunaowajua na kuziba mianya ya wizi kama mh.zitto alivyokuwa amenuia huko bungeni ndipo sote kwa pamoja tuwageukie wazungu wezi.
Kitendo hiki cha mh.zitto kuwarukia wazungu wakati hili la kuwashughulikia wezi wa ndani kinatoa tafsiri mbaya sana juu yake juu nia aliyokuwa nayo kuhusu tuhuma alizozitoa bungeni za pesa za wizi zilizofichwa uswisi, binafsi naona zitto anataka kutumia mwanya huu wa kuwashambuliwa wazungu kufifisha suala zima alililojiapiza kushiriki kulikabili yaani suala la watanzania kuficha pesa za wizi uswisi na kwingineko.
Zitto kuruka ruka na hoja ambazo azisimamii bado anazidi kudororesha imani ya raia wa tanzania kuwaamini vijana katika shughuli za kuikwamua nchi yetu kutoka kwenye lindi la matatizo mengi ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kadhalika.
Kwa mara nyingine namtahadharisha zitto aache mtindo wake huu wa kudidimiza nia ya watanzania ya kuwaamini vijana kuwa na uwezo wa kukwamua nchi yao kwani yeye bado anabeba taswira ya mwanasiasa kijana. Kama hawezi kujirekebisha basi ajiuzulu masuala yote ya siasa na aendelea na shughuli zake nyingine.
---mpigakelele
ungekuwa mwanachama wa chadema ningekupa kazi ya kusafisha washroom ya katibu mkuu kila siku.
Kwa sbabu ni mwana ccm ambaye akili zako na upembuzi wa mambo umejikita kwenye hasira dhidi ya viongozi wa chadema hasa wale wanaotetea haki za watanzania nakupandisha cheo kuanzia leo wewe ni houseboy wa kudumu wa nape nauye
zitto sio level yako,zitto hajawahi shindwa jambo.zitto anafocus mbali kwa manufaa ya taifa
U a mong them!!!Inakuuma sana Kamanda kuona Unaitwa Mgambo..Zitto anaitawa FBI.
Jitahidi sana labda ipo siku nawewe huyo babu ataipigiwa salute
Kweli maji hufuata mkondo. Zito ananikumbusha Jakaya alivyokwenda South Africa akakurupuka eti wazungu watulipe kama fidia ya biashara ya utumwa. Jamaa akawa hata hajui ni sehemu gani ya Tanzania ambako wazungu walikuja kuchukua watumwa. Alionekana kama katoka pangoni. Kwa nini hawa watu wanakosa ujasiri wa kuhoji Waarabu waliojizolea watumwa lukuki Africa na kwenda kuwaua kikatili huko kwao?
Haki huokoa Taifa. Achieni upendeleo. Mzani wa haki humpendeza Mungu. Kuwadai wazungu na kuwaacha mataifa mengine kama waarabu na mafisadi wa ndani ni dalili za chuki binafsi dhidi ya Wazungu na kutokuwa na nia ya dhati ya kukomboa taifa.
Hakuna haja na sababu za kujificha! anzisha wewe na sisi Great thinkers tuko tayari kujadili hoja zako lakini ziwe na source...!