Zitto akataa posho ya mil. 238

Ama Kweli you can not win with People...
Angechukua angelaumiwa..., anazitoa msaada pia lawama ?

Ama kweli Binadamu Mpuuzi, Ukimfadhili atakuuzi, Bora Mfadhili Mbuzi, Atakupatia Mchuzi..
 
Hata ingekuwa mimi ningekataa,ww unafikiri rostsm azizi amempa sh ngapi mpaka sasa hivi?unafikiri kwa jinsi watawala na wala rushwa wanaichukia chadema ukiweza kufanya kazi kama ya zito utapewa bei gani?
 
Reactions: Pai
Zito! Zito! Muogope Mungu! Zile ulizoenda kuchukua CRDB zilikuwa halali yako? Zile za kigeni zilizopelekwa ujermani ktk a/c ya yule dada je zilikuwa halali yako? acha hizo ndugu ni aibu kwako kudanganya umma!

Unao uthibitisho wa unalolisema au unatokwa na povu tu. Walioanzisha hizo tuhuma Mbona hawakumpeleka mahakamani kama ml a rushwa achunguzwe au unaropoka tu. Jikomboeni acheni ulimbukeni. ..
 
Zito ni tajiri mkubwa sana,inawezeka ni tajiri kuliko wabunge wote
 

Hicho anachostahili kwa mujibu wa sheria ni vema kikaainishwa, kama ni zote 238 au sehemu yake.

Na la pili sidhani kama ni sahihi kusema amezikataa, kimsingi amezipokea ila akapenda kufafanua namna atakavyozitumia. Kila anayepokea mafao hayo haramu ana namna zake za kuyatumia. Wengine watajiimarisha kiuchumi binafsi na wengine watazitumia kujiinua kisiasa kama alivyofanya Zitto..
 
Reactions: Pai
Mnafiki sana huyu jamaa, na hili linadhihirisha kuwa kweli jamaa.ni wakala wa.CCM, hivi ZZK ana tofauti gani na Mpendazoe? Kwanini yeye alipwe wakati Mpendazoe na wengine hawalipwi na serikali hii ya CCM?
 
Kina Mbowe, Lema, Mnyika, kuchukuwa milioni 230 kila mmoja na kukaa kimya siyo wanafiki?

Wewe nafuu ungekaa kimya kwani hiki unachokifanya katika hii thread ni kuuweka ubongo wako UCHI, wewe ni mwanaCCM na CCM ndio chama chenye wabunge wengi Bungeni ni vema ungejenga hoja ya kuwashutumu hao wabunge wa chama chako kuhusiana na suala hili kwani wamekaa kimya kuliko kuandika upu uzi wa kishabiki usiotumia akili.
 
taratibu mkuu zitto hakufukuzwa, zitto alijiuzuru hivyo malipo ni halali yake. kama nahisi alifukuzwa leta ushahidi

Zitto alikosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge baada ya kufukuzwa uanachama wa chama ambacho 'kwacho' alipata kuwa mbunge. Hakuwa na namna nyngine kisheria ya kuendelea kuwa mbunge. Au unataka kuniambia ulikuwepo uwezekano wa kuendelea kuwa mbunge ilhali si mwanachama wa CHADEMA? Hata wanaoshabikia kauli za kusema eti alijiuzuru naona kama hawajui wanachosema. Kujiuzuru unafanya pale ambapo unapokuwa na uhuru wa kuchagua kufanya hivyo au kuacha. Zitto hakuwa na uhuru huo. Ni sawa na yule Waziri 'aliyejiuzuru' wakati mbadala wake ameshateuliwa!
 
Mbowe kishawashika masikio hao!
Acha kuwa msukule. .au mpaka uombewe? Unao uthibitisho wa unalolisema au unatokwa na povu tu. Walioanzisha hizo tuhuma Mbona hawakumpeleka mahakamani kama ml a rushwa achunguzwe au unaropoka tu. Jikomboeni acheni ulimbukeni. ..
 

Ni lini CHADEMA walimfukuza Zitto?
 
Kwa hiyo wabunge wa UKAWA ndiyo waongee.
 

Kwa nini hakukataa zile za PAC?.
 

Kama kawaida huyu kijana ni mtu wa kutenda si maneno! Haya sasa wabunge wa UKAWA mufuate nyayo otherwise nyie ni wachumia tumbo tu kama wale wa CCM.
 

Usiangaike kijana yeye anafanya ukiuzika mshauri huyo mbunge unayempenda na yeye atangaze! Kimya chao kinaashiria nini? Kama sio uchumia tumbo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…