Viongozi wangu Mbowe na Dr Slaa, tunawapenda sana pia tunawaamini, hebu msameheni Zitto, tunataka tuone ile triple army kama ya zamani, msameheni bila masharti.
Zitto na wewe hebu tunaomba utulie kamanda, epukana na kauli tata tujenge chama.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.
Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.
Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.
Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.
Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti, ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.
Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.
Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.
Safi sana! Nawe pia unakaribia kuyala matapishi yako. umeshayanusa na kulamba kwa mbaaali.
Nikikumbuka matope uliyowahi kumsiliba Mh.Zitto, nabaki kutahamaki tu.
Najua tatizo lilikua ni uchaguzi maana alikua ni tishio hasa kwenye uenyekiti. Na angeshinda ule ukurugenzi si ungeusikia redioni?
Anyway, ushapata ulichokua unakilinda mnalegeza misimamo.
1:Hivi alifukuzwa ndani ya chama?
3:Tuwe wakweli ,je hakuelezwa makosa yake tena kimaandishi?
Kuna msamaha wenye masharti?
Kweli kabisa , ulikuwa ni uoga wa Ucjaguzi.Wamefanikiwa MBOE MCHAGA na MNYIKA MPARE.Safi sana! Nawe pia unakaribia kuyala matapishi yako. umeshayanusa na kulamba kwa mbaaali.
Nikikumbuka matope uliyowahi kumsiliba Mh.Zitto, nabaki kutahamaki tu.
Najua tatizo lilikua ni uchaguzi maana alikua ni tishio hasa kwenye uenyekiti. Na angeshinda ule ukurugenzi si ungeusikia redioni?
Anyway, ushapata ulichokua unakilinda mnalegeza misimamo.
Mwenyekiti nae anataka kutuaminisha hiki chama ni chake sasa, kwani kuna shida gani wakasameheana kujenga upinzani wenye nguvu, najua Zitto amejutia usaliti wake na sidhani kama atarudia tena, asamehewe tu.
Zitto akisamehewa narudisha kadi Yangu CHADEMA
Nimeguswa!....nimejiona kundi langu, na reserve comments zangu kwenye hili, kuepuka kunyoosheana vidole!.
Asante.
Pasco
Siungi mkono Zitto kurejea Chadema. Lakini siamini kama Mbowe kwa ukomavu wake kisiasa na busara yake ya hali ya juu aliyonayo tangu Zitto na sisimizi wenzie walipoanza fujo hadi sasa, Mbowe hawezi kukasirishwa na visharti vya kitoto vilivyowekwa na Zitto. Mbowe kiongozi wangu mimi hababaishwi na visharti vya kijinga. Atakuwa amevipuuza hivyo visharti siku nyingi! Mleta thread lengo lako linajulikana. Ni mbinu ile ile, ya watu walewale kwa malengo yale yale. Hamtafanikiwa!Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.
Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.
Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.
Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.
Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti, ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.
Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.
Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.
Wasamani=Wa thamaniWewe ndo umeongea, Wakubwa acheni fujo hapa! Zito akirudi, UKAWA mtatikisa sana. Kila mmoja wenu ni wasamani kwa Watanzania. Tunahitaji ng'oa mbuyu 2015! Acheni malumbano!
Wasamani=Wathamani