Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Kesi za namna hii mwanzoni zinakua na wapambe kibao,lakini watapukutika mmoja baada ya mwingine mpaka itabaki familia tu.
Wakati wa kesi ya Babu seya na wanawe,watu walifikia hatua ya kuandamana,lakini sidhani kama kuna kati yao anaekwenda gerezani
Mabosi wake tangu awekwe nondo hawajamuona, maana nn?
 
Zitto alivyo na siasa za bila kumtukana MTU
Wala kumvunjia heshima mtu

Alipaswa kumpa ushauri huo lema
Ili afanye siasa za akili na sio kutafuta kick kwa matusi
Pole sana kazi ya kuhukumu waachie mahakama.
 
Zitto haaminiki na hata maneno yake hayaaminiki.huyu sio Zitto yule tunayemfahamu wa enzi zileeee.Yeye aseme alikuwa anatafuta mwanya wa kumsalimia mke wa Lema bhassss
 
Zitto alivyo na siasa za bila kumtukana MTU
Wala kumvunjia heshima mtu

Alipaswa kumpa ushauri huo lema
Ili afanye siasa za akili na sio kutafuta kick kwa matusi

Acha kujitoa ufahamu we kjana,even if unalipwa 7500,matusi yanayoporomoshwa na viongozi wa chama chenu dhidi ya wapinzani hailezeki!!!!!,kuanzia huyo boss wenu mpaka ninyi vibarua..acheni kuwaonea watu kisa dola inawasuport,haya mambo yanamwisho...MSIJIDANGANYE..
 
Zitto haaminiki na hata maneno yake hayaaminiki.huyu sio Zitto yule tunayemfahamu wa enzi zileeee.Yeye aseme alikuwa anatafuta mwanya wa kumsalimia mke wa Lema bhassss

Enzi zipi! Enzi zile za List of shame?
 
Huwa najifunza mengi sana kwa zitto kabwe ni mtu mstaarabu na pia mvumilivu na ni mwanasiasa wa kweli aisekuwa na lepe la unafki
Si rahisi kivile kuwa mwanasiasa bila kuwa mnafiki. Ili uwe mwanasiasa wa kweli na nguli kweli kweli lazima u-blend unafiki na ukweli pamoja.

Mi namkubali san tu ZZK. Unafiki wake si wa kiwango kikubwa sana. Kwa hili na kumtembelea Lema (kama story hii ni ya kweli) amefanya jambo jema la kuigwa na wapenda haki wote.
 
Hiyo haki anayopigania lema ambayo haipo ni ipi. inafaa kudefine watu wajue wazi lema na upinzani siku hizi mnapigania nini. kama ni haki ya kutukana viongozi matusi ya nguoni tujue. kama ni haki kuleta siasa za maono au za kidini tujue. zitto hapa anacheza unafiki kwa watu waliyomfukuza kwenye chama chao kwamba ni msaliti. siju anategemea kupata nini.
 
Wasiokuwa akiri kichwani wataamini Lema hajafanya upumbafu

Umejiunga juzi hapa unaleta mambo ya kike ukidhani watu tunafagilia huo uonevu wa kipuuzi. Maendeleo yamewashinda kuleta mmebaki kutumia dola kunyanyasa wengine. Sifa aliyonayo huyo mkuu ni kutumia ubabe usio na faida kwa taifa, kuna mikataba kibao mpaka sasa inaliumiza taifa hamna lolote la maana zaidi ya kujiboost na madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…