Zitto alia na Tembo wetu

Zitto alia na Tembo wetu

nice 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
747
Reaction score
520
Operesheni linda tembo pambana na ujangili

Zitto Kabwe
Toleo la 277
16 Jan 2013
MWAKA uliopita, ulijaa habari za kukamatwa shehena za meno ya tembo kutoka Tanzania huko Hong Kong zikielekea China. Desemba, shehena ya tani 1.3 ya meno ya tembo iliyofichwa kwenye magunia ya alizeti ilikamatwa na maofisa forodha wa Hong Kong.

ivory.jpg


Shehena hii ilikuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 1.5. Wiki mbili kabla, takribani tani nne za meno ya tembo zilikamatwa huko huko Hong Kong. Kwa matukio haya mawili, hawa ni sawa na tembo 900 waliouwawa.

Desemba hiyo hiyo, 2012, polisi mkoani Arusha walikamata nyara nyingi za serikali eneo la Kisongo. Nyara hizo ni pamoja na ngozi za Simba na wanyama wengine, pembe za ndovu na wanyama wengine na vichwa vya wanyama.

Nyara hizi zilikuwa tayari kwa kuuzwa nje ya Nchi. Mkoani Katavi walikamatwa majangili kadhaa na kuachiwa huru kwa amri kutoka ‘juu' kwa mujibu wa taarifa za maofisa wa wanyamapori.

Ujangili umeshamiri sana na kwa kasi ya kutisha. Takwimu za serikali zinaonyesha mwaka 2010 tembo 10,000 waliuwawa Tanzania pekee. Hii ni sawa na tembo 37 kila siku. Hali imekuwa mbaya zaidi mwaka 2012, jumla ya tembo 23,000 waliuwawa sawa na wastani wa tembo 63 kila siku.

Kwa hesabu ya haraka, kutokana na kasi hii ya ujangili, ifikapo mwaka 2017/2018 Tanzania haitakuwa na tembo hata mmoja. Hivi sasa Tanzania ina tembo kati ya 150,000 na 170,000.

Maofisa wengine wa wanyamapori wanasema tembo wanafika 250,000 na nusu yao wapo Pori la Selous- kusini mwa Tanzania. Sote tunawajibu wa kulinda urithi huu.

Kasi ya ujangili imechangiwa na mambo mengi lakini kubwa ni kukua kwa uchumi wa China na nchi nyingine za Kusini Mashariki mwa Asia. Kwa hiyo, takribani nchi zote za Afrika zenye tembo zinaathirika na biashara hii ya pembe za ndovu.

Tanzania, Kongo-Kinshasa na Msumbiji zipo kwenye hatari zaidi ya tembo wake wote kumalizika kutokana na nguvu kubwa waliyonayo wafanyabiashara wa pembe za ndovu.

Kenya na Nigeria inasemekana jumla ya tembo 25,000 waliuwawa mwaka 2011 pekee. Inadaiwa kuongezeka kwa wafanyabiashara wengi kutoka China na pia wafanyakazi kwenye kampuni za kichina kuzagaa Afrika, kunachangia kwa kiasi kikubwa ujangili na biashara hii haramu.

Mtandao wa ujangili ni mpana na wenye nguvu za pesa, kisiasa na kimamlaka. Mtandao huu huanzia chini kabisa kwenye mapori na hifadhi ambako wauaji ni watu masikini wa vijijini na wengine hutumia magobole tu.

Hawa hulipwa kwa kuua tu. Wakataji nao huingia hapo na kukata meno na kuandaa usafiri ambao hufanywa wakati mwingine na magari ya serikali.

Hivi karibuni gari za polisi, Muhimbili na hata magari ya baadhi ya viongozi wa dini yamekamatwa yakiwa na meno ya tembo huko mkoani Iringa.

Baada ya kusafirishwa na kufikishwa maeneo ya mijini hufungwa na kusafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Katika mtandao huu kuna watu wa vijijini, masikini ambao hutumia ujangili kama sehemu ya kupata kipato.

Pia kuna watu wa kati kama maofisa wa polisi, maofisa wanyamapori na madereva wa magari ya serikali wenye tamaa. Juu kabisa kuna wafanyabiashara wakubwa na inadaiwa wamo wanasiasa wanaolinda biashara hii.

Nikaribia kumaliza kitabu cha kurasa 301 kiitwacho "Killing for Profit: Exposing the illegal Rhino Horn Trade" ambacho kimeandikwa na mwandishi wa habari, Julian Rademeyer wa Afrika Kusini.

Kitabu hiki ni cha uchunguzi, mwandishi amechunguza mtandao mzima wa biashara haramu ya meno ya faru. Mwandishi anasema, kule nchi za Kusini Mashariki mwa Asia kama Vietnam, meno ya tembo na faru yana bei kubwa kuliko dhahabu na dawa za kulevya.

Anasema biashara hii imejaa tamaa za mali na rushwa ya kiwango cha juu. Mwandishi anaonyesha kwa ushahidi namna biashara hii ilivyotumika kuendeleza vita Msumbiji na Angola kwa nguvu ya serikali ya makaburu.
Hata baada ya ukaburu kuisha anaonyesha namna ambavyo wanasiasa watawala wanaendeleza biashara hii na kupata fedha za kampeni.

Katika kitabu hicho, mwandishi anathibitisha kuwa meno ya tembo na faru huko Asia hutumika kama mapambo kwa kutengeneza bangili zenye bei aghali na mapambo mengine kwenye mikufu na hereni. Hata hivyo, anasema meno haya hutumika kama dawa na hasa dawa za kuongeza nguvu za kiume kwa wanaume na hivyo kusababisha bei yake kuwa kubwa sana.

Jinsi uchumi wa mataifa hayo unavyokuwa na kuongeza watu wa tabaka la kati, ndivyo mahitaji wa meno ya tembo na faru yanavyoongezeka. Mwandishi anaonyesha kwamba mwaka 1960 kulikuwa na faru 100,000 katika nchi za Zimbabwe na Afrika Kusini. Hivi sasa kuna faru 2400 tu.

Nadhani ni muhimu kupata pia takwimu za Tanzania kuonyesha hali upande wetu ikoje. Watafiti waliofanya tafiti kwenye eneo hili watujuze.

Jambo moja lipo wazi hapa Tanzania ni kwamba maeneo ya Hifadhi za Taifa takwimu za ujangili ni chache kuliko maeneo ya mapori ya akiba kama Selous. Hii inatokana na ukweli kwamba maeneo ya mapori ya akiba uwezo wa nchi kulinda wanyama ni mdogo maana hakuna askari wa kutosha na waliopo maslahi yao ni madogo.

Hivyo moja ya mapendekezo ya dhati ni kuimarisha ulinzi kwenye mapori ya akiba. Pori kama Selous ambalo ni urithi wa dunia ni vema liundiwe mamlaka yake (Selous Games Authority) kama ilivyo Mamlaka ya Ngorongoro.

Mapori mengine yawekwe chini ya wakala wa serikali na yawezeshwe kutokana na mapato ya uwindaji wa kitalii.

Lazima kutoa motisha ya kutosha kwa askari wa wanyama pori na pia kutoa adhabu kali kwa askari atakayejihusisha na ujangili.

Hata hivyo, wataalamu wa wanyamapori wanasema ‘kuua majangili hakuleti mafanikio yoyote. Kuna watu wengi masikini wapo tayari kuingia kuua tembo ili wapate pesa kidogo.

tembo.jpg


Hata ukiua mamia yao, hawatamalizika. Suluhisho pekee ni kuua soko la biashara hii haramu. Soko hili litakufa kwa kuusambaratisha mtandao wa ujangili kwa kuanzia na wafanyabiashara wakubwa.

Hii ndio opresheni. Operesheni linda tembo. Sasa ianze. Tafuta namba ya simu ya mbunge wako au mbunge yeyote mwandikie "nataka ulinde tembo wetu; "Operesheni Linda Tembo kwa kuihoji na kuiwajibisha Serikali". Mabadiliko ni mimi, ni wewe, ni sisi. Tumia simu yako kutaka viongozi wako wawajibike. Ni wajibu wetu kikatiba kulinda urithi wetu.

Source Raia Mwema - Operesheni linda tembo pambana na ujangili

Ushauri wangu: Tujadili mada na sio mtoa mada wala mleta mada, maana JF sikuhizi inageuka kuwa kijiwe cha majungu, kwa mtindo huo Tanzania haitasonga mbele.

Mimi binafsi nimeshawasiliana na MB wangu kumwambia aihoji Serikali
 
Tumelia siku nyingi na wengi wamelia lakini hakuna kinachofanyika...

Its about time tuache kulia na kufanya vitendo (nadhani kwa jamaa kuwataja wale wezi wa pesa zetu Uswisi itakuwa mwanzo mzuri).., Ama sivyo tutaendelea kumsaidia kulia mpaka machozi yakauke
 
Baada ya kesi ya masalia anajigaganua huyo kaposti mwenyewe hapa kucheki upepo oya mdebe umeziba bro chauma is there for you
 
Kiasi nafarijika kuona japo wapo watu wanaotetea maliasili zetu
Uhalisia kwa kweli wanyamapori wanauwawa kwa kiasi kukubwa sana na yanayofanyika kwenye mapori haya ya akiba, WMA,open areas na hata national park ni ya hatari na mtandao huu sio mdogo wa hawa majangili wanaoua wanyamapori.
Nguvu za ziada zinahitajika kuusambaratisha mtandao huu na sio kuwakamata wanavijiji ambao wengi wanakuwa wametumwa au wana watu ambao wanawatuma wakafanye kazi ya kuua wanyamapori
Tutakuja kushtuka tembo na faru ni wanyama adimu kuonekana au tutakuja kuwaonyesha watoto wetu kuwa kulikuwa na mnyama anaitwa tembo au faru
 
hivi operesheni dhidi ya ujangiri wa Tembo katika hifadhi ya Seluu iliyoongozwa na Kamanda Tossi ilizaa faida gani! mbona serikali haikutoa mrejesho (feedback). walitumia mapesa ya wananchi bila faida yoyote! biashara ya meno ya tembo ni mtandao...kuanzia wawindaji ambao ni wananchi wa maeneo husika wanaolipwa na wafanyabiashara wakubwa hadi viongozi na watendaji wakuu katika serikali na wizara husika! niko worried kufikia mwaka 2020 wajukuu zetu watakuwa wakiangakia tembo katika picha tu au kama wazazi wana pesa basi watawaona katika zoo!
 
Sawa lakini swala la Uswizi lingeisha kwanza. tatizo ni kwamba tutashindwa ku_handle haya mambo!
 
....hivi operesheni dhidi ya ujangiri wa Tembo katika hifadhi ya Seluu iliyoongozwa na Kamanda Tossi ilizaa faida gani! mbona serikali haikutoa mrejesho (feedback). walitumia mapesa ya wananchi bila faida yoyote..

Jeshi letu la Polisi inabidli libadilishwe jina na kuitwa Comedians Police Academy. Na hao Maafisa waandamizi kama Kamanda Kova na Tossi vyeo vyao vibadilishwe, vianze na Maneno: Professional Comedians ....... Ebu jaribu kuitafakari Sinema ya Joshua Mkenya ambayo kila uchao inaongeza episodes, uunganishe na zifuatazo:


  • Action Cinema ya Mauaji ya Wafannyabiashara wa Madini wa Morogoro iliyochezwa na Stirling Zombe
  • Fiction Film ya Wizi wa Mishahara ya Askari Polisi iliyoibiwa ndani ya Kituo cha Polisi Msimbazi
  • Action Cinema ya Wizi wa zaidi ya 150M mbele ya Kituo cha Polisi ambazo ziliokotwa na askari na leo hazijulikani zilipo
  • Organized crime ya wizi na utoroshaji wa pembe za ndovu iliyogharimu umauti wa askari wawili Karagwe wiki chache zilizopita
Na mwisho wacha nikupe kali nyingine jinsi Professional Comedian Tossi alivyopata umaarufu. Kwa wasiojuha, Tossi hakuwa akikamata majambazi wala majambazi hawakuwa wakisalimisha silaha kwa Tossi kama umma ulivyoaminishwa! Katika sekta ya umma kuna njia mbili za kuonyesha utendaji kazi:


  1. Public Accountability na
  2. Performance measurements
Njia ya kwanza, wengi wanachokifanya ni kuuaminisha umma kwa kuonyesha tu kwamba wako kazini-wanawajibika. Matokeo ya kuwepo kwao kazini au kuwajibika kwao siyo suala la msingi na umma wetu ni mkarimu sana-hautaki shari hivyo hauhoji! Wakati njia ya pili hutakiwi kuonyesha bali kuthibitisha kuwa kweli umefanya au unafanya kazi. Jeshi letu la Polisi ni muumini wa njia ya kwanza kwa kutumia vyombo vya habari. Tossi baada ya kupewa kuongoza operation maalumu alichokuwa anafanya ni kwenda magerezani, anatoa wafungwa/mahabusu/watuhumiwa, anakwenda ghala la silaha-anaazima silaha, anaongozana na deffender zake zikiwa na mahabusu mpaka Habari Maelezo (Tollywood) kucheza sinema zake. Wananchi wakitazama na kusoma kwenye vyombo vya habari wanafurahi sana na kupongeza kusikia Jeshi lao limewakamata Majambazi wenye silaha! Wakati huo huo ujambazi mitaani na ujangili mabarabarani ulikuwa katika kasi ile ile ya kabla ya Operation lakini tu kulifanyika mkakati maalumu kutopewa coverage. Kwa jinsi hii, umma bila kufikiri mara mbili ukawa unahitimisha kwa kumuona Kamanda Tossi ni muwajibikaji na jasiri kwelikweli.
 
Mauaji ya Tembo hasa Selou Game Reserve unaendeshwa na mtandao mkubwa hasa viongozi wa serikali, Mfano kunawatu walikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kosa la uwindaji haramu, lakini wametolea na wanaendelea na maisha yao ya uwindaji haramu tena kwa kasi kubwa zaidi ya mara ya kwanza, ufuatilia kwa undani swala la hili kujua watu wanaoshilikiana nao ni viongozi wa wilaya, wakuu wa halimashauri na maasikali wenyewe. Sasa utapeleka wapi malalamiko yako ili swala hilo la uwindaji haramu litokomezwe litokomezwe? Hapa tutakua tunacheza ngoma tusiojua, kama kweli tunataka kulitokomeza swala hili ni kushirikana wote kuwatoa madarakani wa MACCM kwani hawa wameweka mfumo wa kuharibu kila rasilimali iliopo Tanzania. Kumpigia simu mbunge wako haitasaidia kitu kama na yeye ni mwana mtandao atafanya nini zaidi ya kukupa majibu mepesi yakua atalifanyia kazi, na wewe kurizika kua atalifanyia kazi. Ukienda vijijini hawa maharamia sio kama hawafahamiki wana fahamika sana ila ni majeruni hata kwa serikali za vijiji kwani wanajua hawawezi kuwafanya kitu, kwanza wanapesa pili wanalindwa na viongozi wajuu ambao wanashirikiana nao, fikilia katika kijiji kimoja kwenye mbuga ya Selou kinaitwa Mbuga wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro kilo moja ya meno ya tembo inauzwa laki moja(100,000) tena mchana kweupe bila woga, huku Gari la serikali ikibeba mzigo huo unategemea kutafanyika la maana katika kuzuia ujangili usiendelee,Maisha magumu MACCM wamefanya watu wawe na maisha magumu kwanini mtu asifanye ujagili ili aendeshe maisha yake. Naongea haya sio kama natunga huu ni ukweli kwani miongoni mwa watu wanaofanya biashara hio walisha nifata na kuniambia nishilikiane nao kwa kuwaletea risasi za kupia na mimi nitapata mgao wangu baada ya kazi lakini niliwakatalia kufanya biashara hio. Ili kukomesha swala hili hatuna budi kuwaondoa MACCM madarakani la sivyo tutakua tunacheza tu kwa kuwapigia simu wabunge wetu.
 
Back
Top Bottom