Alichokifanya ndio kazi aliyoitaka na akapewa. Zitto hawezi kuomba msamaha huyu maana CCM itamshangaa na kumtapika. Hata suala la kutaja wenye fedha Switzerland ni moja ya mikakati yake ya kisiasa ya kutupa mashambulizi ya kupumbaza watu mapema kujihami au kutimiza lengo lake au la waliomtuma (political phony pre-emptive strikes). Kwa vile baadhi ya watu ni wavivu kusumbua vichwa vyao kutafakari kwa undani hayo mashambulizi anayoyafanya kama vile hoja binafsi basi tukafikiri kuwa Zitto ni Mtatezi wa wanyonge.
Hakuna hoja yoyote ya Zitto iliwahi kuzaa matunda mwishoni (kwa ajili ya wanyonge), kwani makusudi yake huwa si kuzaa matunda bali kunyanyua umaarufu wake na kuwalinda wale ambao wamemtuma. Mtakumbuka habari ya wenye fedha (jambo ambalo halikuwa jipya nchini Tanzania kusikika hata kusomeka) but was another phony pre-emptive strike ambapo aliishia kusema hakukuwa na haja ya kuwataja wahusika maana hana imani na Serikali kama itafanya chochote, mara akajisahahu tena akasema atashirikiana na Mwanasheria Mkuu kusaidia kutoa taarifa kwa kumtumia Confidant wake wa huko Switzerland na tena akasema atakwenda mwenyewe huko kuibua wahusika. Kwa kufanya hivi akateka mjadala wa wezi wetu na hivyo hakuna anayeshughulika na hilo, watu wanakaa wanaota eti tunamsubiria Zitto (mtu ambaye hana chombo chochote cha dola wala hata saini inayotambulika ndani wala nje ya nchi yetu kama kiongozi wa Serikali) eti ndiye apewe na mabenki ya Switzerlands majina ya Watanzania wateja wao wenye fedha huko, kiasi cha fedha na zaidi ya yote eti aweze kutueleza pasi na shaka njia walizozitumia kuzipata hizo fedha eti kazi ambayo yeye anaiweza lakini Serikali yetu haiwezi! Kusudi lake lilisha timia maana alipata umaarufu toka kwa wanaCCM na Wapinzani wengi at the same time in the house on that material day lakini siku zote tupo wachache tusiokubali kudanganywa!
Hata Leka dutigite haikuwa kwa ajili ya kuwanyanyua akina Kiba, Mwasiti, Banana, Chege, Diamond, Ommy wala wenzao bali kwa ajili yake ndio maana akasema eti aliguswa sana na Wabunge (aliokuwa amewateka pasipo kujua) walipochochewa kutamka hadharani kuwa hakutakuwa na mgombea Urais kama yeye. Siku iliyofuate,Zitto akaanza kuwadhalilisha wenzake kwa kusema analiamini gazeti lililoandika habari hizo kuliko Wabunge wenyewe akina Halima Mdee!
Je tayari mmeshasahu michango yake ya utetezi wa majenereta ya mafisadi yanayoifilisi TANESCO hadi leo na sisi wateja kubebeshwa gharama kubwa? Hebu nikumbusheni, matokeo ya ile Tume iliyoundwa na Rais na yeye akazawadiwa ujumbe; je mwishoni ilizaa matunda gani kwa wanyonge?
Sitashangaa kikao cha Bunge lijalo akazuka na hoja nyingine ya kuzuga watu. Anaweza kuzuka na hoja binafsi Bungeni ya kum-impeach Rais (kwa vile watu wanasema ni rafiki yake) na wasiohangaisha vichwa watashangilia na kusema "huyu ndiye Zitto asiye na uoga", lakini watu wenye akili watasema, subiri mwisho wa hiyo hoja binafsi tuone matunda yake mwishoni! Zitto ni kama Lowassa hasafishiki hata kwa the strongest bleaching agent. Watu wa namna hii, hata kama wangeweza kufanikiwa kuwanunua baadhi yetu; wakanunua na baadhi ya watu kwenye media ikiwemo na mitandao ya kijamii; wakaweza kutoa michango mikubwa sana makanisani, misikitini na kwa vijana-Masalia wenye njaa kwa mtaji wa umaskini wetu na ujinga wetu; Wallahi, wataibuka watu WASIODANGANYIKA NA WATAKATAA USALITI WAO NA WATAWAADHIBU VIKALI SANA SIKU ZA USONI!!