Zitto aanza vita ya wazi dhidi ya Rais Magufuli

Combative

Member
Apr 19, 2014
58
103
Sasa ni wazi kuwa Zitto kaanza rasmi kumshambulia Rais Magufuli, ukiangalia trend ya tweet zake za hivi karibuni ameaonekana kukosoa juhudi za Rais Magufuli tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma kidogo.

Mfano wa tweet zake na zingine ameaonekana kucopy kwa JK:

"@JrMalcolm88 @MariaSTsehai @Mkandara Rais ana historia ya kuingiza Taifa hasara. Mmesahau Meli ya Samaki? Mmesahau petrol station Mwanza?"

17m17 minutes ago
Zitto Kabwe Ruyagwa ‏@zittokabwe
@MariaSTsehai @jmkikwete Rais anasema watu ready handed wafungwe hapohapo? Hamjui nyie kuna watu hubambikiwa kesi mitaani? Tuwe makini sana

18m18 minutes ago
Zitto Kabwe Ruyagwa ‏@zittokabwe
@MariaSTsehai @jmkikwete Rais huyu analalamika wakwepa kodi hawafungwi ilhali yeye mwenyewe aliwapa muda kwenye makontena! Maria umesahau?

Sifa kubwa hasi ya mwanasiasa huyu ni ukigeugeu. Lakini pia duru za siasa zinasema amefanya kujaribu kulobby kwa Rais Magufuli ili japo chama chake kiweze kunufaika na uongozi wa awamu ya tano, imeonekana aliweza kufanya hivyo ktk uongozi uliopita na kwa kiasi fulani alifanikiwa. Sasa hivi anajaribu kuidhihaki serikali hii kwa sayansi yake ya kitoto ya saisa, ngoja tuone anakoelekea.
 

Attachments

  • upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    44 bytes · Views: 75
  • upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    73 bytes · Views: 40
  • upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    76 bytes · Views: 35
  • upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    upload_2016-2-6_18-24-11.gif
    75 bytes · Views: 34
Kwani kuhusu meli ni uongo? hiyo petrol station je? Mahakama za mafisadi huku unawaachia wafungwa waliosababishia serikali hasara ya mabilion? Hiyo mahakama anayoitaka bila kufuata sheria eti haina haja ya kupeleka bungeni? kweli hajasema uongo.
 
Ivi ile ya meli unaitaji kuwa judge kujua ilienda fyongo.
Ni sawa na mtu kakutwa na meno ya tembo alafu unaambiwa kashinda kesi.
Apo ni majudge na DPP sioni JPM akihusishwa apo.
Naitafuta ile rulling niipitie ili kujua why wale jamaa wa meli waliachiwa.
Iyo ya Mwanza siijui nkiipata ntaweza comment.
 
Zito yupo upinzani
Unategemea aache kukwamisha harakati za magufuli
Kwa faida ya maisha yake ya kisiasa lazma aendelee hivo
Hata uwaziri kivuli hajapewa
Kubenea nae?
 
Wanasiasa wa upinzani wanatafuta umaarufu kwa kutumia migongo ya watu maarufu ama kwa kujipendekeza au kukashifu juhudi wafanyazo. Hawabuni na kutoa agenda yao wenyewe.
 
Kwani kuhusu meli ni uongo? hiyo petrol station je? Mahakama za mafisadi huku unawaachia wafungwa waliosababishia serikali hasara ya mabilion? Hiyo mahakama anayoitaka bila kufuata sheria eti haina haja ya kupeleka bungeni? kweli hajasema uongo.

Ndugu kumbuka kipindi hicho kesi zinafikia hukumu yeye Magufuli anakuwa alishaondolewa ktk Wizara. Ukifuatilia kwa karibu kesi hizo ziliingia ktk sintofahamu ktk hukumu.

Ukiangalia vizuri nilichokiandika wala hupaswi kunitukana nimeelezea namna mwanasiasa huyu alivyo kitabia.
 
Ndugu kumbuka kipindi hicho kesi zinafikia hukumu yeye Magufuli anakuwa alishaondolewa ktk Wizara. Ukifuatilia kwa karibu kesi hizo ziliingia ktk sintofahamu ktk hukumu.

Ukiangalia vizuri nilichokiandika wala hupaswi kunitukana nimeelezea namna mwanasiasa huyu alivyo kitabia.
Umetukanwa wapi?
 
Serikali yake kupitia Magereza si imeandika barua Mahakamani kutaka adhabu ya Mramba na Yona viwe kifungo cha nje , Unawezaje kusema JPM anataka wahujumu uchumi wachukuliwe hatua kali wakati serikali yake inafanya kinyume?
 
Zito katoa maoni yake kwa jinsi alivyoona. Nami namuunga mkono kwa jinsi rais anavyoonekana kuwa juu ya katiba. Sijui labda kuna tatizo kwa washauri wake huenda. Kuna haja ya kuusema ukweli huenda anaburuzwa na washauri wake. Ukimsikiliza vyema unayaona makosa mengi ya kisheria na uvunjivu wa katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.
 
Back
Top Bottom