Zitto aichokoza CHADEMA na kuwapa somo wanachama wake

Zitto aichokoza CHADEMA na kuwapa somo wanachama wake

Leka Tudigite kufanya kazi (biashara) na NSSF iliyo chini ya PAC ni sawa, lakin viongozi wa chama kufanya biashara na chama cha ACT ni dhambi. Kwahiyo, hii ni ahadi kama zingine, isipotekelezwa sintashangaa.
 
Zitto-akiandika-maoni-yake-2-1024x683.jpg

​



CHANZO:
Amekaa kinafiki
 
Kwenye kutangaza mtu madeni yake nadhani hili sasa wanaingilia personal life za watu. Madeni na mikopo yangu mimi binafsi yanahusikanaje na Chama? Sii ndio kesho habari ya kutangaziana Mkandara anadaiwa na CRDB mil. 10 tu zimemshinda kulipa!.

Hahahaha ndiyo ujamaa huo mkuu, ni kuvumilia tu.
 
Kunywa mvinyo kasha tangaza maji ... Association of Criminals in Tanzania ni zaidi ya FUTUHI ...
 
Zito ni msanii tena sana. Km kweli Act ni wazalendo atuambie gharama za ukumbi walzotumia na atuambie gharama za kuonyesha live masaa 3 ITV na Azam TV. Lasivyo atakuwa msanii aliyetumwa na ccm kuja kuua ukawa.

Hajamzid Mbowe kwenye usanii
 
Safi sana ZZK, sera za ACT ni matumaini mapya kwa Taifa, Ila kikubwa tunachohitaji kwenu ni siasa safi na Uongozi bora, then hapo mtapata watu, mkishapata watu mtashinda uchaguzi, mkishashinda uchaguzi mtashika dola, mkishashika dola mtakuwa wasimamizi wa Ardhi yetu, na hapo ndipo Wanaofanya siasa za kiuanaharakati na kimatukiotukio watakapojua kwamba nyinyi ni tofauti. Inaweza kuchukua miaka 50,lakini one day you will be there.
 
madeni ni kwa bqadhi ya watu au hata akina Mwigamba? manaake kama ni wote si fujo zitaanzia hapo? Manaake tumeishawahi kuona mabaunsa walivyo muandama katibu mtendaji kwa Madeni!
 
Hata Urusi wameacha na sasa Cuba inaanza mahusiano na US yeye anataka kutwambia habari za Ujamaa. Mbona anaendesha magari ya Hammer kama ni mjamaa
Sasa usipo fanya biashara Chama utaendeshaje?

UJAMAA UNATUCOST MPAKA LEO

CHINA NA URUSI WALISHA UACHA UJAMAA

AMEBAKIA KIFUTU WA KOREA TU NAYO TUNAONA NCHI YAKE ILIVYO TOFAUTI NA WENZAO WA KUSINI WALIOFATA SERE ZA UBEPARI.
 
Mleta thread umemaliza au bado anaendelea kubwabwaja huyo sultani wa makharia zzt?
 
Zitto-akiandika-maoni-yake-2-1024x683.jpg

​

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT – Wazalendo, Kabwe Zitto ameahidi chama chake kuendesha shughuli zake kwa uwazi, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku viongozi kufanya biashara na chama hicho, jambo ambalo limekuwa likidaiwa kufanyika ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Ndani ya Chadema, mara kadhaa imekuwa ikidaiwa kwamba Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, amekuwa akifanya biashara na chama chake.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa ACT-Wazalendo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Zitto, bila kutaja chama wala jina la mwanasiasa yeyote, alisema chama chake kinapozungumzia wananchi kurejesha taifa mikononi mwao ieleweke kwamba wanazungumzia uwajibikaji.

“Chama cha ACT Wazalendo kimeelekeza kikanuni kwamba kila kiongozi wa chama lazima atangaze mali zake na madeni yake. Kila kiongozi lazima aweke wazi maslahi yake ya kibiashara na mengineyo wazi ili kila anapotenda au kusema jambo wananchi wajue maslahi aliyonayo au la katika suala husika.

“Viongozi wote wa kitaifa wa ACT Wazalendo wamefanya hivyo na tutaweka saini zetu mbele yenu kama mashahidi. Naomba Mwanasheria wetu aje hapa tutekeleze matakwa haya ya kikanuni.

“Fomu hizi zitakuwa kwenye tovuti ya chama ndani ya muda mfupi ujao ili kila mtanzaina aone. Kila Kiongozi wa Chama ambaye miiko ya uongozi inamtaja anapaswa kuwa amejaza fomu hizi na kuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Uadilifu katika ifikapo tarehe 30 Juni 2015.

“Tunapopinga viongozi wa umma kufanya biashara na serikali na hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi na kushamiri kwa ufisadi, hivyo hivyo tunapinga viongozi wa chama chetu kufanya biashara na chama. Ni marufuku serikali kugeuzwa kuwa genge la watu wachache wanaopora rasilimali za umma. Uadilifu tunaoutaka serikalini ni lazima uanzie kwetu tunaohubiri.

“Tutafanya haya kwa kubadilisha siasa zetu kuelekea kwenye masuala yanayowahusu wananchi; wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara ndogo ndogo, vijana, wanawake na wazee wetu.

“Tunataka kurejesha nchi yetu Tanzania kwa kujenga uchumi wa wote. Tunaporejea kwenye Azimio, hatusemi tunakwenda kutaifisha kila kitu na Serikali kuendesha shughuli zote za kiuchumi. Tunaheshimu na kuthamini sekta binafsi na mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

“Tunamaanisha kuwa ni lazima Dola isimamie uchumi. Sio kazi ya Serikali kufanya biashara. Lakini tunamaanisha kuwa ni lazima kurekebisha baadhi ya makosa yaliyofanyika kwenye ubinafsishaji na hususan ubinafsishaji holela uliofanyika kwenye sekta ya Kilimo na kupora ardhi ya wananchi wetu na kuwageuza kuwa manamba kwenye ardhi yao wenyewe. Tunataka kutomokeza ukwepaji kodi,” alisema Zitto.

CHANZO: Raia Mwema

Pia angesema ni lini atarudisha pesa alizochukua ktk brifcaise pale crdb na zile alizokuwa anachukua kupitia kwa yule dada wa kidhungu pale ujerumani.
 
Zito ni msanii tena sana. Km kweli Act ni wazalendo atuambie gharama za ukumbi walzotumia na atuambie gharama za kuonyesha live masaa 3 ITV na Azam TV. Lasivyo atakuwa msanii aliyetumwa na ccm kuja kuua ukawa.

Mkuu huyo ni msaliti na katumwa ili kudhoofisha ukawa,ila atashindwa vibaya sana kuyatekeleza hayo.
 
Kwenye kutangaza mtu madeni yake nadhani hili sasa wanaingilia personal life za watu. Madeni na mikopo yangu mimi binafsi yanahusikanaje na Chama? Sii ndio kesho habari ya kutangaziana Mkandara anadaiwa na CRDB mil. 10 tu zimemshinda kulipa!.

Mkandara yupi mkuu huyu wa mlimani na kwao ni kule kwenye jiwe lenye mzizi?
 
Leka Tudigite kufanya kazi (biashara) na NSSF iliyo chini ya PAC ni sawa, lakin viongozi wa chama kufanya biashara na chama cha ACT ni dhambi. Kwahiyo, hii ni ahadi kama zingine, isipotekelezwa sintashangaa.

Leekadutigiiteeeee,mutoto wa maamaa
 
Back
Top Bottom