Zitto amzidi kete Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto amzidi kete Spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JOHN MADIBA, Jun 30, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, alimwongezea Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, muda wa kuwasilisha utetezi wake dhidi ya Baraza la Mawaziri, lakini mbunge huyo aliwasilisha utetezi wake jana alasiri.

  Asubuhi ya jana Makinda alisema amemwongezea muda hadi Jumatatu ijayo, ili athibitishe tuhuma zake kwamba Baraza la Mawaziri lilishawishiwa kubadili msimamo na kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge.

  Kwa mujibu wa Makinda, wakati akitoa taarifa jana bungeni, Zitto alikuwa amemwomba Spika amsaidie kupata nyaraka kutoka Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha na Uchumi ambazo zinahusu mjadala wa CHC zitakazomsaidia katika utetezi wake.

  Uamuzi huo ulitolewa jana bungeni na Spika Makinda, wakati akitoa taarifa hiyo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

  “Waheshimiwa wabunge, kwa mujibu wa sheria, nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri; na hili liliwahi kuelezwa na Spika wa Bunge aliyepita Julai 2008 alipokuwa akizungumzia suala la TICS. Hivyo, ofisi yangu haiwezi kumsaidia Zitto kupata nyaraka hizo, ila namwongezea muda hadi Jumatatu Julai 4 mwaka huu, awe amewasilisha utetezi wake,” alisema Spika Makinda.

  Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili jana alasiri na kuthibitishwa na Zitto mwenyewe zinaeleza kuwa mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni aliwasilisha utetezi wake, ukiwa na viambatanisho vyote muhimu.

  Ingawa Zitto hakuwa tayari kueleza kwa undani aina ya vielelezo alivyowasilisha katika utetezi wake, habari ambazo gazeti hili lilizipata zinaeleza kwamba katika moja ya viambatanisho vyake, mbunge huyo amewasilisha vivuli vya waraka wa Baraza la Mawaziri.

  Zitto aliibua hoja hiyo wiki iliyopita wakati akichangia Azimio hilo la CHC, lililowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, hivyo kuwalazimu mawaziri watatu; William Lukuvi (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge), Waziri Mustafa Mkulo na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, kusimama kila wakati kujibu hoja zake.

  Akichangia hoja hiyo, Zitto alisema azimio hilo limegeuzwa tofauti na ilivyokuwa na kusisitiza kuwa hali hiyo imetokana na ushawishi (lobbyist) ambao baraza la mawaziri lilipewa, hivyo aliwataka wabunge kutoyakubali maamuzi hayo akisema yataigharimu nchi.

  “Nawaombeni sana waheshimiwa wabunge fumbeni macho muangalie suala hili kwa kutokubali maamuzi haya ya Baraza la Mawaziri, maamuzi haya yanatokana na lobbyist, naamini Baraza la Mawaziri halikuwa well advised (halikushauriwa vema),” alisema Zitto na kumfanya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimama na kuomba mwongozo wa Spika akimtaka Zitto kuthibitisha kauli yake.

  Katika mwongozo huo, Mkuchika alisema Zitto amewadhalilisha kwa kulituhumu Baraza la Mawaziri kurubuniwa na watu kupindisha maamuzi hayo ya Bunge, hivyo kumtaka aombe radhi lakini pamoja na hatua hiyo Zitto alisema ana uhakika na anachokisema.

  Hatua hiyo ilimfanya pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, kukazia kauli ya Waziri Mkuchika na kumtaka Zitto kuthibitisha kauli yake lakini pamoja na kauli hiyo ya Lukuvi Zitto alisimama na kusema kuwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri yanatokana na matokeo ya ushawishi kwa baraza hilo na kuitaka serikali kupeleka pendekezo la awali la CHC lililotolewa na Waziri wa Fedha na kuongeza kwamba, “Na tusiruhusu baraza la mawaziri kuendeshwa na malobbyist.”

  Baada ya Zitto kueleza hayo, Lukuvi naye alisimama na kusema anafahamu kuwa Zitto ana uchungu na anakerwa na hali hiyo na kumsisitiza kuthibitisha kauli yake lakini baadaye Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), alisimama na kusema, “Kwa kuwa Zitto amekwisha kutoa taarifa hiyo na kujibiwa na serikali, mwisho wake humrudia mwenyewe (Zitto) ili alihitimishe.”

  Katika mapendekezo yake Zitto alisema ndani ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na hata katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, walikubaliana kwamba CHC wapewe muda wa kutosha kukamilisha kazi na majukumu yao halafu baada ya hapo ndipo Waziri Mkulo apeleke bungeni Azimio hilo na si kuwapa kipindi cha mpito cha miaka mitatu kama alivyowasilisha azimio hilo jana.

  Alisema kuwa chombo hicho kinaangalia mali za umma na mashirika, hivyo kutaka kukiua na kupeleka majukumu haya kwa Msajili wa Hazina ambaye uwezo wake wa kulinda mali za umma ni mdogo sana, ni kutaka kuiba mali za Watanzania.

  Alisema azimio la serikali la kuipa CHC kukamilisha majukumu yake limelenga katika kuwasaidia wafanyabiashara walioiba mali za umma ikiwa ni pamoja na kukopa mabilioni ya fedha kutoka iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ambao kesi zao zipo mahakamani, kupata ahueni kwa vile hatua hiyo itapoteza ushahidi.

  Pamoja na Zitto, hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola (CCM), Mbunge wa Kalenga, Dk. William Mgimwa (CCM) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), waliokomelea msumari wa mwisho katika kupinga hoja hiyo.

  Kutokana na hatua hiyo, Spika Anne Makinda, alihitimisha mgongano huo na kumpa siku saba Zitto (hadi Juni 29) kuthibitisha kauli yake hiyo.

  Hatua hiyo ilimfanya Waziri Mkulo kulazimika kurekebisha azimio hilo na kusema kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha sheria ya benki, Bunge linaazimia kuongeza muda wa uhai wa Shirika la CHC kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Julai mosi hadi Juni 30, 2014 ili kutoa fursa kwa shirika hilo hodhi la mali za mashirika kukamilisha taratibu za kiutendaji na kisheria na baada ya hapo serikali itafanya tathmini ya shirika hilo la CHC na kupeleka taarifa bungeni ili kuona namna litakavyoshughulikiwa.

  Awali akiwasilisha hoja ya msingi, Waziri Mkulo ililiomba Bunge kupitisha Azimio hilo ili CHC iweze kuongezewa kipindi cha mpito cha miaka mitatu imalize majukumu yake na baadaye majukumu yake yahamishiwe Ofisi ya Msajili wa Hazina.
   
 2. m

  mob JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  kama aliweza kufanya harakati chuo na hakufukuzwa je bungeni watamweza
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Safari hii b kiroboto asikae na huo utetez kama wa lema
   
 4. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mimi naomba Zito auweke humu jamvini.
   
 5. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Sasa spika aseme tena anachotaka. sidhani kama mawaziri wote wanakubaliana na kila aina ya uzembe, kwahiyo Zitto kupata hizo nyaraka ilikuwa very simple. na kwa vile ni siri huwezi kumhoji yeye inabidi wao mawaziri waulizane nani kazitoa nje. Tunakutakia kila la kheri Zitto.
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  CONSOLIDATED HOLDING CORPORATION
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


  INTERVIEW WITH THE DIRECTOR GENERAL OF THE CONSOLIDATED HOLDING CORPORATION (CHC), MRS. EDWINA A. LUPEMBE
  Source: The Guardian Newsletter

  1. When was CHC formed and what are its objectives?

  ANSWER:

  The Consolidated Holding Corporation (formerly NBC Holding Corporation) was established on 1[SUP]st[/SUP] October, 1997 by the Parliament through the enactment of the National Bank of Commerce (Re-
  organisation and Vesting of Assets and Liabilities) Act. No. 23 of 1997, as amended (also known as Cap. 404).

  CHC is one of the three successor entities of the former National Bank of Commerce (NBC) whose re-organisation gave rise to the existence of the Consolidated Holding Corporation, NBC Limited and the National Micro- finance Bank.

  You may wish to know that the Corporation's first life span was five years, from 1[SUP]st[/SUP] October, 1997 to 30[SUP]th[/SUP] September, 2002. However, before the expiry of the tenure, the Corporation was granted a new lease of life by the Parliament for another period of five years up to 30[SUP]th[/SUP] September, 2007.

  In April 2007, the National Assembly passed an amendment to the Act through Act. No. 10 of 2007, granting the Corporation another new lease of life up to 30[SUP]th[/SUP] June, 2011. The amendment also vested all the remaining activities from the Loans and Advances Realisation Trust (LART), Air Tanzania Holding Corporation (ATHCO) and Simu 2000 Limited, whose life spans had expired.

  In November, 2007, the Act was further amended through Act No. 26 of 2007 vesting all the remaining tasks of the Presidential Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) to the Corporation.

  Among the Corporation's key functions include holding all assets and liabilities relating to the banking business to which the former National Bank of Commerce was entitled or subject to, in respect of non- banking assets and liabilities not transferred and vested in NBC Limited or National Micro- finance Bank Limited; dealing with cases inherited from the former NBC as well as cases of the former LART, ATHCO, SIMU 2000 and PSRC; liquidation of public enterprises; and divestiture of parastatals transferred to CHC when PSRC's legal tenure expired on 31[SUP]st[/SUP] December, 2007.

  2. It is learnt that you have taken over the defunct PSRC functions. Does this also include the privatization of the remaining enterprises like NIC, NAFCO & NARCO farms etc?

  ANSWER
  The Corporation has taken over all the remaining tasks of the former PSRC when its legal existence ended on 31[SUP]st[/SUP] December, 2007. Among the tasks include the divestiture of the National Insurance Corporation (NIC), NAFCO farms and others. As for NARCO ranches the Government has decided that these should be divested directly by the sector Ministry, that is the Ministry of Livestock Development and Fisheries.

  3. It is also learnt that you have taken over LART activities of liquidating companies to pay debts owed to the defunct CRDB and NBC. How successful have you been in carrying out these functions?
  ANSWER
  As I pointed out earlier, all activities which remained when the legal tenure of LART expired were transferred to CHC. Recovery of Loans and Liquidation of assets are among key tasks of the Corporation, especially bearing in mind that CHC is technically a liquidating organization, charged with the responsibility of ensuring settlement of the former NBC liabilities against realizable assets as well as those transferred from SIMU 2000, ATHCO and PSRC. The performance of the Corporation since its inception is good. It has managed its tasks efficiently in line with its Corporate Plan. We are determined and are optimistic to complete these tasks within the given time frame of our legal mandate which expires on 30[SUP]th[/SUP] June, 2011.

  4. Both LART and PSRC were funded by the Government. Is it true that CHC is self financing its operations?

  ANSWER
  It is true that CHC is financing its operations without depending on Government subsidy. However, for the time being divestiture of the remaining parastatals and facilitation for the full establishment of EWURA, the Fair Competition Commission (FCC) and the Fair Competition Tribunal (FCT) will continue to be funded through the World Bank Credit under the Privatisation and Private Sector Development Project (PPSDP) which expires on 30[SUP]th[/SUP] September, 2009. CHC is the implementing agency of the Project.

  5. CHC is said to be monitoring and evaluating the performance of the privatised enterprises some of which have not started operating for a number of reasons. Are you going to "deprivatise" and look for other strategic investors if the current ones fail?
  ANSWER
  The Corporation's main functions are defined in sections 6 and 10 of the National Bank of Commerce (Re – organization and Vesting of Assets and Liabilities Act, Cap 404) as amended. Under this Act, CHC is legally empowered to undertake monitoring and evaluation of all privatised parastatals to determine their performance within the context of the divestiture agreements. For parastatals which have not performed since they were privatised (for your information these are very few) the Corporation will carefully study their situation and make appropriate recommendations to the Government on the way forward. New investors with be sought if it is firmly/clearly established that the existing investors have completely failed to comply with the divestiture Agreements and their Business Plans.

  6. It is said that privatisation has mainly benefited foreigners (investors). Do you agree with this argument?

  ANSWER
  The privatisation programme is being implemented in a transparent and competitive manner. Tenders are advertised in newspapers locally and internationally to invite bidders to express their interest in parastatals which are advertised for divestiture. This means that the opportunities are available to local and foreign investors without discrimination.

  Let me take this opportunity to let you know that so far more than 336
  parastatal enterprises have been divested. Out of this figure 180
  enterprises have been divested 100% to local investors compared to
  27 divested 100% to foreign investors. The remaining enterprises have been privatized on joint venture basis between the Government, local investors and foreign investors.

  In large commercial/industrial enterprises the Government has decided to retain minority shares which it will off-load to Tanzanians when the respective enterprises have shown a track record of profitability. For example the Government has already sold its shares to Tanzanians in the following companies: Tanzania Breweries Limited, Tanzania Cigarette Company Limited, Tanga Cement Company Limited, Tanzania Portland Cement Company Limited, Tanzania Oxygen Limited (TOL) and Swissport (formerly known as DAHACO). Sale through an IPO of 21% out of 51%
  of Government shares in the National Micro-finance Bank was launched
  on August 18[SUP]th[/SUP] 2008 and is scheduled to be completed within three
  weeks, that is up to September 8[SUP]th[/SUP] 2008.

  From the above explanation it is clear that Tanzanians have actively and meaningfully participated in the country's privatisation programme.

  7. There have been problems with workers retrenched after privatisation. How are you dealing with their compensation?

  ANSWER
  Workers' rights and issues are seriously considered in the execution of the privatisation programme. I wish to point out here that privatisation does not necessarily lead to retrenchment. However, in the event that retrenchment cannot be avoided, the affected employees are properly compensated in accordance with the existing labour laws and employment contracts they had sealed with their employers. For parastatals which cannot pay retrenchment benefits the Government pays them statutory entitlements. As of now almost all retrenched workers have been paid their dues. The Corporation continues to listen to workers with outstanding claims with a view to taking appropriate action in accordance with the law.
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ushahidi ukiielemea serikali, Bi Mkora( Spika) atauficha kama alivyofanya ule wa Lema na Pinda.
   
 8. l

  luhwege Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naunga mkono hoja tukipata viongozi wa aina ya Zitto 3 hakika tungesonga mbele. Tumtakie kila la kheri Mheshimiwa Zitto ktk utetezi wake
   
 9. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  huu utetezi unatakiwa usomwe mbele ya kadamnasi kwani nasi tunataka kusikia hu utetezi wa zitto
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Governments often attempt to conceal information from other governments and the public. These state secrets can include weapon designs, military plans, diplomatic negotiation tactics, and secrets obtained illicitly from others ("intelligence"). Most nations have some form of Official Secrets Act (the Espionage Act in the U.S.) and classify material according to the level of protection needed (hence the term "classified information"). An individual needs a security clearance for access and other protection methods, such as keeping documents in a safe, are stipulated.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  spika alidhnai akisema hovyo basi zitto hawezi kupata nyaraka hizo??!!!
  namshangaa sna huyu bibi
   
 12. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  There are currently 61 users browsing this thread. (12 members and 49 guests)
  JOHN MADIBA luvcyna Gottee Middle MINAKI tufikiri Shapu mankipe bennynho muhimili Lyaule Kitundu babuwaloliondo

  Spika anajipya pamoja na wasidizi wake ni vibaraka wa Mafisadi nani anabisha??
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  zito nakuongezea ushahidi.
  kwanza kataa kupeleka huo ushahidi wanao utaka wa kudai walirubuniwa.
  kama nilikusikia vizuri ulisema walishawishiwa,kuna tofauti kati ya kushawishi na kurubuni.
  nilisikia mara nyingi ukisema baraza la mawaziri limeshawishiwa lukuvi akadai uthibitishe kama kweli wamerubuniwa,hapo ukipeleka ushahidi utakuwa umekosea ni sawa na mtu akustaki kwa kosa la kuuwa kumbe bado mtu yupo haspitali.
  subiri mpaka watakapoleta madai ya kuthibitisha kama wameshawishiwa ndipo upeleke ushahidi.

  wapige bao hao magamba mtuy wangu kwa ushahidi zaidi nipm nikupe data hapa hata mkono haoni ndani.
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Magamba mtateseka sana mwaka huu, raha tupu. Halafu nasubiri kwa hamu lile movie la THE RISE OF BALALI
   
 15. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu sana kuficha uovu na wema, magamba hilo wamelisahau wakidhani kwamba uovu wao unafichika.
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  hivi HAKUNA NAMNA KAMBI YA UPINZANI IKADAI HEARING YA MADAI YOTE YA CHADEMA WANAYOSEMA USHAHIDI ULETWE?
   
 17. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo CCM wameshikwa pabaya
   
 18. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Samahani, Eti spika Makinda ana kiwango gani cha elimu?
   
 19. T

  Technology JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Zitto bado naendelea kuamini ulipaswa kua mwenyekiti wa chadema, Is it was not a crime, to fight, for what was yours!!!!
   
 20. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zitto hawezi kukiongoza chama cha chadema? sababu muulizeni Mbowe na Slaa
   
Loading...