Zitto Kabwe ataka Rais Zuma aondolewe madarakani mara moja

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondolewe kwenye nafasi ya Urais mara moja hata wiki hii.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii kufuatia uchaguzi wa Chama Cha ANC cha nchini Afrika Kusini ambapo walikuwa wakifanya uchaguzi kuchagua Rais na Makamu wake ndani ya chama.

"Jumatatu (leo) tutakuwa na Rais mpya wa Chama cha ANC. Kura zinapigwa hivi sasa huko Johannesburg. Ingawa nina ukakasi na Cyril Ramaphosa kuhusu Marikana, ninaunga mkono yeye kushinda na Makamu wake awe Lindiwe Sisulu. Pia Zuma aondolewe Urais mara moja baada ya wiki inayoanza kesho (leo)" aliandika Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa ushindani wa uchaguzi wa ANC ni funzo kubwa kwa vyama vya siasa kuhusu Demokrasia ya ndani ya vyama hivyo.

"Uongozi imara wa Afrika Kusini ni muhimu sana kwa SADC na AU. Ushindani mkali wa Uchaguzi wa ANC ni funzo kubwa kwa vyama vyetu kuhusu Demokrasia ya ndani" aliandika Zitto Kabwe

EATV
 
Zitto ni nani mpaka atake Zuma aondolewe urais Afrika kusini
 
Zitto bana. Yeye alijipa cheo kinachoitwa ''kiongozi MKUU wa Chama'', aliye juu ya Mwenyekiti wa Chama bila uchaguzi wowote na hauoni huo unkurunzinza wake. Zuma hawezi kuondolewa ''urais mara moja'' kizembe hivyo.
 
Amalizane Kwanza Na Anko Magu Huko Alikoparamia Wabunge Wa Huko Walitosha Wenyewe Tu Kwa Zuma
 
JPM ni noma sana. Zitto kapelekwa maboya kabisa anaanza kuongea siasa za S.A hapa Tz kupata kiki.
Hayari sana.
 
Zito kaishiwa pumzi kila Siku anashinda mitandaoni,ofiyake haina chakufanya? tumekuchoka hunajipya,2020 hatukupi ubunge ukatafute udiwañi kijijini kwenu.yakwenu yamekushinda unaingilia yajirani,tena ukome.
 
Z , zi, mwanangu,,,,, sauti ya baba yake Z ilisikika kutoka chumbani Mzee akiwa anakaribia kuaga dunia... Mwanangu, urithi huu kwako,,, usiongee ongeeee ovyo ovyo na daima tathimini sana unayotaka kuyasema... Baki salama kijana.... Mzee, Akakata roho.

Ila Z, tangia ahitimu chuo na kujiunga kwenye siasa anafanya tofauti kabisa na wosia wa Mzee wake aliouacha.

Any way, Z yuko hivyo akili humrudia na ghafula akili zote humtoka.

Kama hapa, naona akili zimeenda ziwa Tanganyika kupunga upepo.
 
Dah..inadikitidha knoma hadi inafurahisha..akili zmeenda kupunga upepo[emoji23] [emoji23]
 
Nlpoona zito nkajua atakua rai wa sauz kmbe ni another comedy
 
Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondolewe kwenye nafasi ya Urais mara moja hata wiki hii.

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii kufuatia uchaguzi wa Chama Cha ANC cha nchini Afrika Kusini ambapo walikuwa wakifanya uchaguzi kuchagua Rais na Makamu wake ndani ya chama.

"Jumatatu (leo) tutakuwa na Rais mpya wa Chama cha ANC. Kura zinapigwa hivi sasa huko Johannesburg. Ingawa nina ukakasi na Cyril Ramaphosa kuhusu Marikana, ninaunga mkono yeye kushinda na Makamu wake awe Lindiwe Sisulu. Pia Zuma aondolewe Urais mara moja baada ya wiki inayoanza kesho (leo)" aliandika Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa ushindani wa uchaguzi wa ANC ni funzo kubwa kwa vyama vya siasa kuhusu Demokrasia ya ndani ya vyama hivyo.

"Uongozi imara wa Afrika Kusini ni muhimu sana kwa SADC na AU. Ushindani mkali wa Uchaguzi wa ANC ni funzo kubwa kwa vyama vyetu kuhusu Demokrasia ya ndani" aliandika Zitto Kabwe

EATV
Hii ameiandika akinywa balimi
 
Back
Top Bottom