Zitto achukua fomu Kigoma mjini

Zitto achukua fomu Kigoma mjini

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
1,387
Reaction score
680
Zitto apiga tambo kuelekea bungeni

zitto.jpg


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Safari ya mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe kurejea bungeni imeanza rasmi baada ya kiongozi huyo wa chama kipya cha ACT-Wazalendo kuchukua fomu za kuwania kuongoza jimbo la Kigoma Mjini.

Uamuzi huo wa kulitaka jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amekuwa akizitoa kwa muda mrefu kuwa hatarudi tena Kigoma Kaskazini kwa kuwa alishawatimizia kila kitu na haoni sababu za kuwawakilisha tena wananchi wa eneo hilo.

Kauli yake iliibua ubashiri kuwa Zitto anataka kubadilishana jimbo na mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, uvumi ambao aliukanusha akisema hadhani kama CCM inaweza kupata jimbo Kigoma.

Zitto, ambaye alijiondoa Chadema baada ya kukiuka katiba kwa kufungua mashtaka dhidi ya chama hicho, hakufanya mbwembwe wakati akienda kuchukua fomu kwenye ofisi za ACT Ujiji jana, badala yake aliita viongozi wa kata na matawi bila ya kutaarifu vyombo vya habari.

"Nimeamua kugombea ubunge wa Kigoma Mjini ili niwatumikie ndugu zangu ambao wamekuwa wakipata tabu katika kupigania haki zao za msingi ambazo walistahili kuzipata kama ilivyo katika mikoa mingine," alisema Zitto alipoongea na mwandishi wa Mwananchi kwa simu.

"Nitakapokuwa mbunge wa Kigoma Mjini nitahakikisha barabara za mitaani zinapitika katika kipindi chote cha mwaka, nitahakikisha watu wanaacha tabia ya kulima mashamba katikati ya mitaa na makazi, lakini nitahakikisha kila mmoja anajiunga na mifuko ya kijamii ili kujiwekea akiba ya uzeeni pamoja na kupata huduma ya matibabu, elimu na nyinginezo zinazopatikana kwa kutumia mifuko hiyo."

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema bonde la Mto Luiche bado halijatumika ipasavyo kuzalisha chakula kwa wingi.

"Nakusudia kuibana Serikali ijenge skimu ya umwagiliaji maji ili wakulima walime kilimo cha mpunga kwa mwaka mzima bila kupumzika, jambo ambalo litainua uchumi wa wakulima na kuongeza chakula hapa Kigoma," alisema.

Kuhusu umeme wa gridi ya Taifa, Zitto alisema lazima upatikane ili kusaidia jitihada ya ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi na kilimo kwa kuwa hivi sasa mji wa Kigoma Ujiji unategemea umeme wa jenereta ambao hauwezi kuendesha shughuli za viwanda, hali inayochangia mkoa kuendelea kuwa masikini licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi.

Katibu wa ACT wa Jimbo la Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema Zitto alichukua fomu hiyo jana kwa malipo ya Sh100,000 mbele ya viongozi 72 wa kata na matawi kutoka jimboni humo.

"Kwa hali ya sasa Kigoma Mjini inahitaji kupata mbunge anayeweza kufuatilia mambo kwa kina ili kuleta maendeleo ya wananchi baadala ya yule anayekwenda bungeni kujifunza," alisema Ally.

"Watu wanakabiliwa na kero mbalimbali kama ubovu wa barabara za mitaani, uhaba wa umeme wa uhakika unaoweza kuendesha viwanda vikubwa na vidogo, pamoja na wengi kufanya kilimo cha kujikimu zaidi."

Zitto alitofautiana na uongozi wa juu wa Chadema uliomtuhumu kuwa alikuwa amefanya uasi na kwamba alishaanzisha chama kingine akiwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani na kusababisha avuliwe nyadhifa zote, ikiwamo ya unaibu katibu mkuu.

Hata hivyo, wakati Chadema ikijiandaa kumjadili na pengine kumvua uanachama, Zitto alifungua kesi akitaka mahakama imuamuru katibu mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vilivyomvua madaraka na kuomba amri ya kuzuia vikao hivyo visimjadili.

Katika hukumu ya kesi hiyo, mahakama ilitupilia mbali hoja zake, uamuzi uliotafsiriwa kuwa umefungua njia ya kutimuliwa kwake kwa kitendo cha kufungua kesi mahakamani kinyume cha katiba.

Mkazi wa Gungu mjini Kigoma, Zuberi Mrisho alisema ujio za Zitto kugombea Ubunge wa jimbo hilo utaamsha ari ya wananchi kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kupiga kura tofauti na chaguzi zilizopita.

"Mwaka 2010 Vijana wengi hatukupiga kura hapa kwa sababu tulikosa imani na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini kwa ujio wa Zitto sasa nina hakika wengi tutajitokeza kupiga kura ili tupate viongozi makini kwa maslahi ya mji wetu,' alisema Mrisho.

Chanzo: Mwananchi

==========

My take;- Alisema majimbo ya Segerea, Ubungo na Ukonga wanamhitaji. Vipi kawasaliti hawa tena?
 
Kudos zitto yaaan pengo lako bungeni halizibiki tumeona hapa kwny bajet palipo pwaya lissu akikanyaga sheria na ww ukikanyaga uchumi na ufisaf mambo yanaenda
 
Hahahahahahh.....

Kamkimbia Mnyika Ubungo? Kamkimbia Mdee Kawe?

Mtamkimbia Mnyika mmoja baada ya mwingine, alianza Nape, kakimbilia Mtama. Sasa ni NURU YA CHAMA kakimbilia Kgm Mjini? Hapo juzi alikuwa na mbwembwe nyingi oooh, nagombewa na Wananchi wa Ubungo, Kawe, Kahama, Shinyanga.....nk Maweeeeeeee kakimbilia Kigoma Mjini baada ya kuvurunda jimbo lake la Awali..!!!

Poleni wanakigoma Mjini ila si Mbaya anakuja mgombea wa UKAWA hapo mpeni ushirikiano.

BACK TANGANYIKA
 
Inaonyesha unajua kuandika na kusomo tu yaan unataka alisema , ameombwa , kigoma mjini,segera kahama, ubungo,ukonga, sasa yeye amechagua kigoma mkoa wa nyumba kulingana na washauri wake , wew ulitaka ajigawe au
 
Inaonyesha unajua kuandika na kusomo tu yaan unataka alisema , ameombwa , kigoma mjini,segera kahama, ubungo,ukonga, sasa yeye amechagua kigoma mkoa wa nyumba kulingana na washauri wake , wew ulitaka ajigawe au
Hawa uwa wanachekesha sana kwao Zitto ana jema, angeenda kugombea Kahama wangesema kakimbia kwao mwingine anasema kamkimbia Mnyika Ubungo wakati Mnyika mwenyewe kurudi bungeni miujiza.
 
Last edited by a moderator:
Zzk akiacha tamaa ya fedha,madaraka,utoto na uchonganishi (ukiwemo uongo na uzushi) anaweza kuwa kiongozi mzuri hapo baadae.
 
Hivi zito si alisema anastaafu siasa anaenda kufundisha? Kwakweli wanasiasa sio wa kuamini wana ndimi nyingi.
 
Mkapa alishawahi kutoa maana ya mwanasiasa na Kiongozi.. Zitto ni aina wa wanasiasa wa Mkapa ambae anaamini katika uongo uongo ili kujijenga haya yanayotokea leo wadadasi humu ndani walipata kuyaandika na yeye kuyakanusha.
Leo naamini maneno yake "Tusiwaamini wanasiasa wenye kaliba yake".
 
Hivi zito si alisema anastaafu siasa anaenda kufundisha? Kwakweli wanasiasa sio wa kuamini wana ndimi nyingi.

Werema alimkaribisha kwenda kufundisha akakimbia..Werema sasa hivi anafundisha School of Law Tanzania.Jamaa mwongo sana huyu
 
Kudos zitto yaaan pengo lako bungeni halizibiki tumeona hapa kwny bajet palipo pwaya lissu akikanyaga sheria na ww ukikanyaga uchumi na ufisaf mambo yanaenda
Falsafa za Lissu na Msaliti Zitto ni mbali mbali.
 
Ingekua vema angeenda mkoa mwingine na kanda ingine ili kupigana vita vya kizalendo kwa vitendo halisi.
 
Mkuu ulitaka Zitto afanye nini ili akufurahishe weka maneno ya akiba kamanda.

Teh teh teh teh.....

Maneno ya akiba? Ninayo mengi mkuu mengi sana.. Na ndiomaana ninachokiandika hapa ni tofauti na nilichokiandika hapo mwanzo tulipokutana na wewe somewhere..!! Kama unabisha weka ushahidi hapa wa kufanana kwa naneno yangu na ya hapo mwanzo ambayo hata hivyo ulikosa majibu na kutokomea kusikojilikana..!!

Mkuu wangu Ritz, Chochote anachokifanya Zitto mimi ninakifurahia na ndiomaana unaona hapo mwanzo (ktk post uliyoninukuu) nimeanza kwa kucheka..!! Hivi ulitaka kuiona faraha gani nyingine toka kwangu zaidi ya hiyo?

Halafu Mkuu hukumsikia Zitto akisema Anagombewa na Wananchi wa Ubungo, Kawe, Shinyanga, Kahama na kwingineko?

Labda hasira zangu hapo ziko wapi mpaka unitake nifurahi kwa kile atakachokifanya Zitto?

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Zitto kaenda kupambana kwenye jimbo la CCM angeenda kugombea kwenye jimbo la upinzani tungesikia lawama nyingi tu Zitto anauwa upinzani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom