Zitto aiumbua Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto aiumbua Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALEX PETER, Jun 8, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]

  IMEDAIWA kuwa, serikali isingepaswa kuendelea kuomba msaada wowote wa fedha kutoka nje ya nchi, kama ingetekeleza mapendekezo ya bajeti ya kambi ya upinzani, yaliyotaka kupunguzwa kwa misamaha ya kodi kufikia asilimia moja ya pato la taifa, ambayo thamani yake ni sawa na fedha zote za misaada kutoka nchi wahisani.

  Kauli hiyo, ilitolewa jana na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe, ambaye aliweka wazi kuwa misamaha ya kodi ya asilimia tatu ya pato la taifa ni sawa na shs trilioni 1.03 ambazo ndizo zinazotolewa na nchi wafadhili kuisaidia Tanzania.

  Zitto akitangaza mwelekeo wa bajeti yake kwa mwaka ujao wa fedha wa 2012/13, na kuainisha vipaumbele mbadala, alizidi kuianika serikali na kuitaka itoe maelezo ya kina ya kwa nini imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa bungeni, kwamba misamaha ya kodi itapunguzwa mpaka kufikia asilimia moja ya pato la taifa.

  Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema kama serikali ingeyafanyia kazi mapendekezo ya kambi ya upinzani, yangewasaidia Watanzania kupunguza ukali wa maisha, na kuboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa.

  Alitaja mapendekezo yaliyopendekezwa na kambi ya upinzani, katika bajeti inayoisha, lakini yakawekwa kapuni na serikali kwa sababu zisizojulikana kuwa, mbali za misamaha ya kodi ni kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petroli na dizeli ili kushusha mfumuko wa bei.

  Vipaumbele vingine vya kambi ya upinzani vilikuwa kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances) na kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

  Waziri huyo kivuli alisema ni mapendekezo mawili tu ya kodi za mafuta ya petroli na diseli na tozo ya SDL yaliyokubaliwa na kutekelezwa, wakati pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa, lakini serikali imeshindwa kulitekeleza, ikiwa ni pamoja na kukataliwa kwa pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao, ambalo kambi ya upinzani imerejea wito wake wa kufutwa kwa mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).

  Soma zaidi...http://www.freemedia.co.tz

   

  Attached Files:

 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna jipya.
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kufutwa misamaha ya kodi ni ndoto maana kuna makundi ya kijamii yananufaika sana nayo!
   
 4. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Jipya lipo zomba, hukumbuki serikali ilipotaka kufuta misamaa ya kodi ya mashirika ya dini ni kundi gani lilimtolea macho rais?
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yani nch maskini kama tanzania inawezaje kuafford kusamehe watu kulipa kodi...dont understand
   
 6. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama hakuna jipya kwanini hatuendelei
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unafikiri Tanzania ya leo ndiyo ya jana na juzi?
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Of course. kundi mojawapo ni CCM
   
 9. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Wakifuta wakaacha kuombaomba safari za kutembeza bakuli zitatoka wapi tena?
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Leta ushahidi!
   
 11. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh.kasema mana ugumu wa maisha yanazidi kuwa magumu siku hadi siku
   
 12. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ya Leo ni maskini zaidi ya ile ya juzi na jana, wajawazito bado wanajifungulia Chini kwenye vumbi, watoto wa shule wanakaa chini, hakuna maji safi, watu wanaajiriwa lakini hawalipwi mishara, serikali ina ukata yaani ni balaa tu.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana si umesema tusimguse...tukimgusa hatutaiona kesho,Lol! zomba na wewe una mikwala kweli
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kupunguza misamaha ya kodi kutapelekea kupunguza utegemezi, na kupunguza utegemezi kutapunguza safari za Kikwete kwenda nje ya nchi kuomba misaada na Kupungua kwa safari za Kikwete kwenda nje ya nchi kutapunguza Posho zake na starehe zake nje ya nchi, na kupunguza Posho za Kikwete na starehe nje ya nchi kutapunguza uwezekano wa yeye kukubali kupunguza misamaha ya kodi. Conflict of interests :confused2:
   
 15. awp

  awp JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hizo ni ndoto, na wimbo ni uleule
   
 16. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Heri Muungano uvunjwe tu, kama wenzetu mnaongea tu juu juu bila kufafanua namna hii. Kiuchumi hamchangii chochote na hata maoni tu yanakuwa jumla jumla? Taja hata makundi mawili kujustify
   
 17. P

  PACHOTO JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  labda PENGO akubali ndio misamaha itaondolewa la sivyo ng'ooo haiondolewi na hata slaa alivimba macho macho pale waziri mkulo alipotaka kuondoa maana asilimia 90 ya misamaha ni ya kanisa ikiondolewa tu makanisa yanakufa
   
 18. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,646
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Misamaha ya kodi ni moja ya nyenzo za nyinyieme kuwabana wafanyabiashara ukiwa nao mambo yako saaafi ,maana ukisamehewa kodi huku untao kamchango kwa chama percent fulani .sasa ikiondolewe watampata nani?
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kanisa.
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,682
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa na walalahoi (ultimate consumers).
   
Loading...