Zitto ataja mawaziri mizigo

Zitto ataja mawaziri mizigo

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ametaja mawaziri watano wanaotaka kukwamisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Zitto alisema mawaziri hao hawataki mabadiliko ndiyo maana wamekuwa wakikwamisha juhudi za Rais Jakaya Kikwete za uundwaji wa katiba mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Aliwataja mawaziri hao aliowaita ni wahafidhina, wasiopenda mabadiliko ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, William Lukuvi, Stephen Wassira, Mathias Chikawe na George Mkuchika.

Zitto alisema kama Rais Kikwete anataka kufanikiwa kwenye mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ni vema akawafukuza kazi mawaziri hao kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo jana mkoani Tabora alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara na kufungua matawi ya CHADEMA wilayani Nzega.

Alisema viongozi hao kwa wakati tofauti wamekuwa wakimshauri Rais Kikwete vibaya, hususan katika suala la katiba, hali ambayo imewaweka njia panda wananchi.

Zitto alisema mawaziri hao hivi karibuni wakati wabunge wa vyama vya upinzani walipotoka bungeni kupinga baadhi ya vipengele katika mchakato wa muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, walitoa kauli tofauti zenye madhara kwa jamii.

Alisema Pinda alishindwa kutumia nafasi yake kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuepusha mtafaruku.
Aliongeza kuwa wakati Lukuvi na Wassira walipotoa lugha ya maudhi kwa viongozi wa upinzani juu mustakabali wa Tanzania katika mchakato wa katiba mpya, rais aliwapuuza na kuamua kukutana na wenyeviti wa vyama vitatu vya upinzani.

"Kama mnakumbuka Lukuvi alilidanganya Bunge kuwa Wazanzibari walishirikishwa katika mchakato mzima, Wassira aliamua kutembea kifua mbele na kusema hakuna nafasi ya wapinzani kwenda Ikulu kujadiliana na rais.
"Chikawe aliamua kumtisha rais kwa kumweleza kuwa ataingia katika mgongano na Bunge.

Hivi ni vitisho, na kwa bahati mbaya kwao, Kikwete amewashitukia sasa sijui kwanini hawatimui kazi." alisema.


Alisema uamuzi wa Rais Kikwete kukubali kukutana na viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi huku akikubali kuwa kuna mambo yanayoweza kujadiliwa kwa utaratibu mzuri, ni uthibitisho kuwa washauri hao wa rais hawapaswi kuendelea kushikilia nafasi walizonazo.

Zitto alisema viongozi hao bado wanaamini suala la katiba ni mambo ya CCM, na kwamba Watanzania hawana nafasi ya kujadili au kuamua kupitia kwa wawakilishi wao.

Kuhusu waziri mkuu, Zitto alisema ameshindwa kuwaunganisha wabunge na shughuli za Bunge, hali aliyoeleza kuwa inaifanya serikali isemewe na wabunge.

Alisema wakati kesho ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 14 tangu kufariki dunia kwa Mwalimu Nyerere, serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeamua kwa makusudi kuwasahau wakulima.
 
message sent to all concervative followers.
Cc ze marcopolo,le mutuz,mwana diwani,chama,chris lukosi,pasco etc.
 
Hongera ZZK na huo ndo ukweli halisi japo hao mawaziri wanawashirika wao, kuna mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wa mambo ya ndani, naibu spika,na wengine wengi
 
Tungekuwa na CHADEMA TV au Radio tungepata hizi hotuba bila chenga!
 
Hasa hasa huyu Wasira.analeta mambo ya mwaka 47.
 
Tuungane pamoja kuwanyoa kwa vigae vya chupa 2015, wametufanya sisi wehu wa barabarani, time will tell
 
message sent to all concervative followers.
Cc ze marcopolo,le mutuz,mwana diwani,chama,chris lukosi,pasco etc.

You are giving them the credit they don't deserve,You should call them CCM sycophants or CCM minions instead coz they deserve it.
 
Huyu mkimbizi naye mnafiki tu mi sioni anachozungumza ni comedy tu sasa hana cha maana hata kimoja.
 
zitto ni zaidi ya kiongozi heshima kwako.
 
Kanyaga twende kamanda Zitto kanda ya magharibi imeshaiva hiyo kazi iliyobaki ni kuwaunganisha wananchi kwa ajili ya mabadiliko makubwa ya kiuongozi na kiutawala.
 
Last edited by a moderator:
hawa mawaziri ni vilaza na mizigo kwa taifa, ila JK nae amezidi kudanganywa hashtuki tu? kitendo cha kumdanganya au kumshauri vibaya rais ni serious offense inayotakiwa mtu awe stripped off madaraka yake!!
 
Back
Top Bottom