Zitto Kabwe alimaanisha hivi..

Zitto Kabwe alimaanisha hivi..

Mpangawangu

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
887
Reaction score
965
Zitto alikuwa kamchapa Spika Kiufundi

Ilikuwa hivi;Bunge lilifikia ukomo wa mjadala na kutakiwa kufanya maamuzi.

Wakawa wanatafuta lugha gani ikitumika haitaonyesha Bunge kuingilia Mihimili mingine kama Serikali na Mahakama.

Walipofika kumuwajibisha Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini mvutano ukawa mkali.

Ndipo Spika akamteua Chenge atoe mchango wake.

Chenge akasema.

"Bunge linapendekeza Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Kichukuliwa hatua na Mamlaka za uteuzi"

Wabunge wengi hasa wa upinzani hawakuridhishwa si tu na maelezo hayo bali hawakuwa na imani hata na alie kuwa anayatoa maana yeye ndio KUBWA LA MAADUI,ndipo Spika alipo Mtaja Mh Zitto ambae kwa karibu sana alikuwa akishauriana na Halima Mdee.

Ndipo Zitto akasema

"Nashauri tuikubali sentensi(maelezo)iliyosema na Mh chenge itumike kwa mapendekezo ya kamati yaliyobaki.

Kimbuka pendekezo hilo lilikuwa pendekezo nambari saba.

Pendekezo namba 8,9...yalihusu kuwajibishwa Masele,Muhongo,na Pinda.

Spika kwa kutokukua mtego wa Zitto uliolenga Mamlaka ya uteuzi imuwajibishe mpaka waziri mkuu ambae Spika amejipanga kumlinda kwa nguvu zote,

Spika akaona apige kura haraka haraka,kama kawaida ccm wakasema Ndiyoooo......

Punde tu Ole Sendeka ambae nae anataka wote wawajibike isipokuwa Pinda na Masele akashtuka na kumjulisha Spika haraka,wakati huo wapinzani karibu wote walikuwa wakilalamika kwa Spika kupigisha kura haraka haraka isipokuwa WENJE.

Ndipo Spika akagutuka na kurudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa kipendekeza kwa kila mmoja

Wenje akaanza kumzonga Spika kuwa tumeshafanya maamuzi,na Maamuzi yalikuwa ni Ndiyo hivyo Spika asimamie maamuzi ya wabunge.

Hivi ndivyo Zitto alivyokuwa kamaliza Mchezo kirahisi kwa wale waliomuelewa,lkn wengi hawakumwelewa alichokimanisha.

Pamoja na hayo bado wote kwa umoja wetu hatupaswi kuondoka kwenye hoja ya msingi ambayo nikuona wezi wanawajibika.

Kesho Bunge litaendelea saa tatu asubuhi.
 
chenge kasema " mamlaka ya uteuzi iwachukulie hatua zinazostahili". ilikuwa kauli ya kijanja. wabunge wengi walikuwa wanapinga serikali kwenda kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa. kwakusema zinazostahili unakuwa unaipa serikalli uwanja wakufanya mambo mengi ikiwemo kuwachunguza. na nchi ilivyo uchaguzi mkuu ungefika uchunguzi bado unaendelea. kwa namna fulani zito kaokoa.
lakini makinda asingetengua uamuzi zito alikuwa anatuzika maana wakina muhongo, werema na hata pinda wangeenda kuchukuliwa hatua wanazostahili ikiwemo kuchunguzwa tena, kuhamishwa, kusafishwa au kusamehewa.
 
msimamo wa kukataa kuburuzwa ndio mzuri. tungekubaliana na maoni ya zitto, utekelezaje usingefanyika...wezi wote wangesafishwa sawia!
 
Zitto alikuwa kamchapa Spika Kiufundi

Ilikuwa hivi;Bunge lilifikia ukomo wa mjadala na kutakiwa kufanya maamuzi.

Wakawa wanatafuta lugha gani ikitumika haitaonyesha Bunge kuingilia Mihimili mingine kama Serikali na Mahakama.

Walipofika kumuwajibisha Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini mvutano ukawa mkali.

Ndipo Spika akamteua Chenge atoe mchango wake.

Chenge akasema.

"Bunge linapendekeza Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Kichukuliwa hatua na Mamlaka za uteuzi"

Wabunge wengi hasa wa upinzani hawakuridhishwa si tu na maelezo hayo bali hawakuwa na imani hata na alie kuwa anayatoa maana yeye ndio KUBWA LA MAADUI,ndipo Spika alipo Mtaja Mh Zitto ambae kwa karibu sana alikuwa akishauriana na Halima Mdee.

Ndipo Zitto akasema

"Nashauri tuikubali sentensi(maelezo)iliyosema na Mh chenge itumike kwa mapendekezo ya kamati yaliyobaki.

Kimbuka pendekezo hilo lilikuwa pendekezo nambari saba.

Pendekezo namba 8,9...yalihusu kuwajibishwa Masele,Muhongo,na Pinda.

Spika kwa kutokukua mtego wa Zitto uliolenga Mamlaka ya uteuzi imuwajibishe mpaka waziri mkuu ambae Spika amejipanga kumlinda kwa nguvu zote,

Spika akaona apige kura haraka haraka,kama kawaida ccm wakasema Ndiyoooo......

Punde tu Ole Sendeka ambae nae anataka wote wawajibike isipokuwa Pinda na Masele akashtuka na kumjulisha Spika haraka,wakati huo wapinzani karibu wote walikuwa wakilalamika kwa Spika kupigisha kura haraka haraka isipokuwa WENJE.

Ndipo Spika akagutuka na kurudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa kipendekeza kwa kila mmoja

Wenje akaanza kumzonga Spika kuwa tumeshafanya maamuzi,na Maamuzi yalikuwa ni Ndiyo hivyo Spika asimamie maamuzi ya wabunge.

Hivi ndivyo Zitto alivyokuwa kamaliza Mchezo kirahisi kwa wale waliomuelewa,lkn wengi hawakumwelewa alichokimanisha.

Pamoja na hayo bado wote kwa umoja wetu hatupaswi kuondoka kwenye hoja ya msingi ambayo nikuona wezi wanawajibika.

Kesho Bunge litaendelea saa tatu asubuhi.
kesho makinda akisema maelezo ya mapendekezo ya PAC yatamletea shida na serikali inabidi aseme ni kwa jinsi gani na siyo tu kung'ang'ana. pia kusema serikali ikawachukulie watuhumiwa hatua zinazostahili sio ushauri. bunge lishauri lenyewe linaona watuhumiwa wanastahili adhabu gani?
 
msimamo wa kukataa kuburuzwa ndio mzuri. tungekubaliana na maoni ya zitto, utekelezaje usingefanyika...wezi wote wangesafishwa sawia!
pengine zito alijua akifanya vile watamnasa na PM, kumbe kwa kutaka samaki wakubwa tungepoteza hata wadogo. ilikuwa move hatari sana.
 
Kwa hiyo unataka kusema Chenge alikua amaipeleka Serikali yake machinjioni.?

Hapo hamna maamuzi yoyote ambayo yangefanyika zaidi ya kuambiwa Rais bado anaumwa tusubirie apone.

Zitto aliona Chenge anvyopendekeza karibia Bunge Zima linamwelewa kwa maana linakubaliana na maoni yake.

Hivi unafikiri Kikwete yupo tayari kuwawajibisha hao watendaji wake wakati na yeye ni sehemu ya Dili.?

Pac ilitoa mapendekezo mazito, ila zitto aliona karibia yote yanaenda kuchakachuliwa ndio maana akasema akili imechoka.

Maana aliyoyatarijia yote yalikua yanaenda kuwa kazi bure.

Mbowe aliona kijana amekata tamaa akaamua atumie akili ya Ziada kuliko kuwa sehemu ya madudu ya CCM.
 
Asante kwa ufafanuzi kwa kweli hata mimi pale alinichanganya manake action and reaction ilikuwa in split seconds..
 
Zitto hapo alikua kateleza ndiyo maana akajistukia na kudai kwamba anajua wapo ambao hawakupendezwa na kauli yake na hivyo hataweza kuchangia tena kwani amechoka.
 
Mhe Zitto kweli hakuwa sahihi pale alipokubaliana na wezi kwa kuikubali formulation ya Chenge, ambayo msingi wake mawaziri hao, mwanasheria wa serikali na katibu wa nishati na madini kwamba mamlaka ya rais iamue hatima yao.
Zitto kabla ya kulidhiria hilo la chenge tukumbuke aliwashika kooni hao wezi wanaoteteana kwa kauli zake kali za kuwataka wezi wawajibishwe.
Kilichompelekea Mhe Zitto uenda nahisi hao wezi labda walimtishia maisha kwanini anataka kuleta mahafa makubwa zaidi kwao, hivyo Zitto akalegeza uzi mamlaka ya uteuzi iwachukulie hatua zinazostahili na sio kukubali Bunge limtake raisi awawajibishe.
Ushauri wangu kwa zitto hasilegeze uzi kwa hao wezi, kaza buti Fedha zetu zirudi, hata ikibidi watu kufilisiwa na ikiwa hivyo unarudisha imani kwa wananchi na kukufanya umalize mwaka vizuri.
 
Hili liko wazi sana, alivyosimama Chenge nilimuona at that time alipewa muda wa kuongea Wenje then baadae akaja Chenge akaongea aliyoyaongea ngoma ikasapotiwa kiCCM then zitto akamaliza short n'clear.
Kuanzia mwanzo wabunge wa CCM walikuwa wanakataa katibu mkuu kujiuzulu ili mambo mengine yaendelee sasa alichoongea Chenge na kikakubalika kiCCM ndiyo hichohicho kingeendelea kwa Sos, Werema na Pinda.
Zitto akaona huu ni ujinga kumbe waizi wanateteana mpaka bungeni, wacha wateteane
 
kwa namna escrow ilivoleta mafanikio kwa kijana zzk hakika chadema haina budi kumrudisha kundini na imethibitika tu pale baba wa zito kisiasa mh mbowe alipoona mwanae anasema akil imechoka bila hayana alisimama na kumpigania jahaz lisizame welcom home again mh zito its cdm mzee
 
mimi nilimwelewa hiyo kuwa ccm wangeuziwa mbuzi ndani ya gunia hata na hivyo nafurahi sana kumuona ZZK ndani ya UKAWA kiukweli mwakani ukawa wanachukua nchi
 
huyu Zitto kabwe ni fundi sana namkubali sana lkn chonde chonde usirudi chadema wamekudhalilisha sana wakasusa msiba wa mama yako achana nao
 
mimi nilimwelewa hiyo kuwa ccm wangeuziwa mbuzi ndani ya gunia hata na hivyo nafurahi sana kumuona ZZK ndani ya UKAWA kiukweli mwakani ukawa wanachukua nchi

kiukweli jamaa ni muhimu sana kwana ana uwezo wa kushawishi, ila wawe nae makini kiac! lakn kama watayamaliza na akiwa ndani ya ukawa sina shaka ccm watapata wakati mgumu sana!
 
huyu Zitto kabwe ni fundi sana namkubali sana lkn chonde chonde usirudi chadema wamekudhalilisha sana wakasusa msiba wa mama yako achana nao

Kaka siasa ndivyo zilivyo. Ni unafiki mwanzo mwisho. Hiyo migogoro ndo imeisha hivyo na utawaona wakienda naye ikulu kwa prezdaa kunywa juisi. Hapo aibu inabaki kwa wapambe akina NGURUV3,MCHAMBUZI,YERIKO, BEN SAA8 and Co. Tehteteteteh.
 
Back
Top Bottom