Solomon David
JF-Expert Member
- Mar 1, 2009
- 1,146
- 17
Kaka hizi details ulizotoa hapa zinanipa picha kuwa upo ndani unajua mengi kuliko hao unaobishana nao hapa. Tafadhali achana nao watu wanafrustrations zao za maisha ambao ili kujipa moyo kuwa maisha hayajawakalia vibaya basi njia rahisi ni kugeuza wengine wote kuwa ndio wenye matatizo....
Wengine ndio hivyo ni mabingwa wa kulia ukabila wakati wao ni wafaidika, waumini na waendekezaji wakubwa wa ukabila na udini wao. Unapoona mtu anamgeuzia mwezanke kuwa adui eti kwa kuwa aliquestion mantiki ya magazeti yanayomilkiwa na watu wa kabila moja kumshambulia wakati akiwa katika ushindani na mtu wa kabila lao basi ujue ni ukabila huohuo ndio unaoshape chuki zake hizo.
Mwenzao Zitto badala ya kukimbilia umaarufu kwa siasa za kikasuku amechagua kwenda kujielimisha zaidi kuhusu sekta ya madini na kujiongezea maarifa kwa upana zaidi katika upeo wa kimataifa na kufanya utafiti wa kisayansi ili aweze kutoa mchango madhubuti zaidi jinsi ya kuyashughulikia mapungufu yaliyopo katika sekta hiyo hapa kwetu.
Tatizo wengi wanamjua Zitto kwa muono wa buzwagi na mengineyo wanasahau kuwa uwezo wa kuthamini, kutafuta na kujielimisha kuhusu masuala aliyochagua kuyasimamia hata kabla ya buzwagi ndio imekuwa na inaendela kuwa nguvu yake kubwa kama kiongozi mahiri.
Hawa wao wanasubiri WAHANDISI WETU WA HABARI kutoka katika vyomboi vya havbari vilivyogubikwa na maslahi binafsi za wamiliki wake ndio wawapashe, wa-shape na kuongoza mitizamo yao katika mnasuala muhimu ya nchi.
Asante sana Solomon for this peace of advise, lets talk about them..
Omar,
Mpaka pale Zitto atakavyofikia viwango vya elimu vya baadhi ya members hapa ambao wanampinga Zitto, nadhani ndipo utakuwa na audacity ya kutoa misifa kibao kwa elimu ya Zitto (ambayo bado anaitafuta na hakuna guarantee yoyote kuwa ataipata).
Msijione kuwa mnajua mambo mengi kuliko watanzania. Kuna watu kibao tu hapa wana elimu na uelewa zaidi ya Zitto. Tafadhali vijana, kama ndivyo mnataka uongozi wa nchi hii kwa maneno ya dharau na kashfa kama haya, basi mjue kuwa mna kazi kubwa sana mbele yenu.
Waberoya,
We always talk about them. Check it for yourself. There are more than a thousand and one threads here talking about every one else but Zitto.
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kesho atatoa majibu ya kauli zilizotolewa na naibu wake Zitto Kabwe, ambaye alisema kuwa ataendelea kumtetea rafiki yake, David Kafulila kwenye kampeni za ubunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.
Awali Dk Slaa alisema hawezi kuzungumzia kauli hiyo ya Zitto iliyosababisha mwenyekiti wa zamani, Bob Makani kutamka kuwa baraza la wazee litajadili na kutoa uamuzi mzito dhidi ya mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.
Lakini jana mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo alisema kuwa kauli hizo za Zitto zitatolewa ufafanuzi na Dk Slaa kesho kwenye kongamano la Vyuo Vikuu lililoandaliwa na Chadema na kufanyika jijini Dar es Salaam.
"Leo hii kama ulivyoona tumezungumza suala la kongamano letu, masuala ya Zitto siku hiyo yatatolewa ufafanuzi na Dk Slaa pamoja na (mwenyekiti wa Chadema, Freeman) Mbowe kwa kuwa watakuwepo. Ni wazi kuwa wataulizwa swali nini maamuzi ya chama kwa Zitto, kwa hiyo kila kitu kitajulikana siku hiyo," alisema Tumbo.
"Leo haikuwa siku maalumu ya kuzungumza kuhusu kauli ya Zitto, lakini kama unataka ufafanuzi wa suala hili njoo kwenye kongamano kwa kuwa suala hilo litafafanuliwa na, kama sio, Mbowe basi Dk Slaa."
Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu wa kongamano hilo ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mwakajila Emmanuel alisema watafanya mijadala yao kwenye ukumbi wa DDC Mlimani jijini Dar es Salaam.
Alisema kongamano hilo litajadili mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwelekeo wa hali ya siasa nchini na vita dhidi ya ufisadi.
"Pia kongamano litajadili mwelekeo wa sera za Chadema kuelekea uchaguzi mkuu 2010, masuala ya huduma za jamii, ulinzi na uendelezaji wa rasilimali za nchi na mfumo wa utawala na ujenzi wa demokrasia," alisema Emmanuel.
Emmanuel, ambaye ni mwenyekiti wa vijana wa Chadema (Bavicha) mkoani Mbeya alisisitiza kuwa kongamano hilo litakalowashirikisha wanafunzi 1,000, kutoka vyuo mbalimbali nchini, limeandaliwa na Chadema na kuwashirikisha watu mbalimbali.
"Ukweli ni kwamba kongamano hili linaitwa kongamano la Chadema kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini," alifafanua Emmanuel.
Alisema kuwa katika kongamano hilo ambalo mgeni rasmi ni Mbowe, mada ya hali ya siasa nchini na vita dhidi ya ufisadi itawasilishwa na Dk Slaa; mada kuhusu mwelekeo wa sera za chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2010 itawasilishwa na Susan Lyimo (Mb); mfumo wa utawala na ujenzi wa demokrasia utawasilishwa na msomi, Prof Mwesiga Baregu.
Alisema malengo ya kongamano hilo ni kuwafanya wanafunzi kutafakari hali ya siasa nchini, kuhimiza jamii vyuoni kushiriki katika chaguzi mbalimbali, kuelimisha jamii kutorubuniwa na wanasiasa pamoja na kukitaka chama hicho kueleza wazi ni kwanini kiungwe mkono na wananchi, kina hoja na sera gani zitakazowasaidia Watanzania.
Jumatatu wiki hii, Zitto aliibuka tena na kutonesha majeraha ya mgogoro uliokuwapo ndani ya chama chake, akisema haridhiki na uamuzi wa chama hicho kuwaengua David Kafulila na Danda Juju.
Ingawa Kabwe hakutaja jina, kauli yake kupinga maamuzi ya kuwavua madaraka wanachama hao; imeonyesha kumzungumzia Dk Willibrod Slaa kwa vile ndiye muajiri wa wafanyakazi wa sekretarieti kwa nafasi yake ya katibu mkuu na ndiye mwenye mamlaka ya kuwatimua.
"Mimi sipendi siasa za kinafiki, uamuzi wa kuwavua nyadhifa zao kina Kafulila haukuniridhisha kwa sababu haukuwa mzuri, ingawa ulipitishwa na mamlaka husika, katika vikao husika," alisema Kabwe katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa na kituo cha televisheni cha TBC1 juzi asubuhi.
Akizungumza na gazeti hili juzi kutoka nchini Ujerumani aliko masomoni Zitto alisema hawezi kuzungumza lolote kuhusu kauli ya Makani kuwa atajadiliwa na uamuzi mzito utatolewa dhidi yake.
MWANANCHI 08-01-20010
natumaini busara itatumika katika kujibu masuala
ya zitto hususan kama zitto mwenyewe hatakuwepo.
MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema haoni ubaya wowote kwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kumuunga mkono swahiba wake, David Kafulila katika harakati zake za kugombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini akiwa chama kingine.
Kafulila alikuwa afisa habari wa Chadema huku akifanya mikakati ya kugombea ubunge wa jimbo hilo, lakini akatimuliwa na bosi wake, Dk Willibrod Slaa kwa tuhuma za kuvujisha siri za chama. Hata hivyo, Kafulila ameendeleza nia yake ya kuwania ubunge, lakini akiwa chama kingine cha NCCR Mageuzi.
Zitto hakufurahishwa na uamuzi wa Dk Slaa kumfukuza msaidizi wake pamoja na Danda Juju, ambaye alikuwa akishughulikia masuala ya Bunge, akisema kuwa Kafulila alifanya mambo mengi ya kukitangaza chama mkoani Kigoma na ana nafasi ya kuwa mbunge na hivyo umakini ulitakiwa katika kushughulikia suala lake.
Wakati mjadala huo ukielekea kupoa, taarifa ziliibuliwa kuwa Zitto ameanza kumsaidia Kafulila na kwamba magari yake yalitumika katika moja ya shughuli zake mkoani Kigoma akiwa NCCR Mageuzi.
Baadaye Zitto aliweka bayana kuwa atamsaidia kwa kila hali ili aweze kushinda uchaguzi, kauli ambayo imepingwa na viongozi wenzake wa Chadema.
Lakini Profesa Lipumba aliiambia Mwananchi kuwa haoni ubaya kwa Zitto kumsaidia Kafulila kulichukua jimbo la Kigoma Kusini.
"Mimi sioni ubaya au tatizo lolote kwa Zitto kuendelea kumsaidia Kafulila baada ya kuhamia NCCR madam hajatoka kambi ya upinzani," alisema Profesa Lipumba.
Hali ya siasa katika jimbo la Kigoma Kusini linaloshikiliwa na mbunge wa CCM Manju Msambya inaonyesha kwamba chama hicho kinaongoza kwa kuwa na mtandao mzuri, kikifuatiwa na NCCR na baadae Chadema.
Lipumba alifafanua kuwa kama Kafulila anakubalika Kigoma Kusini na kwa vile ana chama cha kumdhamini kugombea ubunge jimboni hapo, hakuna tatizo kwa Zitto kumuunga mkono na kumsaidia kimawazo hata kwa mali.
"Kwa vile NCCR Mageuzi ina mtandao mzuri Kigoma Kusini, nadhani Kafulila ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri jimboni hapo," alisema Lipumba.
Profesa Lipumba alisema kwa kuwa Kafulila ni kijana aliyekuwa ananyanyukia katika siasa za Tanzania ndani ya Chadema kutokana na ushawishi wake, kitendo cha kuvuliwa nyadhifa kinaonekana kililenga kumkata miguu ili asisonge mbele.
"Hiyo ndiyo sababu iliyofanya baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema kutoridhishwa na uamuzi huo na wakatangaza wazi kuendelea kumuunga mkono,"alisema Profesa Lipumba.
Lipumba hakufurahishwa na tabia ya viongozi wa Chadema kujibizana kwenye vyombo vya habari, akisema kwamba jambo hilo linaweka taswira mbaya kwa chama na baadhi ya wananchi kujenga mashaka na chama hicho.
Kwa maoni yangu kitendo cha Zito kumsapoti rafiki yake Kafulila ni cha kawaida kabisa katika siasa duniani.CNN mwaka 2008 katika kipindi cha MEET THE PRESS walimhoji Genaral Collin Powel(Republican) kuhusu maoni yake kati ya Barrack Obama(Democrat) na John McCain(Republican) na kwa uwazi kabisa alimsapoti Barrack Obama kwa kuzingatia uwezo na hoja za wagombea bila kujali anatoka chama gani.Jamani umefika wakati tusifungwe sana na vyama na kuacha kuwasapoti wenzetu eti kwa sababu hatupo nao chama kimoja.Nawasilisha......MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema haoni ubaya wowote kwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kumuunga mkono swahiba wake, David Kafulila katika harakati zake za kugombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini akiwa chama kingine.
Kafulila alikuwa afisa habari wa Chadema huku akifanya mikakati ya kugombea ubunge wa jimbo hilo, lakini akatimuliwa na bosi wake, Dk Willibrod Slaa kwa tuhuma za kuvujisha siri za chama. Hata hivyo, Kafulila ameendeleza nia yake ya kuwania ubunge, lakini akiwa chama kingine cha NCCR Mageuzi.
Zitto hakufurahishwa na uamuzi wa Dk Slaa kumfukuza msaidizi wake pamoja na Danda Juju, ambaye alikuwa akishughulikia masuala ya Bunge, akisema kuwa Kafulila alifanya mambo mengi ya kukitangaza chama mkoani Kigoma na ana nafasi ya kuwa mbunge na hivyo umakini ulitakiwa katika kushughulikia suala lake.
Wakati mjadala huo ukielekea kupoa, taarifa ziliibuliwa kuwa Zitto ameanza kumsaidia Kafulila na kwamba magari yake yalitumika katika moja ya shughuli zake mkoani Kigoma akiwa NCCR Mageuzi.
Baadaye Zitto aliweka bayana kuwa atamsaidia kwa kila hali ili aweze kushinda uchaguzi, kauli ambayo imepingwa na viongozi wenzake wa Chadema.
Lakini Profesa Lipumba aliiambia Mwananchi kuwa haoni ubaya kwa Zitto kumsaidia Kafulila kulichukua jimbo la Kigoma Kusini.
"Mimi sioni ubaya au tatizo lolote kwa Zitto kuendelea kumsaidia Kafulila baada ya kuhamia NCCR madam hajatoka kambi ya upinzani," alisema Profesa Lipumba.
Hali ya siasa katika jimbo la Kigoma Kusini linaloshikiliwa na mbunge wa CCM Manju Msambya inaonyesha kwamba chama hicho kinaongoza kwa kuwa na mtandao mzuri, kikifuatiwa na NCCR na baadae Chadema.
Lipumba alifafanua kuwa kama Kafulila anakubalika Kigoma Kusini na kwa vile ana chama cha kumdhamini kugombea ubunge jimboni hapo, hakuna tatizo kwa Zitto kumuunga mkono na kumsaidia kimawazo hata kwa mali.
"Kwa vile NCCR Mageuzi ina mtandao mzuri Kigoma Kusini, nadhani Kafulila ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri jimboni hapo," alisema Lipumba.
Profesa Lipumba alisema kwa kuwa Kafulila ni kijana aliyekuwa ananyanyukia katika siasa za Tanzania ndani ya Chadema kutokana na ushawishi wake, kitendo cha kuvuliwa nyadhifa kinaonekana kililenga kumkata miguu ili asisonge mbele.
"Hiyo ndiyo sababu iliyofanya baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema kutoridhishwa na uamuzi huo na wakatangaza wazi kuendelea kumuunga mkono,"alisema Profesa Lipumba.
Lipumba hakufurahishwa na tabia ya viongozi wa Chadema kujibizana kwenye vyombo vya habari, akisema kwamba jambo hilo linaweka taswira mbaya kwa chama na baadhi ya wananchi kujenga mashaka na chama hicho.
Kwa maoni yangu kitendo cha Zito kumsapoti rafiki yake Kafulila ni cha kawaida kabisa katika siasa duniani.CNN mwaka 2008 katika kipindi cha MEET THE PRESS walimhoji Genaral Collin Powel(Republican) kuhusu maoni yake kati ya Barrack Obama(Democrat) na John McCain(Republican) na kwa uwazi kabisa alimsapoti Barrack Obama kwa kuzingatia uwezo na hoja za wagombea bila kujali anatoka chama gani.Jamani umefika wakati tusifungwe sana na vyama na kuacha kuwasapoti wenzetu eti kwa sababu hatupo nao chama kimoja.Nawasilisha......

sawa sawa kabisa:ukiwa unatoa mifanao jaribu kuweka like for like
wakati collin powell anayasema hayo hakuwepo kwenye frontline politics za republican.
angekuwa kwenye frontline politics za republican angesema hayo, angetakiwa kujiuzulu.
Zito yuko kwenye frontline politics za chadema.
Ni chadema kama chama ndio kinatakiwa kiseme kitamuunga mkuno kafulila.
kama chadema wakisimamisha mgombea wao na wakamtuma zitto akamfanyie kampeni, zitto akikataa what next???