Ni kweli kwa Tanzania ana haki ya kwenda mahakamani lakini hana haki ya kurudi na ushindi, hata kama akirudi na ushindi itakuwa very late 2015 mwezi mmoja kabla ya bunge kuvunjwa rasmi.kwani huyu kafulila hana haki ya kukata rufaa mahakamani? grounds anazo nyingi sana ikiwemo mamluki waliochahaguliwa na mbatia kwani alisahwapnga kumkataa,mbatia kawa a judge on his own course.
pili tuhuma zake zimethibitishwa pasipo kuacha mashaka??? walifikiria wananchi waliomchagua? kwanii wasiige kwa wenzao magamba
¨kule hata uwe fisadi mla watu haufukuzwi chama unaambiwa vua gamba iweje chama chenye wabunge wawili watatu wamtimue uanachama huku wakijua wanapoteza mbunge na ruzuku itapunguzwa??
huyu mchaga kadata kabisa kaniudhi sana,Kafulila hebu rudi kasulu pale nunua radi ya sh 20 tuma kwa mahasimu wako. Waambie ni kwanii Malecela haendi Kigoma.
Akienda mahakamani si bado anakuwa mbunge? Mpaka mahakama ihalalishe?Ni kweli kwa Tanzania ana haki ya kwenda mahakamani lakini hana haki ya kurudi na ushindi, hata kama akirudi na ushindi itakuwa very late 2015 mwezi mmoja kabla ya bunge kuvunjwa rasmi.
Naanza kupata hisia hoja ya Magamba kufuta Chaguzi ndogo kupata nguvu zaidi. Lets wait and see.
Sasa mbona watu wa Kigoma ndiyo wanakaribishana wenyewe?
CDM inatakiwa iwe makini sana na hii jamii inayotokea jirani na Burundi!
Anarudi kufanya nini wakati alisema CDM ni chama cha kikanda?faida ya kuropoka ndio hiyo.Kama alipiga magoti kwa Mbatia basi awapigie magoti wana CDM kwa maneno yake ya kebehi ili asamehewe.Bado yeye ni kijana mpambanaji ila tuu nidhamu ni ziro.
Jamani uchumi wa nchi yetu hivi sasa tunavyoingia mwaka mpya 2013 ni tete kuliko unavyoweza kufikiri. Pengine tukikuwekea ushahidi hapa, kama ni kigogo pengine tutakusikia tena tu hospitali ya Apollo kule India. Usipime kaka!!!
Swala la Kafulila linaonyesha jinsi gani sheria ya mgombea binafsi ni ya muhimu sana nchini kwetu. Sasa hivi jambo linaloonekana mbele yetu hapa ni la watu wawili waliogombea Ubunge katika majimbo yao; mmoja akashinda na mwingine akashindwa. Sasa yule aliyeshindwa akatokea kuwa ni mwenyekiti wa chama kilichowasimamisha wagombea hao wawili. Kutokana na uneyeyekiti wake, anaamua kumvua unachama mbunge aliyechaguliwa na wanachi kwa kujua kuwa hatua hiyo itamvua ubunge pia.
Kwa wenzetu kama Marekani, mtu unaweza kuchaguliwa kwa kupitia chama kimoja halafu ukaamua kuachana nacho na kuingia chama kingine kama vile alivyofanya Senator Arlen Spector alipohama kutoka Republican na kujiunga na Democrat. Utaratibu wetu unaonyesha jinsi gani wapiga kura wasivyokuwa na sauti kwani mgombea wao anaweza kuvuliwa kiti chake kirahisi tu kwa vile eti hakubaliani na mwenyekiti wa chama chake. Na hiyo ndiyo tabia mbaya tunayotaka ikomeshwe mara moja kusudi wabunge wetu wasitumike kama rubber stamp tu.
Kama Mbatia anaona kuwa hatua aliayochukua ni sawa, je atawakemea nini wabunge wa CCM wakiamua kukubalia kila upupu unaoletwa na serikali bungeni iluhali serikali hiyo inaongozwa na mwenyeketi wao ambaye akitumia madaraka yake kama Mbatia anaweza kuwafukuza wote kutoka ndani ya CCM na hivyo kupoteza ubunge wao?