Zitto hiyo si demokrasia

Zitto hiyo si demokrasia

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
3,108
Reaction score
2,553
Heshima kwenu wakuu.

Wakati Zitto kabwe akikwaruzana na viongozi wenzake ndani ya CHADEMA alidai kuwa anapambana na mfumo WA kihafidhina ndani ya chama na kwamba alikuwa anapigania chama kuendeshwa kama taasisi na si kwa maamuzi ya MTU mmoja au watu wachache.

Baada ya kutimuliwa CHADEMA na kujiunga na ACT Zitto alijitanabaisha kwamba watajenga taasisi ya kidemokrasia yenye kutoa haki sawa kwa wanachama wote. Hivi karibuni Halmashauri kuu ya chama hicho ilitoa ratiba ya uchukuaji fomu na uteuzi wa wagombea WA nafasi za udiwani, ubunge na urais kwa tiketi ya chama hicho.

Cha ajabu hata kabla wanachama hawajaanza kuchukua fomu Zitto ameshateua na kuwatangaza watu wake watakaogombea ubunge kwenye baadhi ya majimbo bila kufuuta utaratibu wala kuteuliwa na kikao chochote! Wamefanya hivyo kwenye majimbo ya Bukombe, Kahama, Mbowe, Biharamulo na sasa baadhi ya wanachama wanaotaka kugombea kwenye majimbo hayo wameanza kulalamika.

Kwa demokrasia hii ya Zitto ni halali kweli au ndiyo udikteta unaanza kukijenga kwenye chama hicho?
 
Weka ushahidi wa unachokisema, tunachojua yeye alisema/alitia nia ya kugombea ubunge Kigoma Mjini. Hakuna mahala wala maandishi yanayoonesha kuwa ameteua/ameweka watu wake kugombea nafasi mbalimbali uchaguzi mkuu ujao.
 
Malata Junior

Zitto kaishamalizana na Chadema lakini cha kushangaza Chadema bado wanaofuata mpaka ACT - Wazalendo.

Toka lini wafuasi wa Chadema wakawa washauri wa ACT - Wazalendo.

Mkuu ungeaanza kwanza na Mbowe amekuwa kama mfalme anajiongezea muda tu na kuchakachua kipengere cha katiba ya chama hamna ukomo wa uongozi sana Mbowe anaendelea kwa Mwenyekiti wa Chadema mpaka achoke mwenyewe.

Badala ya kupambana na hili unapambana na Zitto ambaye hayupo Chadema.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hujui kuwa Zitto ni mwiba kwa CHADEMA ndio maana bado wanamfuata fuata?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mimi si mwanaccm, ni mwanachama muaminifu WA CHADEMA ila napenda wanasiasa watende vile wanavyonena.
Mkuu vipi Mbowe amekuwa supreme leader pamoja na mgombea urais wa kudumu Dr.Slaa hawa wote marufuku kuwapinga ukijaribu tu kuwapiga utajuta utafukuzwa kama paka.
 
Weka ushahidi wa unachokisema, tunachojua yeye alisema/alitia nia ya kugombea ubunge Kigoma Mjini. Hakuna mahala wala maandishi yanayoonesha kuwa ameteua/ameweka watu wake kugombea nafasi mbalimbali uchaguzi mkuu ujao.
Huyu Bavicha kaokota maneno kwenye vijiwe vya mbege na kuleta JF anajua kabisa wapo pro-Chadema watakubaliana naye bila kuhoji hali muradi katajwa Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu vipi Mbowe amekuwa supreme leader pamoja na mgombea urais wa kudumu Dr.Slaa hawa wote marufuku kuwapinga ukijaribu tu kuwapiga utajuta utafukuzwa kama paka.

kwa hio kama Mbowe na Dr Slaa wamefanya hivo na zito pia afanye hivyo?

Akili za kipimbi hizi
 
Malata Junior

Masikini umekuwa mateka wa Mbowe mpaka umempa na jimbo...Ahahaha.

Eti Zitto kapitisha wagombea kwenye jimbo la Kahama na jimbo la Mbowe.

Bavicha bana.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Bavicha kaokota maneno kwenye vijiwe vya mbege na kuleta JF anajua kabisa wapo pro-Chadema watakubaliana naye bila kuhoji hali muradi katajwa Zitto.

Tatizo hawashirikishi ubongo wao mara mbili mbili,alafu subiri wavamie hapa uone matusi yao ili hali kasemwa Zitto.Huwa nawashangaa sana.Wengine ni watu wenye heshima zao na smart lakini ukiangalia anachodandia inabidi kujiuliza mara mbili mbili.
 
kwa hio kama Mbowe na Dr Slaa wamefanya hivo na zito pia afanye hivyo?

Akili za kipimbi hizi
Unashikiwa akili na wewe unakubali wapi Zitto kafanya hivyo?

Mleta mada kasema yeye ni Chadema tunamwambia aanze na viongozi wake kwanza.

Na wewe ulivyokuwa punguani unaambiwa kuna jimbo linaitwa Mbowe unameza tu.

Acha kutetea ujinga hata kama haupatani na Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Zitto kaishamalizana na Chadema lakini cha kushangaza Chadema bado wanaofuata mpaka ACT - Wazalendo.
huu ni mchango wa Mwanachama Mwandamizi JF.Shaaaame hata kama umejipambanua kuwa mnafiki ila uwe serious sometimes.CCM na Chadema ambao kutwa mitandaoni wanafanya ubishani hawajamalizana??!!!!Zito ambaye moja kati ya singo zake majukwaani ni kujitapa kuiangusha serikali ya CCM,hawajamalizana??!!wa wapi huyu
 
Last edited by a moderator:
Pole zitto
 
Attachments

  • IMG-20150616-WA0005.jpg
    IMG-20150616-WA0005.jpg
    64.1 KB · Views: 359
Unashikiwa akili na wewe unakubali wapi Zitto kafanya hivyo?

Mleta mada kasema yeye ni Chadema tunamwambia aanze na viongozi wake kwanza.

Na wewe ulivyokuwa punguani anaambiwa kuna jimbo linaitwa Mbowe unameza tu.

Duhhhh...Punguani tena...haya Ahsante
 
Zitto kijana Wa ccm anayefagiliwa na watu Wa ccm yuko kazini kufurahisha WANa ccm well done Zitto
 
Back
Top Bottom