Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa

Zitto amemtuma ofisa wake kuisemea CHADEMA kuhusu Lowassa

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
2,650
Reaction score
6,088
Ofisa mmoja wa chama kiitwacho ACT ambaye mara kadhaa amenukuliwa akiwa ni msemaji wa chama hicho, ameandika na kueneza habari mtandaoni kuwa kada mwandamizi wa CCM Edward Lowassa anahamia CHADEMA!

Inashangaza kidogo! Ama ni kwamba wahusika wa chama hicho hawana uratibu wa mawasiliano kiasi kwamba kila mtu anaweza kujiandikia tu au wanaendelea kukubuhu katika siasa nyepesi.

Itakumbukwa juzi mara baada tu ya majina 5 ya makada wa CCM yaliyokuwa yamepitishwa kwenye CC ya chama hicho kuwa yamejulikana (kwa kadri ya utaratibu wao), kiongozi mkuu wa ACT, Zitto, haraka haraka kama ilivyo kawaida yake akakimbilia mtandaoni kuandika kuwa Edward Lowassa anajiunga na ACT na atakabidhiwa kadi.

Wafuasi wa Zitto kwa kuendekeza siasa nyepesi za umaarufu wa mtu, wakakimbilia nao mitandaoni kusema kuwa tayari Lowassa ameshajiunga na ACT na kwamba ni Mgombea urais na 'taswira na nuru' ya chama tayari kapewa cheo cha Uwaziri Mkuu, alas!

Hawakuishia hapo. Wakaenda mbali hata kughushi nembo ya moja ya mashirika makubwa ya habari duniani kisha wakaandika mambo yanayokidhi matamanio yao, kwamba Lowassa kahamia ACT na Zitto kamkabidhi kadi.

Sasa haijajulikana hiyo kauli ya Zitto imeishia wapi ndani ya masaa 48 tu ghafla ofisa wake amekwenda mitandaoni akijigeuza kuwa msemaji wa taasisi isiyomhusu kuwa Lowassa amehamia CHADEMA.

Tumsaidie Zitto asiendelee kufanya siasa nyepesi. Alikuwa mtu wa kwanza kumkaribisha Lowassa kwenye chama chake mapema kabla hata hajachukua fomu ndani ya CCM. Sasa awaambie watu wake vizuri hilo 'deal' limeishia wapi?

Taarifa kutoka vyanzo vyangu zinasema kuwa Lowassa atafanya mkutano na waandishi wa habari kesho saa 3 huko Dodoma. Atakachozungumza anakijua vizuri yeye labda na watu wake pia.

Habari hizo kwamba Lowassa amehamia CHADEMA hazina ukweli wowote. Zinatengezwa na kupikwa na hao 'vijana' kwa maslahi wanayoyajua wao.

Kwa kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA, tunaendelea na maandalizi ya kwenda kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kushika dola na kuongoza serikali kuwatumikia Watanzania. Kila kitu kinakwenda sawa. Maandalizi karibu yote yamekamilika...ni #UKAWA Julai 14.

Hilo ndilo suala la msingi kwa sasa. Baada ya giza totoro la siasa za ghiliba, rushwa na hila huko Dodoma kwa takriban mwezi mzima, wananchi wanasubiri nuru ionekane Julai 14 kupitia UKAWA. Yamebakia masaa mchache kuuona mwanga unaosubiriwa na Watanzania wote wapenda mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, si mabadiliko ya majina na sura za watu kutoka mfumo ule ule uliotukwamisha hapa tulipo.

Makene
 
ZZK sasa kabaki kuendesha gari kwa mafuta kijiko(Kwa kudaka matukio). Lowasa aende zake ACT, CCM kwa mdomo wao wammalize ZZK na ACT yake kwamba kundi la wasaliti,wezi waliotoka kila chama.CDM Hawawezo fanya makosa hata ya kumhurumia.. Lowassa aache siasa au acheze ktk mipaka ya CCM na kuwadhoofisha kutokea ndani.
 
Sioni ubaya lowasa akihamia ukawa kama umma unaimani nae.ccm ilimkata jina kukiuka maadili,kwa ukawa hajakiuka maadil
 
Sioni ubaya lowasa akihamia ukawa kama umma unaimani nae.ccm ilimkata jina kukiuka maadili,kwa ukawa hajakiuka maadil
Bahati mbaya sana....Lowasa yupo ktk option Mbili ama yeye au CCM sio wao kwa pamoja.Lowasa kuhama chama CCM watapunguza kiporo kimoja ...CCM HAWAJAWAHI WAAMBIA WATZ KUVUA GAMBA KULIISHIA WAPI.Lowasa akitoka CCM watasema wao ndio wamemvua kwa kumkata jina,CCM ndipo watamwita Gamba..na hata akipiga kelele sana kwamba anajua siri za CCM bado watamwambia ni kwa vile katemwa....kilio chake kitafanana na ZZK.Na huko alipoenda watasema ni kambi ya Magamba na mafisadi.
 
Kumbe bado ngoma mbichi, mara nyingi Zitto huwa ni microphone ya wakubwa, wakubwa wananong'ona yeye anapaza sauti zao. Tuone kama ni kweli!
 
Hivi kuna watu wanamwamini zito. Lowasa kaficha jambo kubwa analolijua na kamwe hawezi toka CCM atatangaza anastaafu siasa na kurudi kijijini. Lakini naamini kuna siku tutasoma nini kilotokea mpaka akajiuzulu, but it will be too late.
 
Ile Audio Clip ni pure sauti ya Zitto lakini mwenyewe amekana fasta.
lowasa akienda act tunapiga bao la kisigino,ataenda na wafuasi wa ccm na vigogo,ccm wakigawanyika wengine ACT ukawa tunatoboa bila kwere chali angu
 
Kumbuka UKaWa wanapiga vita majizi ya raslimali za taifa, maongo, mafisadi ambapo Lowasa ni mmoja wao. Ninaona kama unamiss point kiongozi. Ni kwamba Lowasa alikiuka maadili ya UKAWA aliyakiuka alipoanza ujizi na mikataba fake ya richmond.

UKaWA ni kinyume cha Ccm kwa mambo yote. Wakati ccm inafagilia Ufisadi,uwongo, hadaa, udanganyifu, kubebana, hila, kutokutumia akili na kuendeshwa na tamaa binafsi badala ya maslahi ya umma, UKAWA ni kinyume cha hayo. Kwa hiyo fisadi Lowasa na UKAWA ni maji na mafuta!.

Sioni ubaya lowasa akihamia ukawa kama umma unaimani nae.ccm ilimkata jina kukiuka maadili,kwa ukawa hajakiuka maadil
 
Makene, wewe ni msemaji wa chama, tena taasisi kubwa sana. Wakati mwingine unaiaibisha CHADEMA. Usikurupuke kijana, sio lazima kila kitu kujibu, yaani wewe unajibu kila kitu. Mi nadhani viatu ulivyopewa vimekupwaya. CHADEMA ni taasisi kubwa, mnatuangusha na siasa za kitoto kama hizi. Mungu bariki CHADEMA
 
Zitto ni mdogo sana kwa Chadema, lakini mbona mnamuattack kila siku? Zitto au afisa wa ACT, msipende kuwajibu. Kumjibu mtu kama Zitto na wafuasi wake ni kuwapa umaarufu wa kijinga. Hizi siasa za kihuni sijui mwisho lini
 
Ni kweli chipa GM. Kama ana madaraka makubwa cdm sio vizur kuandika habar zisizokuwa na reference. Kwamfano hamtaji jina na wapi hiyo habari imetoka. Ni kama umbea vile
 
Last edited by a moderator:
Asante Kamanda Tumaini Makene, hawa Act wameishiwa Hoja sasa wameanza kuwa vioja. Chadema tuko imara na tunazidi kuimarika. Tumeanza na Mungu, tupo na Mungu na tutamaliza na Mungu.
 
Sawa kabsa mikeimani kwakweli hawa vijana wenzetu wakati mwingine tunabidi tuwasaidie na kauli/ matamko yenye mihemko. Mfano ni ile kauli ya Nape ya goli la mkono, ni kauli ya kipuuzi sana, haitakiwi na Makene/ vijana wengine wa Chadema na wao wawe na vikauli kama hivyo. Tunaposema Chadema ni mbadala wa CCM lazima mjitofautishe kwa kila kitu, sio blah blah za kitoto. Wabunge wa Chadema wanafanya kazi nzuri sana, tatizo ni hawa vijana walio nje.

Alafu hizi siasa za kusema watu zimepitwa na wakati, cha kukusaidia tu bwana Makene, usipende kumponda mtu yeyote tena bila sababu. Mfano unamponda Lowassa kwa kipindi kama hiki cha uchaguzi, wakati ambao mngeweza kupata advantage ya kura za wapenzi na wafuasi wa Lowassa ambao wameumizwa na mtu wao kukatwa, sijasema mumpe uanachama Lowassa. Vijana mkue, msidhani ukamanda ni kuvaa magandwa tu, ni pamoja na kuwa na akili beyond CCM. Mungu bariki Chadema.
 
Makene: Ukiamua kusema ukweli basi sema ukweli wote.

Mimi sina tatizo na wewe kujibu huo upotoshwaji uliofanywa na huyo "Afisa mmoja wa ACT". Kwani upotoshwaji ukikaliwa kimya watu wanaweza kufikiri ni kweli.

Mimi tatizo langu liko kwa kusema nusu ukweli, Zitto unamtaja moja kwa moja kwa jina tena zaidi ya mara nne. Lakini huyo "Afisa mmoja wa ACT" humtaji kwa jina, unaishia kusema tu "Afisa mmoja wa ACT". Je hana jina huyo Afisa? na hapa ndio inaonekana habari yako ina mushikheri, aidha ni ya kutunga au huna uhakika na ulichoandika.
 
Hivi kuna watu wanamwamini zito. Lowasa kaficha jambo kubwa analolijua na kamwe hawezi toka CCM atatangaza anastaafu siasa na kurudi kijijini. Lakini naamini kuna siku tutasoma nini kilotokea mpaka akajiuzulu, but it will be too late.

Mkuu tuko pamoja hapa. Naungana na bandiko lako kwamba sio rahisi Lowassa atoke CCM na kujiunga na upinzani kwani anajua fika ni kitu gani kitampata. Lakini pia hawezi kujiunga ACT ambayo ni team B ya CCM. Akifanya hivyo na agombee urais kupitia ACT atakuwa ameipa UKAWA njia rahisi ya kwenda Ikulu kwani Lowassa hatagawa kura za wapinzani bali atazigawa za CCM.

Lowassa kama ulivyosema anaweza kutangaza kustaafu siasa lakini sio rahisi atangaze kuhama CCM.

Tiba
 
Back
Top Bottom