mi huwa nashangaa sana watu wazima wenye akili kama zitto kisha wanaongea pumba za kitoto kama hawana uwezo wa kutathmini kitu, hapa kama hamjabadili mfumo wa vyama vingi na kuweka tume huru ambayo mwenyekiti wake hachaguliwi na mwenyekiti wa ccm basi hata kuwe na mikawa mitatu iloungana hamtakuwa na uwezo wa kuwaondoa watawala madarakani.
tatizo sio wingi wa watu wala wingi wa kura,tatizo ni mfumo wa game ulivyo hata mkipata kura zote hampati ushindi,hii nchi bado inaendeshwa kwa maagizo.
kama kuna jambo kubwa la kulipigania saivi ni katiba na mfumo huu wa vyama vingi ulio batili ufikie mwisho.
Wewe embu kaa chini ujifikirie hili.....
Usaliti wa vyama na wanavyama wao unatoka wapi??
Mathalani
Mtu kama ZZT ni mtu hatari sana tena sana na anabadilika kulingana na upepo na sio siri huwezi mlinganisha na kiongozi yeyote wa vyama vya upinzani.
Na sukufichi huyu jamaa ni pasua kichwa ndio maana huwezi mlinganisha na hata wakina Tundu lisu
Kwanza huwa yuko smart kwa kila anachofanya, hata kama anabolonga anajua namna yu kuliweka kosa lake likawa na maana, likabaki ni sahihi kwa wengi wasiomuelewa na hata kwa wanaomuelewa litabaki ni kosa la kiufundi
Mfano. Leo anakuja na hoja ya kuungana, na atautumia ulimi kutoa hoja ndani ya kichwa chake wengi tutamuunga mkono, lakini tukumbuke kuna mtu/watu wake ndani ya serikali hii hii tunayoipinga, hapa atasemaje?? Ukimpa nafasi ya kukutafutia haya majibu utamjua kuwa huyu ni mtu wa namna gani??
Huyu jamaa hua ni FUNDI
Maana yake anapotaka kubomoa anabomoa kiufundi na anapotaka kujenga anajenga kiufundi
Hapa utanielewa vizuuuri ukimkumbuka ZZK yule alieukataa ukawa kwa hoja za msingi kabisaaaa na ambaye anauunga mkono umoja wa upinzani kwa hojaa nzuri kabisaaaaa...
Tusisahau pia ilani ya ACT anayo raisi iki iweje na kama ni mpinzani kweli?? Anawawakilishi ndani ya serikali yeye ataanzaje kuuunda huu umoja??
TUTEGEMEE MICHEZO MINGI KUTOKA KWA HUYU JAMAA NGULI WA SIASA TZ.
Mpaka kuna wakati nawaza usmart alionao zitto angeupata TUNDU ANTIPAS LISSU upinzani ungepiga hatua
" sasa anaestahili hakupewa, asiestahili kapewa""
Hapo ndipo itaujua ukuu wa Mungu.