Zitto aitaka Serikali ya Mama Samia kuhakikisha vyama vya siasa na vyombo vya habari vitakuwa huru kutekeleza majukumu yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, yuko tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, endapo serikali yake itahakikisha vyama vya siasa na vyombo vya habari, vitakuwa huru kutekeleza majukumu yake.

Mwanasiasa huyo ametoa sharti hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana Jumanne tarehe 23 Machi 2021, wakati anazungumzia picha rasmi ya Rais Samia, iliyotolewa na Serikali.

Rais Samia amechukua madaraka kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, kwenye Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Akizungumzia utawala wa Rais Samia, Zitto amesema yuko tayari kumpa ushirikiano wake, endapo masharti yake hayo yatafanyiwa kazi.

Pia, amesema kiu yake katika serikali hiyo, ni kuona demokrasia inatamalaki kwa kuwa ndiyo suluhisho la changamoto za Tanzania.

“Ninachohitaji katika nchi yetu pendwa ni demokrasia, demokrasia ni suluhisho la changamoto zetu.”

“Nitatoa msaada wangu kwa Rais endapo vyama vya siasa vitakuwa huru pamoja na kuhakikishiwa uhuru wa vyombo vya habari,” ameandika Zitto

Wito huo wa Zitto umetolewa siku kadhaa tangu Katibu Mkuu wa chama chake, Ado Shaibu kusema kwamba ACT-Wazalendo kiko tayari kushirikiana na Rais Samia.

Akizungumza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Magufuli katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, tarehe 20 Machi 2021, Ado alisema kauli iliyotolewa na Rais Samia juu ya Watanzania kuzika tofauti zao na kusonga mbele, inaleta matumaini.

Na kwamba, anaamini mchango wa vyama vya siasa vya upinzani katika ujenzi wa nchi, utaheshimiwa kama ilivyokuwa zamani.

Rais Samia alitoa wito kwa Watanzania kushikamana na kuzika tofauti zao, tarehe 19 Machi 2021, wakati anahutubia taifa baada ya kuapishwa kushika mikoba ya Hayati Magufuli, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, baada ya kupata matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Chato mkoani Geita, Ijumaa tarehe 26 Machi 2021.

Mwanasiasa huyo aliiongoza Tanzania katika kipindi cha miaka mitano na miezi mitano 5 Novemba 20215 hadi 17 Machi 2021.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Na hoja nzito sana ni kweli mama Samia anatakiwa aliangalie Hilo pia ili turudishe amani na mshikamano waandishi wa habari waachwe wafanye kazi zao ili mradi wasivunje Sheria.Na mungu anisaidie mama Samia.
 
Hii hoja ni MFU na ninaipinga.

Zitto anataka:-
1>Ripoti ya ununuzi wa ndege 11 iwekwe hadharani, huo ufisadi si itakuwa shida?
2. Zitto anataka Ufisadi uliowekwa hadharani na PROF ASSAD iwekwe hadharani?
3. Ujenzi wa Hostel Pale UDSM uwekwe hadharani?
4. Siri ya kuuwa mifuko ya hifadhi ya Jamii iwekwe hadharani?
5. Siri ya UDA iwekwe hadhrani?
6. Siri ya MAXCOM iwekwe hadharani?
7. Ujenzi wa uwanja wa ndege chato, kivuko Busisi na tenda ya Stigle iwekwe hadharani?
Ninasimama na serikali, kusiwe na uhuru wa vyombo vya habari.
 
Kawaulize Dubai kwa nini hawana mambo ya vyama vya siasa na wana maendeleo kuliko nyinyi wenye Uhuru wa vyama vya siasa na vyombo vya habari.
Bado hujaniambia vyama vya siasa vinazuia vipi maendeleo? Hapo umenitolea mfano mmona tu, wakati kuna mifano mingi tu ya nchi zenye vyama vingi na maendeleo makubwa.
 
Hii hoja ni MFU na ninaipinga.

Zitto anataka:-
1>Ripoti ya ununuzi wa ndege 11 iwekwe hadharani, huo ufisadi si itakuwa shida?
2. Zitto anataka Ufisadi uliowekwa hadharani na PROF ASSAD iwekwe hadharani?
3. Ujenzi wa Hostel Pale UDSM uwekwe hadharani?
4. Siri ya kuuwa mifuko ya hifadhi ya Jamii iwekwe hadharani?
5. Siri ya UDA iwekwe hadhrani?
6. Siri ya MAXCOM iwekwe hadharani?
7. Ujenzi wa uwanja wa ndege chato, kivuko Busisi na tenda ya Stigle iwekwe hadharani?
Ninasimama na serikali, kusiwe na uhuru wa vyombo vya habari.
Kwahiyo unakubali kuwa hayo yote uliyoorodhesha hapo ya uwalakini?
 
Hivi inawezekanaje unamtukana mtu maisha yake yote na kumwita majina ya ajabu-ajabu, mara mshamba, mara mwizi, halafu inatokea mtu huyo anatangulia mbele ya haki unajipenyeza kwenda kutoa heshima ya mwisho. Au niseme KEJELI ya mwisho.

Kwa lugha ya kunywea juice, hiyo inaitwa hypocrisy of the highest order.
 
Mama pia aanzishe mchakato wa Katiba na Tume huru ya Uchaguzi halafu aitishe Uchaguzi ili a cement utawala wake.
 
Back
Top Bottom