Kinachomkuta Gwajima ni kwa sababu amegusa Mamlaka ya nchi.
Kama Gwaji 2020 aliamua kuingia Siasa na akawa Mbunge mbona Mamlaka haikupiga kelele kwamba kwa mjibu wa sheria za kuanzisha Makundi ya kijamii haruhusiwi kujihusisha na siasa?
Hizo standing orders zimewekwa kwa ajili ya mtu anayeikosoa Serikali siyo anayeisifia Serikali.
Mashehena kila siku wanakaa vikao tena wakiwa na Shehena mkuu vya kusema Samia ni mtume na Yesu .Hiyo sio siasa lakini kupinga mauaji ya CCM na utekaji wa CCM unaofanywa na makundi ya kigaidi ni kufanya siasa .
CCM ikiwa na mlaveushwa na Tapeli Jerry Muro aliyekua anatumia ITV kutapeli wakurugenzi na mapolisi kwa picha uchwara za kuwaonyesha miradi na majumba yao eti atayatoa kwenye TV na magazeti ili wampe rushwa leo amegeuka kuwa msemaji wa Ikulu .
Jeri Muro mjinga kabisa akiwa ITV alikua anatengeneza skendo feki kwa watumishi wa Dawasa na kutaka Rushwa .
Alipowapiga picha askari polisi ndio ikawa gia ya kuishia Wakurugenzi wa Halmashauri . Alikua anapita na vitambulisho vya usalama wa Taifa na pingu .
Huyu Jeri Muro ni kati ya watu waovu walioteuliwa na Serikali ya awamu ya Tano .
Jeri Muro anapaswa atuambie alikua napata wapi pingu na vitambulisho Vya TAKUKURU na usala wa Taifa . Mjinga kabisa .
Jery Muro siku utawala wa Chama kingine ukiingia Madarakani kesi yake ya utapeli na kujifanya ni ,tunaishi wa umma ifufuliwe ili atuambie alipokua anapata vitambulisho vya usalama wa Taifa na TAKUKURU .
Kama alikua anatumwa atuambie alikua anatumwa na nani ?
Bila shaka Jery Muro bado ni kiongozi wa hayo Magenge yanayopita na pingu na bastola na kujifanya polisi na usalama wa Taifa .
Jeri Muro akamatwe mara moja ataisaidia Serikali kujua nani hua anadhamini au anaowatuma wahuni au watu ndani ya serikali au vijana maarufu kufanya misheni za kitapeli au za kificho wakiwa na pingu na vitambulisho lakini wakikamatwa wanaachiwa kama alivyoachiwa yeye bila kumfikisha mahakamani na kujua alipata wapi pingu na bastola na vitambulisho vya watumishi waliokua chini ya ofisi za serikali kuu.
Jeri Muro tapeli baadae akateuliwa na Rais kuwa mkuu wa Wilaya .
Hapa kwa nini tusiunganishe doti . Iweje mtu aliyefoji vitambulisho na kupita na pingu na bastola atishie mkurugenzi aombe mil 20 halafu DPP aondoe kesi yake bila serikali kutoa nafasi ya Wananchi kujua wapi alipata vitambulisho na pingu na bastola na nani alimpa hiyo kazi na hivyo vitambulisho na kwa nini alitumika yeye na isionekane ni kuichafua serikali badala yake baadae apewe ukuu wa Wilaya .
Leo Jeri Muro eti ni Mtu muhimu, mzalendo na mwenye nia njema na Rais kuliko Gwajima Mtumishi wa Mungu aliyehubiri wema wa Mungu ,ukuu wa Mungu , Toba kwa wanadamu na kuacha dhambi ikiwemo wizi wa mali za umma , mauaji,utekaji ,dhulma , uongo ,ufisadi , ushirikina ,utekaji na rushwa . Gwajima amewafanya mamiloni ya Watu duniani kuwa watu wema na watiifu katika haki kwa Mungu na wanadamu ,
Leo Jery Muro anayeshirikiana na Wauaji kujenga taifa la vijana machawa na wabinafsi kwa fedha za umma.