Zitto atamani wapinzani waungane kuing’oa CCM madarakani

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
ZItto.jpg

Mwanza.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameeleza umuhimu wa vyama vya upinzani kuungana akisema ndio mkakati pekee utakaoing’oa CCM madarakani.

Zitto alisema hayo wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini na ndani ya ACT -Wazalendo.

ACT-Wazalendo haikuwa ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, ikiviachia vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi za urais, ubunge na udiwani.

Lakini katika mahojiano na Mwananchi, Zitto alionekana kutambua umuhimu wa umoja katika kupambana na chama hicho kikongwe nchini ambacho kimeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50, kikianzia na jina la Tanu kwa Bara na ASP kwa visiwani.

“Kwa mazingira ya siasa yaliyopo nchini, ushirikiano miongoni mwa vyama vya upinzani kukabiliana na CCM ni jambo lisilokwepeka,” alisema Zitto, mwanasiasa wa kizazi kipya ambaye hajawahi kuwa CCM kama ilivyo kwa wanasiasa wengi wa upinzani.

“ACT Wazalendo tunalitambua hilo ndio maana tunafanya juhudi kubwa kujenga chama chenye nguvu kitakacholeta chachu ya ushindi kwa kushirikiana na vyama vingine.

“Hakuna chama cha siasa chenye nguvu kinachokubali kuungana na kingine kilicho dhaifu. Ndio maana tunajenga chama kuongeza nguvu na ushawishi kisiasa ili tukiungana kusiwepo chama kinachonyonya nguvu ya kingine.”

Kauli ya Zitto ni tofauti na msimamo ambao amekuwa akiuonyesha tangu aondolewe Chadema mapema mwaka 2015 na alitumia kampeni za chama hicho kuponda Ukawa. “Kama unataka siasa za mbwembwe nenda CCM, kama unataka siasa za ulaghai nenda Ukawa, na kama unataka siasa za msingi siasa za issues ni ACT Wazalendo,” alisema Zitto Agosti 28, 2015 wakati harakati za uchaguzi zikiwa zimepamba moto.

hivyo, katika matukio ya hivi karibuni, Zitto amekuwa akishirikiana na viongozi wa vyama vingine, hasa Chadema ambayo ilikuwa na mgogoro naye kwa muda mrefu.

Zitto na Chadema walionyesha dalili za kuanza kuondoa tofauti zao wakati wakipinga uamuzi wa Serikali kufuta matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge.

Oktoba mwaka huo, Zitto aliisifu Ukawa kwa jinsi ilivyopambana na CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini akasema ACT-Wazalendo haitajiunga na umoja huo kutokana na miiko iliyojiwekea katika Azimio la Tabora.

Katika uchaguzi huo, Ukawa ilimsimamisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye aliweka rekodi ya upinzani kwa kupata kura milioni 6.07 ambazo ni takriban mara mbili ya kura zote ambazo wapinzani wamekuwa wakipata tangu kurejeshwa kwa siasa za ushindani mwaka 1992.

Akijibu swali la kituo kimoja cha televisheni kama atagombea urais mwaka 2020, Zitto pia alidokeza umuhimu wa ushirikiano.

“Kwa mazingira yaliyopo sasa, suala la kugombea au kutogombea urais lisiwe maamuzi ya mtu mmoja. Kwa sasa tunahitaji kwenda kwenye uchaguzi wa 2020 vyama vya upinzani tukiwa united front.Tukiwa tunashirikiana, si kuungana kwa sababu vyama vina itikadi tofauti,” alisema Zitto akijibu swali hilo mapema mwaka huu.

Katika kipindi hicho cha kuanzia mwaka 2015, viongozi wa vyama vingine, hasa Chadema walikuwa wakimrushia maneno Zitto na chama chake, wakisema hawatakubali ajiunge Ukawa.

Kuhusu mpango huo wa kuifanya ACT Wazalendo kuwa kubwa, alisema wameandaa mikakati kadhaa ya kukabiliana na changamoto, hasa za kifedha.

“Tumejiwekea mkakati wa kuhimiza kila mwanachama kuchangia Sh1,000 kila wiki, au Sh4, 000 kwa mwezi kugharamia uenezi na ujenzi wa chama; tumegawa kadi zaidi ya 400,000 na iwapo wanachama 100,000 pekee watachanga, tunatarajia kukusanya Sh400 milioni kwa mwezi,” alisema Zitto.

Alisema fedha hizo zitasaidia mikakati ya kujenga chama kuwa cha kimkakati.

Kuhusu kukamatwa mara kwa mara kwa wanasiasa wa upinzani, Zitto alisema:“Naumizwa sana kuona viongozi, hasa wa upinzani wakikamatwa kwa kutekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba ya kuisimamia, kuikosoa na kuishauri Serikali; kibaya zaidi amri za kukamata viongozi wakiwemo wabunge zinatolewa hadi na wakuu wa wilaya.”

Zitto aifikiria ‘Ukawa’ kuing’oa CCM madarakani
 
Mwanza. Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameeleza umuhimu wa vyama vya upinzani kuungana akisema ndio mkakati pekee utakaoing’oa CCM madarakani.

Zitto alisema hayo wiki iliyopita katika mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini na ndani ya ACT -Wazalendo.

ACT-Wazalendo haikuwa ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, ikiviachia vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi za urais, ubunge na udiwani.

Lakini katika mahojiano na Mwananchi, Zitto alionekana kutambua umuhimu wa umoja katika kupambana na chama hicho kikongwe nchini ambacho kimeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50, kikianzia na jina la Tanu kwa Bara na ASP kwa visiwani.

“Kwa mazingira ya siasa yaliyopo nchini, ushirikiano miongoni mwa vyama vya upinzani kukabiliana na CCM ni jambo lisilokwepeka,” alisema Zitto, mwanasiasa wa kizazi kipya ambaye hajawahi kuwa CCM kama ilivyo kwa wanasiasa wengi wa upinzani.

“ACT Wazalendo tunalitambua hilo ndio maana tunafanya juhudi kubwa kujenga chama chenye nguvu kitakacholeta chachu ya ushindi kwa kushirikiana na vyama vingine.

“Hakuna chama cha siasa chenye nguvu kinachokubali kuungana na kingine kilicho dhaifu. Ndio maana tunajenga chama kuongeza nguvu na ushawishi kisiasa ili tukiungana kusiwepo chama kinachonyonya nguvu ya kingine.”

Kauli ya Zitto ni tofauti na msimamo ambao amekuwa akiuonyesha tangu aondolewe Chadema mapema mwaka 2015 na alitumia kampeni za chama hicho kuponda Ukawa,

“Kama unataka siasa za mbwembwe nenda CCM, kama unataka siasa za ulaghai nenda Ukawa, na kama unataka siasa za msingi siasa za issues ni ACT Wazalendo,” alisema Zitto Agosti 28, 2015 wakati harakati za uchaguzi zikiwa zimepamba moto.

Hata hivyo, katika matukio ya hivi karibuni, Zitto amekuwa akishirikiana na viongozi wa vyama vingine, hasa Chadema ambayo ilikuwa na mgogoro naye kwa muda mrefu.

Zitto na Chadema walionyesha dalili za kuanza kuondoa tofauti zao wakati wakipinga uamuzi wa Serikali kufuta matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge.

Oktoba mwaka huo, Zitto aliisifu Ukawa kwa jinsi ilivyopambana na CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini akasema ACT-Wazalendo haitajiunga na umoja huo kutokana na miiko iliyojiwekea katika Azimio la Tabora.

Katika uchaguzi huo, Ukawa ilimsimamisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye aliweka rekodi ya upinzani kwa kupata kura milioni 6.07 ambazo ni takriban mara mbili ya kura zote ambazo wapinzani wamekuwa wakipata tangu kurejeshwa kwa siasa za ushindani mwaka 1992.

Akijibu swali la kituo kimoja cha televisheni kama atagombea urais mwaka 2020, Zitto pia alidokeza umuhimu wa ushirikiano.

“Kwa mazingira yaliyopo sasa, suala la kugombea au kutogombea urais lisiwe maamuzi ya mtu mmoja. Kwa sasa tunahitaji kwenda kwenye uchaguzi wa 2020 vyama vya upinzani tukiwa united front.Tukiwa tunashirikiana, si kuungana kwa sababu vyama vina itikadi tofauti,” alisema Zitto akijibu swali hilo mapema mwaka huu.

Katika kipindi hicho cha kuanzia mwaka 2015, viongozi wa vyama vingine, hasa Chadema walikuwa wakimrushia maneno Zitto na chama chake, wakisema hawatakubali ajiunge Ukawa.

Kuhusu mpango huo wa kuifanya ACT Wazalendo kuwa kubwa, alisema wameandaa mikakati kadhaa ya kukabiliana na changamoto, hasa za kifedha.

“Tumejiwekea mkakati wa kuhimiza kila mwanachama kuchangia Sh1,000 kila wiki, au Sh4, 000 kwa mwezi kugharamia uenezi na ujenzi wa chama; tumegawa kadi zaidi ya 400,000 na iwapo wanachama 100,000 pekee watachanga, tunatarajia kukusanya Sh400 milioni kwa mwezi,” alisema Zitto.

Alisema fedha hizo zitasaidia mikakati ya kujenga chama kuwa cha kimkakati.

Kuhusu kukamatwa mara kwa mara kwa wanasiasa wa upinzani, Zitto alisema:“Naumizwa sana kuona viongozi, hasa wa upinzani wakikamatwa kwa kutekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba ya kuisimamia, kuikosoa na kuishauri Serikali; kibaya zaidi amri za kukamata viongozi wakiwemo wabunge zinatolewa hadi na wakuu wa wilaya.”

Chanzo: Mwananchi
 
mi huwa nashangaa sana watu wazima wenye akili kama zitto kisha wanaongea pumba za kitoto kama hawana uwezo wa kutathmini kitu, hapa kama hamjabadili mfumo wa vyama vingi na kuweka tume huru ambayo mwenyekiti wake hachaguliwi na mwenyekiti wa ccm basi hata kuwe na mikawa mitatu iloungana hamtakuwa na uwezo wa kuwaondoa watawala madarakani.
tatizo sio wingi wa watu wala wingi wa kura,tatizo ni mfumo wa game ulivyo hata mkipata kura zote hampati ushindi,hii nchi bado inaendeshwa kwa maagizo.

kama kuna jambo kubwa la kulipigania saivi ni katiba na mfumo huu wa vyama vingi ulio batili ufikie mwisho.
 
Baada ya Lipumba kuonyesha rangi zake halisi, hawezi tena kurudi Ukawa.. Anatafutwa wa kum-replace kwenye kutengeneza Ukawa mwingine ili apate nafasi nyingine ya kuuvunja kwa mara ya pili.. Zitto Mungu anakuona..
 
Hilo ndio wazo ambalo vyama upinzani vinatakiwa kufanyia kazi. Bila kuungana pamoja na kuwa na mikakati ya pamoja ni kazi kuiondoa CCM
 
Ni ndoto ya mchana viongozi wa vyama vya siasa upinzani kuungana. Waungane kwa jambo lipi, wakati:
1) Viongozi hao hao kila mmoja wao anatafuta umaarufu binafsi wala si wa chama cha siasa anachokiwakilisha!
2) Kuna migogoro ya ushindani na misuguano ndani ya vyama vyenyewe, ambayo inakua kila kukicha!
3) Viongozi wana misimamo na mitazamo tofauti kuhusu utendaji kazi wa Rais Magufuli
4) Mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yanayoletwa na Rais Magufuli yanawagusa kichanya wananchi wote, kiasi viongozi wa upinzani wamebaki kurukia masuala yasiyo na tija kwa maendeleo ya nchi.

WAKATI NDO HUU UPINZANI KUUNGANA NA SERIKALI KWA MAENDELEO YA NCHI
 
Huyu jamaa huwa haeleweki yuko upande gani, ni mtu wa kumuepuka, japo ni kijana smart sana, lakini huu udhaifu wake unamharibia.

Kweli Mungu hakupi kila kitu.
 
Yeye mwenyewe Zitto alishindwa kuungana na UKAWA 2015 ili kuiondoa CCM hizi hadithi anamwambia nani?
 
Anatafuta njia ya kujipenyeza ili aweze kujua kinachojiri ndani ya UKAWA. Huyo mtu ni wa kuangalia kwa makini sana kwani hajulikani ni wa rangi gani
 
Huyu jamaa haishi unafiki, mwenyewe clip yake kule Kigoma akiwa na Magu atuwekee!!

Likely itakuwa baada ya issue ya Bombardier kuona kuwa imemuharibia na uwaziri wa nishati hatomegewa tena,kaamua kurudi location ili aaminike na maboss zake waandae fungu kubwa 2O2O!!!​
 
Mkuu niulize tu!! Hivi kuna UKAWA Tanzania?

Au ndo mwendelezo wa siasa za ghiriba?
Anatafuta njia ya kujipenyeza ili aweze kujua kinachojiri ndani ya UKAWA. Huyo mtu ni wa kuangalia kwa makini sana kwani hajulikani ni wa rangi gani
 
mi huwa nashangaa sana watu wazima wenye akili kama zitto kisha wanaongea pumba za kitoto kama hawana uwezo wa kutathmini kitu, hapa kama hamjabadili mfumo wa vyama vingi na kuweka tume huru ambayo mwenyekiti wake hachaguliwi na mwenyekiti wa ccm basi hata kuwe na mikawa mitatu iloungana hamtakuwa na uwezo wa kuwaondoa watawala madarakani.
tatizo sio wingi wa watu wala wingi wa kura,tatizo ni mfumo wa game ulivyo hata mkipata kura zote hampati ushindi,hii nchi bado inaendeshwa kwa maagizo.

kama kuna jambo kubwa la kulipigania saivi ni katiba na mfumo huu wa vyama vingi ulio batili ufikie mwisho.
nakubaliana na wewe kwa asilimia zoote
 
yeah tatizo kubwa hapa ni hii NEC yetu ambayo ipo jina tu ila utendaji wake unaratibiwa na mpangaji mkuu wa pale magogoni,uchaguzi uliopita mliona ni jinsi gani alivyofanya mabadiliko ya NEC bila ya kumshirikisha yeyote;hii tume lazima iwe huru na iwajibike kwenye Bunge na bajeti yake itengwe na Bunge,hii tume LAZIMA iwe na watumishi wake kwenye ngazi zote yaani kuanzia taifani hadi kwenye mtaa,hii tume lazima iendeshe mambo yake kitaalam,our Home Affairs ministry lazima itoe life books kwa watanzania wote,ikianzia na mara mtoto anapozaliwa lazima apewe id number yake(jina lake)na through hii id number ataishi nayo na kufa nayo.vinginevyo kuitoa au kuichallenge ccm ni ndoto za alinacha.
 
inatakuwa kuna misheni anaenda kuitekeleza..........
 
Back
Top Bottom