Albert Einstein
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 394
- 583
Wasalaam
Na Galila Wabanh'u
Nimesoma makala ya Mhe Zitto Zubeir Kabwe mbunge wa Kigoma mjini akipotosha juu ya mradi wa bandari ya Bagamoyo kama moja ya mradi unaopaswa kutekelezwa katika eneo hilo pamoja na ujenzi wa reli yetu ya kisasa ya SGR.
Kwa wasiofahamu Ndugu Zitto anajulikana kwa kufanya “biashara” ya siasa. Yeye hulipwa ili kuwasemea “wanufaika” wa wanaotaka au wanaotekeleza miradi mbalimbali ya Serikali kwa ubia au wao wenyewe.
Tabia yake hii ameifanya kwenye kutoa taarifa za uongo kwa mataifa ya nje yenye nia isiyo ya wazi juu ya Taifa letu. Pia Ndugu Zitto akishirikiana na wenzake wa aina yake waliungana na kampuni iliyokuwa inayasimamia makampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Bulyanhulu, North Mara na Pangea (Buzwagi). Watu hawa walijaribu kumtisha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa uthubutu wake wa kuamua kuchunguza mikataba ya madini utalipelekea Taifa letu kushtakiwa na kuishia kulipa pesa nyingi, kufukuza wawekezaji na kugombana na mataifa makubwa na taasisi za kimataifa.
Waliyasema hayo hayo Mhe Rais Magufuli alipoagiza mapitio na uboreshaji wa mikataba ya kampuni ya mawasiliano ya Airtel, TICTS iliyopo bandarini, nk. Hata hivyo, mafanikio yaliyopatikana kwa uamuzi huu na hatimaye mapitio ya mikataba yote yamewaacha na aibu kubwa Zitto na kundi lake wanaomtumia.
Zitto huyu huyu na wenzake bila aibu wamekuwa pia wakitumika na makampuni ya kuchapisha noti duniani kuzunguka na kutoa rushwa ili wapate tenda mbalimbali kwenye benki kuu katika mataifa ya Afrika Mashariki.
Aidha, ni bahati mbaya kuwa Zitto na wenzake wanaendelea kutumika na wanyonyaji wa raslimali za nchi bila kung’amua kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli katika uchunguzi wa mikataba mbalimbali imegundua uchafu na madhaifu mengi ya kimikataba ambayo ndiyo iliyoifanya Serikali ya Awamu ya Tano “kushtuka” kuhusu rasimu ya mkataba wa Uendelezaji wa Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone - SEZ) pale Bagamoyo inayojumuisha ujenzi wa Bandari. Mradi huu uliokuwa utekelezwe na kampuni ya China Merchant Port ya jijini Shenzhen nchini China wakishirikiana na Mfuko wa Wakfu wa Oman.
Vipengele vilivyopendekezwa kwenye rasimu ya mkataba vingi ni vya kinyonyaji. Serikali imewaambia wawekezaji hawa kuwa vipengele vyenye ukakasi viondolewe ili mkataba uwe utakaowanufaisha pande zote mbili kwa maana ya mwekezaji na Taifa kama dhamira bado wanayo ya kutaka kushiriki kwenye mradi huo mkubwa wa Serikali vinginevyo haiwezekani.
Ni wenye nia ovu tu ndio wanaweza kubeza na kuona kuwa uamuzi huu wa serikali wa kusimamia raslimali za Taifa kwa maslahi ya wananchi wetu ni uamuzi mbaya usiofaa.
Ndugu Zitto amejaribu kueleza uamuzi wa baadhi ya nchi jirani kutekeleza baadhi ya miradi aliyoianisha ila ni muhimu kumkumbusha na kuwakumbusha watanzania kuwa tunaweza pia kujifunza kuwa sio maamuzi yote yanayofanywa na nchi jirani zetu au hata nchi nyinginezo ni uamuzi sahihi.
Mfano, Wakati nchi jirani ilipoamua kujenga reli ya kisasa ya kiwango cha SGR walijikuta wameingia mkataba mbovu ambao gharama za ujenzi ni kubwa sana karibu mara mbili za ujenzi ukilinganisha na SGR ya Tanzania, SGR yao ni ya kutumia mafuta aina ya Diesel, SGR yao treni inakimbia spidi ya kilomita 120 kwa saaukilinganisha na SGR ya Tanzania ambayo treni yake itatembea spidi ya kilomita 160 kwa saa nk.
Hivyo ni vizuri ndugu Zitto akaanzishe rasmi kampuni ya kibiashara itakayomuwezesha kufanya udalali wa kibiashara aachane na siasa au utumishi wa wananchi.
Siamini kama wananchi wa Kigoma anaowawakilisha wamemtuma kuhujumu Taifa badala ya kuungana na Serikali ya Awamu ya Tano kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wake wakiwemo wana-Kigoma La sivyo, wananchi wanaweza kukiona Chama cha ACT-Wazalendo kama mrija tu unaotumika kupitisha madili ya kiongozi wake bila wanachama wake kujua kuwa wanatumika kwa maslahi ya watu wachache.
#MimiNiMshindi