Tony Gwanco
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 5,913
- 1,217
ganda la muwa la jana,chungu kaona kivuno
kaa akiinua gando mambo yameharibika
ganda la muwa la jana,chungu kaona kivuno
Hata hivyo alishatamka mwenyewe kuwa akimaliza kipindi chake cha ubunge atatafuta chuo anachoweza kuajiriwa na kuanza kufundisha.Zito ni mnafiki sana na anawaadaa tu,hivi haujui kuwa mwakani bunge linavunjwa kuelekea uchaguzi mkuu?.ana kiinua mgongo kama milion 100 hivi,hawezi kitu anachofanya ni uhuni tu,yaani anaendesha chama kingine huku ni mwanachama wa chadema pia,nadhani chadema wanamvumilia sana,tena sana,ana violence na huo ni uhuni ambao sidhani chadema wataendelea kuvumilia.
Hivi uliisha wahi kujiuliza kwanini hakwenda kupeleka mashataka jimboni kwake badala yake alikwenda Kasuru? Umeisha wahi pia kujiuliza, kwanini kina Mwigamba wameenda tena Kasuru kumnadi zzk na sio jimboni kwake kule Kigoma vijijini? For your inform, mimi nimeolewa huko kwao, ninavyojua hata akibaki CDM, jimboni kwake hawezi kupata KURA za kwezesha kushinda uchaguzi, amenusa na pua yake imempa jibu sahihi!
Zitto tuko na wewe, hawakujui kuwa wewe ni mtu wa grassroot.
Ngoja watauona moto.
CHADEMA ni lazima mjiandae kisaikolojia, huyu kijana ni tishio kwa msatakabali wa chama chenu ambacho mwanzoni mlijivua nguvu ya vijana, nguvu ambayo hapana shaka sasa inayumba yumba ikisubiri kuona ZITTO KABWE anaweka wapi mizizi.
Mwanzo na mwisho wa Zito ni Kigoma - maana mtu ni kwao. CCM iliyomrubuni itamwacha peke yake baada wa kufanikisha lengo lao. Mifano ni mingi, yetu macho
Nakubaliana na utetezi wako wote kuhusu Zitto ila hapo huweki record sawa. Wana kigoma sidhani kama wanamkubali Zitto kihivyo maana kwenye urais alimnadi Jk, kwahiyo watu hawamsikilizi yeye bali chama na hata kura alizopata zimezidi kupungua. Kama nyinyi ni washauri wake muambieni ukweli record yake kigoma haimpi kijidai. Ila Zitto ni mwanasiasa mzuri akifanyia kazi mapungufu yake.Nipe takwimu 2005 chadema ilikua na madiwani wangapi na wabunge wangapi mkoa wa kigoma. Na sasa 2010 wapo wangapi?
Hilo swali la pili ni kuwa wale wabunge wa nccr wahesabu kama wa chadema ila mliwakataa na kuwafukuza kwa kuwaita sisimizi wale wote walitokana na ushawishi wa ZITO kwa wanakigoma na kampeini aliwapigia.
Usitumie jeuri na kiburi cha dk.Slaa kwa kumu-hukumia Zito.
Kwa hilo wala hana hatia. Na slaa kura za urais kigoma walimpa nyingi sana kuliko arusha na kilimanjaro.
Tumia jicho la tatu kuangalia.
Hawana majibu wameishia kukaririshwa.
Nakubaliana na utetezi wako wote kuhusu Zitto ila hapo huweki record sawa. Wana kigoma sidhani kama wanamkubali Zitto kihivyo maana kwenye urais alimnadi Jk, kwahiyo watu hawamsikilizi yeye bali chama na hata kura alizopata zimezidi kupungua. Kama nyinyi ni washauri wake muambieni ukweli record yake kigoma haimpi kijidai. Ila Zitto ni mwanasiasa mzuri akifanyia kazi mapungufu yake.
Ungekua umeolewa Kigoma usingeshindwa kujua kama hakuna wilaya inayoitwa Kasuru. Sisi ndo wenye Kigoma yetu usitake kujipendekaza. For your information, hata kama angekwenda Rais Obama wa Marekani hawezi kumshinda Zitto katika jimbo la Kigoma Kaskazini. Siasa za Kigoma huzijui hivyo huna haki ya kuandika utumbo wako.
Zitto hana haja ya kushitaki kwa wapiga kura wake. Wao wanajua kila kitu Mbunge wao alichotendewa na hao wendawazimu Chadema. Ngoja nikwambie kitu, Zitto ni nembo ya Kigoma. Kama kweli umefika Kigoma ungekua unajua hilo. Kila pembeni mwa barabara limeandikwa jina lake. Zitto mbali na kuwa Mbunge keshasimikwa kama Mwami Ruyagwa wa Kasulu.
Utamjua Zitto vizuri akishatangaza kuondoka Chadema. Huo utakua mwisho wa Chadema Kigoma. Nakuhakikishia mwaka ujao si Chadema wala NCCR ambao watakua na chao Kigoma. Politics in Kigoma is built around Mwami Ruyagwa ZZK.
Ndio maana huwa mnaitwa misukule. Umeaminishwa na hao Chagadema kuwa Zitto anatumika. Mungu hakikupa kichwa kwa ajili ya kufugia nywele. Tumia kichwa kufikiria ili uchanganye na za kwako.
Chagadema watawadanganya watu kama wewe tu lakini sisi wenye akili timamu watakwama.
Zitto ndio Mbunge pekee ambaye hawezi nunulika ndio maana hata posho ya vikao vya bunge hachukui. Mr. Zero naye alijaribu kuacha gari la Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni lakini akazunguka tena kimya kimya kulichukua. Kuiga siyo kuzuri it need to come from the heart.
Usipende kusikia mambo ya kuambiwa. Hakuna hata sehemu moja huko Kigoma ambapo Zitto alimpigia Kikwete Kampeni. Babu Slaa kura alizopata zilitokana na ushawishi wa Zitto.
Hili linaweza kuthibitishwa na ziara aliyoifanya hivi karibuni baada ya kuwa na mgogoro na Zitto. Kuna sehemu kabisa alishindwa kuhutubia kwa kukosa watu. Kasulu walienda mbali zaidi kwa kumshusha jukwaani na kumpa kipigo kama mbwa mwizi. Ashukuru askari polisi kwa kumuokoa. Kwa sasa angeshabadilika jina na kuitwa marehemu.
Mwaka ujao siyo mbali. Kama huyo babu Slaa akipitishwa na Chagadema atawajua watu wa Kigoma. Labda asiende kabisa huko.
Zitto aliwekeza nguvu zakutosha ktk kuijenga cdm mkoan kgm lakin jitihada zake ziliharibiwa na Mbowe na Slaa kwakuwafukuza akina Kafulila ambao ndio walikuwa tegemezi la chama ktk majimbo yao
Wana JF,
Katika ukrasa wake wa facebook zito kaandika haya,
Sijui anataka kumaliziaje!
Hapo kwenye unyerere sijamuelewa anamaanisha Nyerere Msanii au marehemu Julius Nyerere? Unyerere wa vitendo ni pamoja na kuachia ngazi zote alizo nazo ikiwa ni pamoja na uenyekiti wa PAC, ambapo atapoteza na kile cheo alichopata juzi juzi kwenye kamati ya PAC za Africa, aachie Ubunge arudi Kigoma kukuza wakala wa CCM.
ZITTO hata akigombea kwa MBOWE anashinda.
Atachukuaje posho huku madollar ya Ujeremani yanaingia kutoka lumumba? Hiyo ni tabia ya wanafiki na wasaliti.Huyo mamluki hana jipya na ndio maana hata mashabiki wake ni wale vijana wachumia tumbo kama wewe na wale mabuku 7. Huu ndio mwanzo wa mwisho wake!