Zitto, Bashe Nao Kuwindwa Na Wang'oa Kucha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Bashe Nao Kuwindwa Na Wang'oa Kucha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babalao 2, Mar 17, 2013.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2013
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,386
  Likes Received: 1,464
  Trophy Points: 280
  MAKALA MAALUMU:

  Uchunguzi wakina wa MTANZANIA Jumapili umeonyesha kuwapo kwa kundi la watu wasiofahamika ambalo limekuwa likifuatilia nyendo za Watanzania wanne kwa ukaribu na hata kuiba baadhi ya vifaa vyao vya kazi katika mazingira ya kutatanisha,vinavyoaminika kuwa na nyarakaau kumbukumbu muhimu.

  Kwa mujibu wauchunguzi huo, watu ambao wamekuwa wakifuatiliwa nyendo zao ni Zitto Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari Ltd (2006) na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana, Hussein Bashe, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd,Absalom Kibanda, na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi,Dennis Msaki na viongozi kadhaa wa dini.

  Uchunguzi umeonyesha kuwa Zitto,mwanasiasa kijana ambaye misimamo yake ya kisiasa inadaiwa kuwakwaza baadhi ya wanasiasa
  wenzake ndani ya Chadema na hata nje ya chama hicho, amekuwa akiishi maisha ya wasiwasi na wakati mwingine ameshindwa kushiriki kikamilifu shughuli mbalimbali za chama chake na zisizo za chama kutokana na hofu ya kuuawa.

  Ingawa hakuna rekodi yoyote ya shambulio la kumdhuru lililokwishaelekezwa dhidi yake,taarifa zilizokusanywa na Mtanzania Jumapili zimeonyesha kuwa Zitto, mara kadhaa amekuwa akizuiwa na watu wake wa karibu kuhudhuria baadhi ya shughuli za kisiasa na hasa zinazohusu siasa za majukwaani, kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazoonyesha mipango ya kumdhuru.

  Vyanzo vya habari vya kuaminika vilivyo karibu na Zitto vilivyofikiwa na gazeti hili wakati wa uchunguzi,vimeeleza kuwa Zitto amekuwa katika hatari ya kudhuriwa na watu wasiojulikana tangu alipoonyesha mwelekeo wa kuwania urais 2015.Jambo hilo limeibua joto la kisiasa ndani na nje ya chama chake,hususani kwa wale ambao wana nia ya kuwania wadhifa huo, baada ya Rais Jakaya Kikwete kung'atuka.

  Zitto mwenyewe amepata kukaririwa zaidi ya mara moja akieleza kuwa anao maadui ndani na nje ya Chadema na kauli ambayo amekuwa akiisisitiza ni ile ya kuwepo kwa kundi maalumu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambalo halifurahishwi na mwenendo wake wa kisiasa,lililoamua kumshughulikia.

  Na hata ndani ya Chadema, Zitto amekuwa na uhusiano wenye shaka na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Willbrod
  Slaa, wanaodaiwa kutofurahishwa na staili ya maisha yake ya kisiasa na hasa ushabiki wake wa siasa za kileo zinazosimamia misingi ya kweli ya kidemokrasia.

  Wa pili katika orodha hii ni Kibanda, ambaye hivi karibuni alivamiwa na kundi la watu wasiofahamika, wakamshambulia na kumjeruhi vibaya na hivyo kulazimu kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

  Kibanda, mwandishi wa habari kitaaluma, ambaye amejijengea jina kubwa kutokana na uwezo wake wa kiuandishi, anatajwa kuwa mmoja wa waandishi ambao kalamu zao zimekuwa na athari mbaya kwa baadhi ya wanasiasa anaotofautiana nao kimsimamo na
  kimtizamo.

  Watu walio karibu na Kibanda wanaeleza kuwa ingawa ni mmoja wa waandishi wa habari wachache mwenye uhusiano wa kirafiki na
  watu wengi, hilo halikumuondoa kwenye hatari ya kuwindwa, baada ya kuweka wazi msimamo wake wa kumuunga mkono mmoja wa
  wanasiasa wa CCM anayetajwa kuwa ana nia ya kuwania urais mwaka 2015.

  Wadadisi wa wafuatiliaji wa mambo ya siasa wa hapa nyumbani wanaeleza kuwa Kibanda amekuwa akiangaliwa kwa jicho baya na
  baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa mwanasiasa huyo ambao wanaamini kuwa ushawishi mkubwa alionao ndani ya wanahabari na nafasi yake ya Uenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ni silaha ya kuwaangamiza 2015.

  Kibanda amekuwa akiwindwa na watu wasiojulikana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa akiwa
  bado anaishi eneo la Ubungo Kibangu, aliibiwa simu yake ya mkononi na kompyuta dogo ‘laptop.'

  Mapema mwaka huu, watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwake majira ya usiku wakiwa na nia ya kuiba baadhi ya nyaraka
  zilizokuwa ndani ya gari lake, lakini kabla hawajatekeleza lengo lao,gari hilo lilianza kupiga king'ora,jambo lililosababisha watu hao
  wakimbie.

  Aidha, Kibanda akiwa Hospitalini nchini Afrika Kusini chini ya uangalizi maalumu, watu wasiofahamika wamekuwa wakijitahidi kumfikia katika chumba alicholazwa pasipo mafanikio.

  Habari kutoka Hospitali ya Mill Park alikolazwa zimeeleza kuwa siku chache baada ya Kibanda kulazwa katika wodi ya wagonjwa
  mahututi ambako madaktari walielekeza abaki katika uangalizi wao pekee, watu watatu walifika hospitalini hapo na kujitambulisha
  kuwa wanatoka ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na kutaka kumuona.

  Mmoja wa watu waliosafiri na Kibanda nchini Afrika Kusini kwenda kusaidia kumuuguza ameeleza kuwa alitaarifiwa na uongozi wa hospitali hiyo kuwa kuna maofisa wa ubalozi waliokuwa wakitaka kumuona ili kumjulia hali, lakini wamezuiliwa hadi atakapofika na kuwatambua, lakini katika hali ya kushangaza,watu hao walipotea eneo hilo baada ya kuambiwa kuwa yeye alikuwa njiani kwenda
  kuwatambua.

  Alisema, baada ya tukio hilo,alipokea simu nyingine kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni ndugu wa Kibanda, aliyetokea Tanzania kwa lengo la kwenda kumjulia hali, huku akitaka amuelekeze wodi aliyolazwa, lakini alipomtaka amsubiri ili waonane kwanza, alikata simu na hata alipompigia tena, simu yake ikawa haipatikani.

  Ni kutokana na mwenendo huo wenye kutia mashaka, Kibanda alilazimika kuwekewa ulinzi maalumu katika wodi aliyolazwa. Mwanasiasa kijana, Hussein Bashe,ambaye ni kada wa CCM, naye yumo katika orodha ya watu wanaowindwa kwa sasa na kundi la
  watu wasiojulikana, huku taarifa nyingine zikionyesha kuwa miongoni mwa watu wanaofuatilia nyendo zake kwa karibu ni polisi. Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa Bashe naye ni mmoja wa wanasiasa ambao misimamo yao ya kisiasa imekuwa ikiwatesa baadhi ya
  vigogo wa kisiasa hapa nchini na zipo pia taarifa kuwa hatua yake ya kutangaza kumuunga mkono mmoja wa wanasiasa waliotajwa
  kutaka kuwania urais kupitia CCM imezidi kumjengea maadui,hususan mahasimu wa kisiasa wa kambi anayoiunga mkono.

  Kwa mujibu wa Bashe, mapema mwaka huu akiwa anatoka ofisini kwake, gari la polisi lililokuwa na askari wenye silaha lililokuwa
  limeegesha nje ya ofisi yake lilianza kumuandama na kumsimamisha akiwa eneo la Sinza Makaburini,ambapo askari hao walidai kuwa
  wana wasiwasi naye na baada ya kumhoji walimuacha.

  Bashe, akizungumza na waandishi wa habari wiki iliyopita, katika mkutano wa wadau wa habari, alisema tukio hilo lilitokea akiwa ameandamana na Kibanda. Alisema kabla ya tukio hilo, gari lake liliwahi kugongwa kwa nyuma na gari aina ya pick up ambalo lilikimbia baada ya tukio hilo na mwishoni mwa wiki iliyopita watu wanaodhaniwa kuwa polisi walifika katika ofisi za New Habari majira ya usiku na kujaribu kuingia ndani ya uzio wa ofisi hizo kwa uficho,kabla ya kutambuliwa na walinzi ambao walifukuzwa pamoja na mbwa.

  Rekodi zilizopo zinaonyesha kuwa Bashe anao maadui ndani ya CCM anaohasimiana nao kwa muda mrefu na chanzo cha uhasama huo
  kinaelezwa kuwa ni vita ya makundi ya ndani ya chama ambayo yanapambana kushika hatamu za uongozi wa dola mwaka
  2015.

  Mwingine katika orodha ni mwandishi wa habari, Msaki ambaye naye taarifa za uchunguzi wa MTANZANIA Jumapili zimeonyesha kuwa amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na kundi hilo la watu wasiofahamika. Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa Msaki, ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, amekuwa akitajwa kuwa karibu na kundi la akina Lowassa, lakini pia akiwa na urafiki wa karibu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi na Zitto.

  Msaki pia anatajwa kulengwa na kundi la wahalifu linalohasimiana na Zitto kutokana na ukaribu wake na mwanasiasa huyo, ambapo
  inaaminika ni mmoja wa makamanda wanaoratibu mikakati ya vita yake ya kisiasa dhidi ya maadui zake.

  Uchunguzi wa Mtanzania Jumapili umeonyesha Msaki aliwahi kuvamiwa na watu wasiojulikana wakati akiwa hayupo, ambao waliondoka na kasiki ya kutunzia pesa iliyokuwa na nyaraka zake mbalimbali za kazi.

  Vyanzo vya habari kutoka Mwananchi Communication Ltd vimeeleza kuwa Msaki aliwahi kuibiwa kompyuta yake ndogo iliyokuwa ofisini kwake na watu wasiojulikana na kwamba katika siku za karibuni amekuwa akiandamwa na watu wasiofahamika, jambo ambalo
  limemfanya aishi maisha ya wasiwasi.

  Mbali na Msaki, miongoni mwa viongozi wa dini wanaowindwa ni pamoja na Askofu Valentino Mokiwa, ambaye misimamo yake inahusishwa na siasa zinazoegemea kundi fulani la watu wanaowania madaraka 2015.

  Tayari Askofu huyo alivamiwa nyumbani kwake wiki iliyopita na watu wasiojulikana ambao baada ya kumkosa walimjeruhi vibaya mlinzi wake.
   
 2. m

  my web JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 1,603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  basi watz wote tunawindwa tunyofolewe kucha,meno .tupelekwe mabwepande.coz leo kila gazeti na watu wake .tanzania daima mzee mengi na lowasa .hapa naona zzk na bashe.waandishi vihiyo.tunawaandishi makanjanja tu by jk
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2013
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,405
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  hii ni makala ya kikanjanja ambayo hata mwandishi hajitambui na hajielewi. Sijajua mwandishi kasomea nini, na kama anajitambua.
  Inawezekanaje mwandishi unaleta mada mchanyato?unaichanganya jamii badala ya kuielimisha au kufikisha ujumbe! Kwa makala hii,kila mtu ni adui wa mwingine. Madainaonesha uhasama ndani ya chadema, uhasama katika tasnia ya habari, uhasama wa uraisi, uhasama ndani ya ccm, uhasama ndani ya balozi za nchi, ndani ya usalama wa taifa, uhasama wa taasisi ya kipolisi, uhasama baina ya jamii nzima ya watanzania...kila mtu ni adui. Nakushauri ujipange upya ,uje na mada inayoeleza kila taasisi kwa utulivu wala si kuhangaika angaika ivo.

  Siku njema mwandishi.
   
 4. meeku

  meeku JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2013
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 571
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  hapo kwenye red, yaliyobaki yote ni poojo. Hata mtoto mdogo analijua hilo.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Mar 17, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,049
  Likes Received: 1,881
  Trophy Points: 280
  Polisi wanawinda watu; watu wanawinda polisi; wanasiasa wanawindwa na polisi; polisi wanawinda wanasiasa; watu wanawindana; wanasiasa wanawindana; waandishi wa habari wanawindwa; waandishi wa habari wanawindana; Zitto anawindwa, Msacky anawindwa, Kibanda anawindwa, Mwigamba anawindwa, kila mwandishi anawindwa. Makundi ya Urais ndani ya vyama vya siasa yanasababisha watanzania wawindane. Njama zinapangwa kuwawekea watu dwa za kulevya na kuwateka, watu wanamwagiwa tindikali na hata huenda wanapigwa nondo vichwani. JF tunawindana! Nchi imejaa wawindaji na wawindwaji sasa ni timing kama ya kumuua kobe ukichez uanamwagiwa tindikali, unapata ajali, unang'olewa meno, unang'olewa kucha hata kung'olewa macho.


  Eee mola tunusuru tuipite salama 2015 manake naona mateso yanainyemelea nchi.
   
 6. m

  my web JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 1,603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh.kimbunga you hav made my day.kila mtu anawindwa.watz tumebaki kulana na kutafunana
   
 7. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2013
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,386
  Likes Received: 1,464
  Trophy Points: 280
  Kuna hatari ya kuzuka kikundi kitakachoingia msituni ili kung'oa tawala dhalimu cjui ni msitu upi ila tusiombe JWTZ wakawinda JKT na FFU wakawawinda Mgambo tutakufa sana.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 15,784
  Likes Received: 2,374
  Trophy Points: 280
  So simple ni
  HUNTERS BEING HUNTED.

  CHADEMA noma inaonekana wako fiti kuliko serekali na TISS yake.

  Kweli AKILI NDOGO kuongoza AKILI KUBWA.
   
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 15,784
  Likes Received: 2,374
  Trophy Points: 280
  Pata picha hapa ndio kwanza hata uteuzi wa majina bado.
  Naamini kipindi cha uteuzi watu wata KOLIBWA au wata MALIMWA.

  Pata picha sasa Kampeni zikianza ni wangapi watafanywa mbaya?

  Pata picha sasa huyu mgombea ndio kasha shinda na yupo madarakani sijuhi hali itakuwaje ni mwendo wa kuua na kufungia tu magazeti, redio na TV na usishangae hata mabalozi kufukuzwa nchini.

  Naona wale maadui 11 hawata subiri 2015, itabidi wakimbie mapema.
   
 10. m

  my web JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 1,603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbowe ana 0 ya form six.slaa diplo ya upadri ndio
   
 11. m

  my web JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 1,603
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kama ningekuwa mimi mwanaharisi ningepiga china wahariri wote wangekwenda jera maramoja hata tanzania daima lisingekuwapo mtaani
   
 12. Alinda

  Alinda Platinum Member

  #12
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 1,543
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Mbona hueleweki) Mwanaharisi ni nini? Jera ni kitu gani? ningepiga china???
   
 13. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2013
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Ha ha ha ha Mkuu Kimbunga unajua tafsiri ya yote hayo ni nini?

  1.Hatuko salama-Tuliowapa jukumu la kutulinda (Serikali) hawako serious.Mfano rahisi bwana kimunga,wewe uvamiwe lada na majambazi eneo la tabata nyumbani kwako usiku,ukawashtukia majambazi kabla hawajaingia ukwapiga simu polisi,kwanza aidha wasiipokee simu au wakipokea hawatakuja au waje kesho yake.Wana msaada gani sasa.

  2.Hakuna wa kumwamini-Sio wanasiasa ,sio wanausalama na sio serikali na sio waandishi wa ajabu.

  3.Aidha waandishi wa habari wanatumika vibaya kuilisha jamii sumu.Inawezekana kati ya haya kuna matukio ya kawaidia kabisa mfano kuibiwa laptop but Likakuzwa.Waandishi wa habari wana uwezo mkubwa wa kuiharibu jamii yetu.

  Ila kiukweli;HATUKO SALAMA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. mhindijohn

  mhindijohn JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2013
  Joined: Nov 25, 2012
  Messages: 470
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hiki ni kizunguzungu kikali! FBI iko wapi? Nikama vile TISS wameshindwa kazi! Zimwi likujualo......
  Sisi raia wakawaida tusiojua hata kurusha ngumi! Mungu atuimarishie self defence ya kukimbia over vogue, maana hawa maharamia wakikuweka kati ni HATARI!
   
 15. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2013
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Ha ha ha ha Mkuu Kimbunga unajua tafsiri ya yote hayo ni nini?

  1.Hatuko salama-Tuliowapa jukumu la kutulinda (Serikali) hawako serious.Mfano rahisi bwana kimunga,wewe uvamiwe lada na majambazi eneo la tabata nyumbani kwako usiku,ukawashtukia majambazi kabla hawajaingia ukwapiga simu polisi,kwanza aidha wasiipokee simu au wakipokea hawatakuja au waje kesho yake.Wana msaada gani sasa.

  2.Hakuna wa kumwamini-Sio wanasiasa ,sio wanausalama na sio serikali na sio waandishi wa ajabu.

  3.Aidha waandishi wa habari wanatumika vibaya kuilisha jamii sumu.Inawezekana kati ya haya kuna matukio ya kawaidia kabisa mfano kuibiwa laptop but Likakuzwa.Waandishi wa habari wana uwezo mkubwa wa kuiharibu jamii yetu.

  Ila kiukweli;HATUKO SALAMA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Makala ya kijinga kabisa, naona kazi ndio imeanza sasa!Usikute haya wanayafanya kwa kujua kabisa!
   
 17. k

  kurya JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2013
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 510
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumia ubongo kufikiri na sio kutunzia kamasi.
   
 18. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2013
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,135
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ulimboka aliporudi alipotafakari alimjua Adui yake ikabidi apotezee.
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,373
  Likes Received: 13,991
  Trophy Points: 280
  Sasa hapa umeandika nini?


   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,373
  Likes Received: 13,991
  Trophy Points: 280
  Waandishi kwa kuandika ujinga awajambo!
   
Loading...