Zitto, imetosha sasa

Tujadili mustakabali wa taifa letu,tuachane na Zitto,anatupotezea muda,kwake uzalendo ulitoka ck nyingi,
 
Analyst kweli nimekukubali jinsi ulivyo jaribu kumuonya huyu kijana, lakini waswahili husema sikio la kufa halisikii dawa!!!!!!!
Kama anasikia ajilekebishe maana kweli Mungu atamudhibu kwa kuwa laghai na mnafiki. Anapandia migongo ya wanyonge kisha anawasaliti kwa fedha za kina RA na LE, kwa Mungu yote yako wazi, njia ya mwongo ni fupi!!!!!!
 
yaani kwa sasa utadhani Zitto ni waziri na Januari ni Naibu waziri.........halafu ngeleja ndo mmoja wa mawakala wa wizara
 


wewe ni muongo mkubwa sana humu janvini na unatumia ID mbili ambazo ni Tanleaks na hii nssf damu....jana umetuletea uongo wa hali ya juu kabisa kuwa magufuri ameachia uwaziri....na umejiunga siku moja tar 11 march 2011...huna hoja za msingi....tunakuomba ukome kuleta uongo wako humu
 
Mie naona mnapoteza nguvu zenu.Zitto ni mtu mzima wewe unapomkalisha chini ujue just unampa ushauri tu, na ana haki ya kuuchukua au kuachana nao na hasa utakapo mpa ushauri wa kipuuzi kwake. wewe unayemsema zitto ulimchagua? Zitto hawezi babaishwa na maneno yako kwani hukumchagua. Na hizo dhana zako kuwa anakula pesa za mafisadi ni dhana ambazo akikuomba ushahidi hutotoa. Au wewe kwa akili yako unadhani kwa vile Zitto yupo CDm basi ndio asiwe na uhusiano binafsi na RA au Jk, acha fikra hizo, au nawe upo kwenye kundi la wale wanaodhani kuwa chama cha upinzani basi uwe adui na wafuasi wa chama kilichopo madarakani? ebu flash hizo fikra zako mkuu.
 
Mh Zitto

Zingatia mawazo ya watu unakoelekea siko ebu rudisha akili zako nyuma kuwa kama zitto wa zamani

Hivi mnambembeleza wa nini?kama kaamua kufuata mkondo huo achaneni nae,tatizo humu ndani kuna watu wanampenda huyu kijana(zitto) kupita kiasi,nashukuru kidogo sasa wanajamii wengi mmeanza kuuelewa upande wa pili wa Zitto mwaka juzi mpaka mwanzoni mwa mwaka jana ilikua ukimzungumzia zitto negative side unashambuliwa mpaka unajuta kuifahamu hii forum,wenye kumbu kumbu nzuri nadhani mnakumbuka mhariri wa gazeti la kulikoni enzi hizo alivyoshambuliwa na mashabiki wa zitto kwa kuandika upande wa pili wa (-ve) wa zitto akimhusisha na haya madudu mnayomuona nayo leo.

"Mwanangu si msikivu" Haya ni maneno ya Bi.Shida mama mzazi wa Zitto,sasa nyie mnaombembeleza hamuoni kwamba mnajaribu kumpigia mbuzi gitaa ili acheze?aah sijui bwana labda atacheza siku moja,mimi kamwe simlilii zitto.
 
Huyu dogo anataka kutuletea ya Gagbo nini??????? Akaulize huko Ivory Cost watapelekana The Hague!!!!!!!! Mwenye macho haambiwi tazama!!!!!!
WATU WAMECHOKA ULAGHAI NA UJINGA!!!!
 
Kazi ipo, ngoja mi nielendelee kuchapa kazi kwani si Zitto wala Jk wala hata Dr. Slaa mwenye jibu la matatizo yangu. Naamini wote wanapiga porojo kwa ajiri ya matumbo yao, familia zao na watu wao wa karibu. Sioni katika hawa mzalendo wa ukweli na mwenye uchungu hata wa kumkaribia Mwl. JK Nyerere (RIP)
 

Mkuu samahani hapo nilikuwa nampa ushauri zitto, siwezi kumbembeleza zitto hata kidogo maana amekuwa ndumilakuwili:smash::smash:
 

Sikubaliani na wewe, Ushauri wangu, kama ameshindikana tupa nje aende kwa anaowajali zaidi ya sisi wapigakura
 
Tatizo la haya mashirika kumejaa ufisadi uliokithiri na wanachama hawafaidiki na haya mashirika. Kuwekeza kwao ni kwa faida ya nani wakati wanachama hawafaidiki na uwekezaji unaofanywa na hayo mashirika?
Hivi Kiwira kununuliwa na NSSF kuna tatizo lipi? au Kiwira ibaki ikijifia bila mtaji na wapewe wawekezaji wa nje bila ubia na Taasisi au mashirika ya ki Tanzania ndio vyema?

Nawashangaa sana wanaoona kuwa NSSF haipaswi kuwekeza Kiwira.
 
Inaelekea Taifa- Kwanza huifahamu mifuko hii ya hifadhi ya jamii kwa undani.PPF walisimamisha kulipa baadhi ya pensheni kutoka na ukata, halikadhalika PSPF kutokana na upungufu wa michango inapata ruzuku ya serikali.
NSSF kupewa kiwira itaanzisha kampuni tanzu ambayo itatoa ajira na kulipa madeni.Fedha zinazokusanywa na NSSF ni nyingi na mabenki hayatoi riba ya kutosha kukidhi haja ili mafao yaboreshwe, I stand to be corrected.
 
Kutokana na michango mbali mbali iliyotolewa kwenye thread hii inaonekana wazi tunacho chama kimoja tu cha upinzani kati ya vyama vilivyopo bungeni, nacho ni CDM, vinavyobaki vyots ni matawi ya CCM, kwa viwango tofauti. Katika hali hiyo kuna umuimu wa kufanya kila linalowezekana kuinusuru CDM kama chama pekee cha upinzani hapa nchini.
 

Tatizo la Tanzania sasa hivi kila analysis ya jambo haifanywi tena objectively bali watu wanaangalia personalities zilizomo.Nani kasema nini, nani anatoka dini gani! TUTAFIKISHWA PABAYA KAMA SCOPE NA LENSE OF ANALYSING THINGS ITAKUWA NI DINI/UDINI! Pamoja na kwamba sijafuatilia sana huu mjadala nimeona watu humu wakiuliza " kwanini watu wanapinga NSSF kwanini hawaangaliii pia PPF!" Cha ajabu, PPF haijajikita kutaka kufua umeme! Utalinganisha vipi? Tuache huu mtizamo una bore sana.Tuangalie jambo lililopo tulijadili kitaalamu zaidi bila kujali nani yumo ndani ya taasisi.
 
Zitto your good time has gone....

NSSF wanaweka pesa za wananchi maskini, je umefikiria % risk kwenye huo uwekezaji? je mmetushirikisha na sisi wadau (wachangiaji wa mfuko huu) au nyie ndiyo mnatuamulia mnachotaka?

Hii mifuko si ya kuchezea chezea please!!
 



Hamna mtu anaangalia nani yuko ndani ya taasisi

linalozungumzwa ni mfumo wa muundo na utendaji wa NSSF

unajua nssf wanaidai kiwira mabilioni ya hela ambazo hata hawajui watazipataje?

unajua nssf wanaidai kagera sugar mabilioni ambazo hawajui watazipataje?

unajua nssf ndio waliifunga hospitali ya THI hospital ambayo ilikua ya kwanza kutoa huduma za moyo hapa tz? waliangalia umuhimu wa hii hospital kabla ya kuifunga au walifuata amri za kijinga za wanasiasa wachache wasiojua hata kwa nini wako kwenye ofisi za uma?

nssf na mradi wa kigamboni bridge wamefikia wapi?

hizi hela zetu wanazotaka kuinvest kwenye nishati je sisi kama wanachama na wadau wa nssf ambao ndio wenye hela tunafaidika vipi?
shirika halijasimama lenyewe linafanya kazi kwa maamuzi ya kichama na serikali:smash:
 
Kumekuwepo na watu fulani, pengine kwa itikadi zao, au kwa makusudi fulani wamekuwa wakitumia vyombo vya habari, na zaidi JF kumchafua Zitto bila sababu zilizo wazi.
Kwa ufupi ni kuwa wamekuwa wakimchonganisha Zitto na wanaCHADEMA na wananchi kwa ujumla. Wamekuwa wakitumia reference za baadhi ya misimamo ya Zitto, kama kisingizio cha kumchafua. Wamekuwa wakimhusisha bila ushahidi wowote, na mafisadi, na ufisadi. Wamekuwa wakimhusisha vibaya na TISS bila ushahidi wowote. Lakini pia wamekuwa wakijenga dhana mbaya bila ushahidi wowote juu ya mahusiano ya Zitto na JK.
Binafsi nimekuwa nikiyasoma maoni yao, awali nikidhani labda kuna taarifa zenye ushahidi na Mantiki katika hizo lawama zinazoelekezwa kwa Zitto. Baada ya muda mrefu, nimekuja kugundua kuwa hakuna lolote, zaidi ya njama, au chuki binafsi au vyote kwa pamoja, zinazofanywa na wabaya wa Zitto, wabaya wa CHADEMA na wabaya wa wapenda maendeleo ya nchi hii.
Situmi post hii kujibu lolote juu ya lawama zinazoelekezwa kwa Zitto, kwani hakuna yenye msingi, na baadhi yake amekuwa akizijibu mwenyewe hapa, au kujibiwa na watu wenye taarifa. Kwa hii post simaanishi kwamba namuunga mkono Zitto katika misimamo yake au la, bali napinga kile kile kinachoonekana kuwa mpango maalumu wa kudhoofisha wanaharakati, na kuidhoofisha CHADEMA, unaofanywa na kundi la wachache, wenye nia mbaya dhidi ya taifa na utaifa.
Nawapongeza sana wale ambao wamekuwa na mawazo tofauti na/au mbadala kwa mawazo na mapendekezo fulani yanayotolewa na Zitto, bila kumnyooshea kidole, au kumdhalilisha. Mzee mwanakijiji, na baadhi ya watu wameonekana wazi kabisa wakipingana na mapendekezo ya Zitto juu ya suala la nishati, na Dowans. Hata hivyo sijawahi kuwaona wakimhusisha na mafisadi au na njama zozote mbaya.
Nawalaani sana, tena nawaonya wale wanaoingia na kuanza kumshambulia Zitto bila kuwa na hoja zenye ushahidi. Tena wapo wanaopinga tu mapendekezo yake, bila kuwa na mapendekezo mbadala.
Mi naomba kwa wanaCHADEMA, na wanaharakati wote, wasilaghaiwe na njama za maadui zetu ambao wanajua kuwa kwa kumchonganisha Zitto na CHADEMA, au kumuondoa CHADEMA, watakuwa wameirudisha sana CHADEMA nyuma. Zitto ni naibu katibu mkuu wa CHADEMA, lakini pia ni mwanasiasa anayeheshimiwa sana Tz, hilo tunalijua. Naombeni tu niwaambie kuwa juhudi zinazofanywa kumchonganisha Zitto na CHADEMA, zinaenda sambamba na juhudi za kuimega Kigoma kutoka CHADEMA. Wote mmejionea na mnaendelea kujionea yanayotendeka. Tunaweza kuyapuuzia kwa sasa, lakini kama tunapenda mabadiliko; Tujihadhari sana na vijinjama vidogo hivi, yapo manjama makubwa ya kupambana nayo huko mbele ya safari. Huu ndio wakati wa kuchukua hatua, la sivyo, tusishangae tutakapokuja kubaini kuwa

"The string that united us is already cut, and Things have Fallen apart"

Lets remain united by accepting to differ, but never allow to separate by differing in what we accept.
 
Zitto hachafuki bila sababu, ana mambo mengi ya chini kwa chini yasiyolenga kuikomboa tanzania ndio maana maliberali tunaona bora CDM imtumulie mbali alalame poa tu.

Mtu huchafuka kwa matendo yake: mfano mwakyembe ni ccm mbona hapa jf cdm hawampondii?

Matendo matters than just to wear CDM combat na kujiita mwanaharakati
 

Ushahidi wa uovu wa Zitto dhidi ya wananchi wa Tanzania ingawa ni wa kimazingiza lakini is overwhelming.Zitto ni ndumi la kuwili.Zitto amenunuliwa na mafisadi, no question about it.Anaye bisha ni kipofu.Kwanza huyu anayemtetea Zitto katumwa na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…