Zitto amburuza Kilewo polisi

Zitto amburuza Kilewo polisi

Status
Not open for further replies.

mawenge

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2012
Posts
286
Reaction score
71
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.

Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.
 
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

"Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine," alisema Kileo.

Mfa maji haachi kutapatapa. So my comrade Kilewo vuta subira na hakika kesi hii utashinda na hatimaye litakuwa pigo lingine tena kwa Zitto na hatimaye tutamsahau kabisa kisiasa. Walikutengenezea ya UGAIDI sembuse hii. Shame on them.
 
Mimi hapa ndio napozidi kumuona Zitto ndumi la kuwili,kwa sababu kwenye press conference hakukanusha wala kufafanua waraka huu wa yeye kuhongwa pesa na pia kushirikiana na TISS na hata hajazungumzia uhusiano wake na Jack Zoka na Ighondu na mnyumbuliko wa pesa hizo kutoka NMB kwenda Ujerumani kwa Andrea na pia kuwatumia wakina Kitila,Mwampamba,Mchange,Ben Saanane,Juliana Shonza etc.

Baadala yake kakimbilia Polisi na kufungua defamation case ili suala hili liishe kimya kimya na kuepusha kwa Zitto kufafanua bali Kileo na obviously Polisi inajulikana kwenye siasa inavyotumika!!

Ben Saanane upo kwenye waraka ule kuwa ulitumiwa pesa na Zitto,please tueleze ulipewa kwa minajili gani??!!
 
Tusiibeze hii ishu unajua wanaweza kujipanga wakamtoa mtu kafara, sii huwa unaona ushirikiano wao hata kwenye mawasiliano ya E-mail? Huku unamkuta Mwigulu, kule Emmanuel Mnchimbi, pale unamkuta Lukuvi na hapa unamkuta Zitto. Kila ishu inayofanywa na hawa watu inabidi tuitupie macho yoote siwaamini kabisa toka nimesoma ule mpango wa 'kumpumzisha' Waryoba
 
Wote tunajua kuwa Ben Saanane ni verified user member wa JF.... Ombi laku ni kumtaka aje athibitishe kama kweli alitumiwa mgao wa vijisenti kutoka kwa Prezooo! Na zilikuwa kwa lengo lipi? Kama alilipwa kwa kupiga deki nyumbani kwa ZZK - Prezooo atueleze... Plz Mods muiteni Ben Saanane aje kujibu......
 
Mimi hapa ndio napozidi kumuona Zitto ndumi la kuwili,kwa sababu kwenye press conference hakukanusha wala kufafanua waraka huu wa yeye kuhongwa pesa na pia kushirikiana na TISS na hata hajazungumzia uhusiano wake na Jack Zoka na Ighondu na mnyumbuliko wa pesa hizo kutoka NMB kwenda Ujerumani kwa Andrea na pia kuwatumia wakina Kitila,Mwampamba,Mchange,Ben Saanane,Juliana Shonza etc.

Baadala yake kakimbilia Polisi na kufungua defamation case ili suala hili liishe kimya kimya na kuepusha kwa Zitto kufafanua bali Kileo na obviously Polisi inajulikana kwenye siasa inavyotumika!!

Ben Saanane upo kwenye waraka ule kuwa ulitumiwa pesa na Zitto,please tueleze ulipewa kwa minajili gani??!!

usimchokoze kamanda Ben,ana ushahidi mtamu zaidi ya sms ya mpesa.Zitto anasubiriwa kwny mahakama ya wananchi
 
..

....ha ha ha ha ha ha unapotaka kufanya jambo lazima utambuwe kupata matokeo ya aina mbili....
 
WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

"Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine," alisema Kileo.

Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.
Hizi sasa sarakasi. Hivi yule aliyeuweka waraka ule kwenye blog yake siye huyu? Mbona mnacheza na akili za wananchi!
 
Very strange, ZITTO ka panick kabisa how childish yaani hasira za Mkizi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom