Nimekutana na hii katika mitaa ya Kigogo round about. nipo karibu na duka moja na foleni ya magari haiendi kabisa. kwenye foleni ikaja gari ya wazungu fulani ikiwa kwenye foleni ikasimama usawa na pale nilipokua nimekaa. Mzungu mmoja akashuka kumbe anaulizia vocha kwenye maduka ya maeneo yale. kama kawaida Opportunistic wakaanza kuchukua nafasi zao kila mtu anataka amsaidie. mmoja ambaye anayajua maduka ya pale vizuri akasema maeneo haya dula lenye vocha ni moja na tena wanauza vocha za kurusha yule mzungu akapelekwa pale. mgogoro ulianza pale jamaa walipoanza kuhangaika kutafasiri neno kwa neno kwamba zipo za kurusha kwa kiingereza itakuaje?. Ngoma ikawa kumuelewesha aina ya vocha zilizopo. kuanzia mwenye duka na genge la vijana ambao walioambatana nae wakawa wanajitahidi kumueleza aelewe alikini wakakwama. Mzungu hakui kiswahili kabisa na ameshindwa kujua wanamaanisha nini; basi mwingine akawa anaonyesha ishara ya mkono kama kutupa jiwe. Mwingine anasema ...we throw voucher...Mzungu akawa haelewewi na akawa katika kupaniki genge la waswahili waliomzunguka. Mwishowe foleni ikaanza kwenda kidogokidogo ikabidi akimbilie kwenye gari huku akiagnalia kule na kule kuonyesha jinsi alivyo desperate kupata vocha ila hakuna jinsi. basi wale wahuni wakabaki kucheka na kila mmoja akijaribu kutetea jisni alivyokua akimueleza basi ikawa ni kuchekana sana mahali pale. Hasara za kukimbia umande ndo kama hizo za Zipo za kurusha inakuwa ... throw