CHAMA cha ACT-Wazalendo kimezidi kutamba kwamba ndicho chama pekee cha upinzani kinachoweza kuzungumzia ufisadi ambao ni tatizo kubwa la maendeleo nchini mbele ya wananchi.
Akihutubia katika mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti mkoani , Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe alisema vyama takribani vyote vya siasa sasa vimechafuka kwa sababu vimekumbatia mafisadi na hivyo hawawezi tena kukemea ufisadi.
Zitto alisema mgombea urais kwa tiketi ya Chadema ambaye anawakilisha vyama vinavyounda umoja wa Ukawa, Edward Lowassa, kabla hajahama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chama hicho pamoja na vyama shiriki waliueleza umma wa watanzania kuwa ni fisadi lakini sasa wamempokea na kumpendekeza kugombea nafasi ya urais, jambo ambalo limeua hoja ya ufisadi na chadema kuendelea kukumbatia mafisadi.