Zitto aiumbua Serikali

Kuna baadhi ya watu wanapenda kumpinga Mh.Zitto bila ya mantiki. Mbona hamtoi mbadala wowote kwa jitiada alizizionyesha huyu Mtanzania? Tena kwa manufaa ya Taifa wala si kwa yeye mwenyewe ama chama chake.
 
Niliwaambia hakuna hoja ya Zitto, leo siri imefichuliwa, ilikuwa hoja ya kamati tena ya mwana CCM, Zitto kwa kuwa ni "opportunist" kama alivyofundishwa na Mwenyekiti na Boss wake Katibu Mkuu akaiwahisha mbio kuwaita waandishi wa habari na kujifanya ni hoja yake. Duh!

Magwanda mmeaibishwa sana leo Jangwani.
 
Ni heri ukawa maskini wa mali kuliko kuwa maskini wa akili, Maana watanzania wanaangamia kwa sababu ya kukosa maarifa
 
Ukiona hao viongozi wa Serikali hawataki kufuata ushauri na kufanya vitu kwa faida ya taifa kwa ujumla, ujue vile wanavyoendelea kuvifanya ni kwaajili ya faida yao binafsi, ili waendelee kujizolea mabilioni kupitia rasilimali za Taifa na kwenda kujifungulia account kwenye Bank za nje ya Nchi kwaajili yao na familia zao, wanagawana uchumi wa Nchi wenyewe kwa wenyewe na kuwaachia wageni uhuru wa kuitumia Nchi wanavyotaka, wao wafaidike, wananchi wateseke na taifa lizidi kudidimia kila siku
attachment.php


IMEDAIWA kuwa, serikali isingepaswa kuendelea kuomba msaada wowote wa fedha kutoka nje ya nchi, kama ingetekeleza mapendekezo ya bajeti ya kambi ya upinzani, yaliyotaka kupunguzwa kwa misamaha ya kodi kufikia asilimia moja ya pato la taifa, ambayo thamani yake ni sawa na fedha zote za misaada kutoka nchi wahisani.

Kauli hiyo, ilitolewa jana na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe, ambaye aliweka wazi kuwa misamaha ya kodi ya asilimia tatu ya pato la taifa ni sawa na shs trilioni 1.03 ambazo ndizo zinazotolewa na nchi wafadhili kuisaidia Tanzania.

Zitto akitangaza mwelekeo wa bajeti yake kwa mwaka ujao wa fedha wa 2012/13, na kuainisha vipaumbele mbadala, alizidi kuianika serikali na kuitaka itoe maelezo ya kina ya kwa nini imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa bungeni, kwamba misamaha ya kodi itapunguzwa mpaka kufikia asilimia moja ya pato la taifa.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema kama serikali ingeyafanyia kazi mapendekezo ya kambi ya upinzani, yangewasaidia Watanzania kupunguza ukali wa maisha, na kuboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa.

Alitaja mapendekezo yaliyopendekezwa na kambi ya upinzani, katika bajeti inayoisha, lakini yakawekwa kapuni na serikali kwa sababu zisizojulikana kuwa, mbali za misamaha ya kodi ni kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petroli na dizeli ili kushusha mfumuko wa bei.

Vipaumbele vingine vya kambi ya upinzani vilikuwa kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances) na kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Waziri huyo kivuli alisema ni mapendekezo mawili tu ya kodi za mafuta ya petroli na diseli na tozo ya SDL yaliyokubaliwa na kutekelezwa, wakati pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa, lakini serikali imeshindwa kulitekeleza, ikiwa ni pamoja na kukataliwa kwa pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao, ambalo kambi ya upinzani imerejea wito wake wa kufutwa kwa mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).

Soma zaidi...Tanzania Daima - Sauti ya Watu

 
Tuwe wa-Kweli tuache unazi... Zitto hana institution ya kuweza kutengeneza Budget ya Taifa... budget ya Taifa inatengenezwa na watu wengi sana from Vijijini to Taifa... tuache uvivu wa kufikiria. Hata waziri wa CCM pia hawezi... wale ni wasomaji tu... wa kazi iliyofanywa na watu wengi sana ambao vyama vya upinzani hawana hiyo capacity.
 
Tuwe wa-Kweli tuache unazi... Zitto hana institution ya kuweza kutengeneza Budget ya Taifa... budget ya Taifa inatengenezwa na watu wengi sana from Vijijini to Taifa... tuache uvivu wa kufikiria. Hata waziri wa CCM pia hawezi... wale ni wasomaji tu... wa kazi iliyofanywa na watu wengi sana ambao vyama vya upinzani hawana hiyo capacity.

Ulishawahi kupata bajeti mbadala ya upinzani ya mwaka wowote wa fedha? Ukijibu hili ndo ninaweza kuendelea na wewe.
 
Tuwe wa-Kweli tuache unazi... Zitto hana institution ya kuweza kutengeneza Budget ya Taifa... budget ya Taifa inatengenezwa na watu wengi sana from Vijijini to Taifa... tuache uvivu wa kufikiria. Hata waziri wa CCM pia hawezi... wale ni wasomaji tu... wa kazi iliyofanywa na watu wengi sana ambao vyama vya upinzani hawana hiyo capacity.

kama huna cha kuchangia uwe unapita tu. mchango wako hauna substance hata kidogo.
 
Misamaha ya kodi iwepo ila kuwe na mageuzi kwenye misamaha hiyo. Vifaa vyote vilipiwe kodi kwanza then kama mtu au shirika linaqualify then waende wa claim hela zao zirudishwe na hapo ndo TRA watapima uzito na kuona kama inafaa au la kurudisha na si sasa ambapo zinakatwa juu kwa juu na wakati mwingine bila kuhakiki vyema. Na isitoshe misamaha ya kodi kwa makanisa ni kidogo sana ukilinganisha na ile ya makampuni makubwa kama ya madini nk.
 
Back
Top Bottom