Zipo faida mme na mke kuwa kabila moja?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Kusema ukweli sasa, inakuwa ni vigumu kumpata mchumba umpendaye wa kabila lako; hasa baada ya watu wengi kuhamia mijini na kwenda walikozaliwa kwa matembezi tu (au kugombea ubunge); ni baada ya utandawazi.

Watoto tunaowazaa wanakuwa ni wa 'mjini' na kwa nadra wanaweza kuongea lugha za makabila yetu. Nachelea kusema, huenda baada ya miongo fulani, lugha zetu za asili zitakuwa zimetoweka katika uso wa dunia. Haidhuru basi, watoto wangeweza kuokoteza neno moja moja kutoka kwa lugha za wazazi wao, lakini na hilo haliwezekani kwa sababu wazazi wenyewe hawasikilizani kwa vile ni makabila tofauti.

Mbali na lugha, watoto wanashindwa kupata mila ya kufuata. Wanabaki kati kati, kwa baba hawapo na wala hawapo kwa mama.

Hakika, Mungu alikuwa na makusudi kumuumba kila mtu katika kabila lake au taifa lake (Mtikila, 1995). Pamoja na mazuri ya utandawazi wa kuoa au kuolewa katika makabila tofauti, binafsi, naona hasara ni nyingi kuliko faida.

WanaJF mnasemaje?
 
Kusema ukweli sasa, inakuwa ni vigumu kumpata mchumba umpendaye wa kabila lako; hasa baada ya watu wengi kuhamia mijini na kwenda walikozaliwa kwa matembezi tu (au kugombea ubunge); ni baada ya utandawazi.

Nikweli kuwa kuna hasara nyingi kuliko faida kwa hoja yako,lakini kwa dunia ya sasa inakuwa ngumu sana kama ulisema ulivyosema kwenye(red) kuondokana na tatizo hili.
 
Ukitaka watoto wafahamu mila wapelekeni vijijini from time to time!Kule ataokota neno moja leo..lingine kesho na mila atajifunza!

Tatizo siku hizi watu wanazaliwa mjini..wanakulia mjini hata kwenda kusalimia tu kijijini hawajawahi!Kwahiyo hata kwenye ndoa za mchanganyiko mila na desturi zinaweza kufunzwa sana iwapo watu wataacha kujifanya WAMJINI!!

Ukienda kijijini mara mbili tatu lazima utajifunza hata kusalimia na mila nazo hazitakupita!!

Nawakilisha!
 
Dawa ni kwenda kusaka hukphuko sitimbi km ww unataka kudumisha mila basi tembelea kileji chako then ibuka na mchuchu wako huko n visit yo homeland severally!
 
Ukitaka watoto wafahamu mila wapelekeni vijijini from time to time!Kule ataokota neno moja leo..lingine kesho na mila atajifunza!Tatizo siku hizi watu wanazaliwa mjini..wanakulia mjini hata kwenda kusalimia tu kijijini hawajawahi!Kwahiyo hata kwenye ndoa za mchanganyiko mila na desturi zinaweza kufunzwa sana iwapo watu wataacha kujifanya WAMJINI!!Ukienda kijijini mara mbili tatu lazima utajifunza hata kusalimia na mila nazo hazitakupita!!Nawakilisha!

Ahsante. Lakini, kuna faida kuoana kabila moja?
 
Ahsante. Lakini, kuna faida kuoana kabila moja?
Sioni tofauti yoyote..muwe kabila moja au tofauti nini kitakachobadilika zaidi ya kuongea lugha moja na kwenda likizo kwenye mkoa mmoja?Popote utakapopenda we penda achana na mambo ya ukabila!

Watu wanaotoka kwenye familia moja tu hawafanani ndo ije kuwa kabila!!
 
kiaina ndio

ila lazima mufanye vitu sawa makwenu...upande mmoja usilalamike

du bora kuoa mbali
 
Kwanza chagua nini unataka, mke au kabila kwasababu si rahisi kupata all in one. If institing of having same tribe na mila basi kaoe kijijini kwenu, however in all mi sioni faida kubwa sana zaidi ya kuanzisha unyanyasaji wa kabila, maana kuna wengine wanaona kabila lao ni bora kuliko lengine.

Ukiwa wewe na mzazi mwenzio mna msimamo nyumbani watoto wanaweza faidika na utamaduni na lugha za pande zote as mentioned above from time to time wapelekeni vijijini kama likizo au zungumzeni kikabila ndani kweni.
 
Mi ni nyakyusa, niliwauliza dada zangu 6 nyakat tofauti kama wangependa kuolewa na wanyakyusa.

Wote walisema hawatak kuolewa na wanaume wa kabila lao, labda itokee tu wameshikwa na MAPENZI MOTOMOTO lakin ktk hali ya kawaida watakwepa ku-date na wanyakyusa.
 
mmmhhhh jamani kwenye ndoa kama kuna Lugha ya upendo na lugha ya kiswahili sioni tatizo.....
 
msambaa ukiwa mwanaume ukaoa mke wa kabila jengine unatengwa na familia,ila mwanamke anaruhusiwa kuolewa na kabila jengine,sijaielewa hii kwa kweli.
 
Sioni tofauti yoyote..muwe kabila moja au tofauti nini kitakachobadilika zaidi ya kuongea lugha moja na kwenda likizo kwenye mkoa mmoja?Popote utakapopenda we penda achana na mambo ya ukabila!Watu wanaotoka kwenye familia moja tu hawafanani ndo ije kuwa kabila!!

Ahsante kwa kutaja faida mbili.

1. Kuongea lugha moja ni faida kwani mnaweza kuyaongea mambo yenu ya siri bila majirani kujua undani wake.
2. Kwenda mkoa mmoja ni faida kiuchumi. Mmoja akienda likizo anazitembelea familia za pande mbili.
 
Mi ni nyakyusa, niliwauliza dada zangu 6 nyakat tofauti kama wangependa kuolewa na wanyakyusa.

Wote walisema hawatak kuolewa na wanaume wa kabila lao, labda itokee tu wameshikwa na MAPENZI MOTOMOTO lakin ktk hali ya kawaida watakwepa ku-date na wanyakyusa.

TRUEEEEE iyo nimeiona ata kwa rafiki zangu akina ntumpe,sekela hawataki kabsa kuwaskia akina MWAKANJONO ,MWAKASUNGURA...et wana majigamboooooooooo.....wana mafagioooooooooooo na dharau teele kama wale waliotoka kule nyonyoni(ziwani)... hasa ukimpata aliyeenda majuu kdg kusoma diploma ya funza na sisimiz daaa utamkoma km anaitwa lusekelo atajiita LUSEE!!!( WAO WALISEMA MI SJASEMA)
kuolewa na wakabila moja if umempata wa kukupenda na wakukupenda kutoka kabila lenu bas poooa inanoga cz mtakuwa mnaonge akinyumbani tu ..wambea wanabak macho kodo kodo tu...mkienda likizo mwaenda wote na mambo mengne pia mtakuwa mnaonmge alugha moja(mnaelewana)miiko,na desturi zote
 
Ahsante kwa kutaja faida mbili.

1. Kuongea lugha moja ni faida kwani mnaweza kuyaongea mambo yenu ya siri bila majirani kujua undani wake.
2. Kwenda mkoa mmoja ni faida kiuchumi. Mmoja akienda likizo anazitembelea familia za pande mbili.
Kama mnataka kuongea kitu cha siri si muende faragha!Kwanza sio ustaarabu kuongea lugha wenzako wasioijua mkiwa mmejumuika pamoja!Itaneni pembeni myamalize!Hiyo nyingine nakubaliana nayo...japo haitoshi kutangaza ndoa!
 
Ahsante. Lakini, kuna faida kuoana kabila moja?

Faida ipo kwenye gharama ya usafiri fikiria wewe mzaliwa wa Lindi upo kikazi Songea umepata mchumba wa Bukoba siku za sikukuu inatakiwa mwende kuwatembelea wazazi hapo ndugu yangu nauli ya Lindi- Bukoba kwenda na kurudi na mazaga zaga kwa wakwe ni maumivu
 
kuolewa na wakabila moja if umempata wa kukupenda na wakukupenda kutoka kabila lenu bas poooa inanoga cz mtakuwa mnaonge akinyumbani tu ..wambea wanabak macho kodo kodo tu...mkienda likizo mwaenda wote na mambo mengne pia mtakuwa mnaonmge alugha moja(mnaelewana)miiko,na desturi zote

Dada Rose nimeipenda.
 
Faida ipo kwenye gharama ya usafiri fikiria wewe mzaliwa wa Lindi upo kikazi Songea umepata mchumba wa Bukoba siku za sikukuu inatakiwa mwende kuwatembelea wazazi hapo ndugu yangu nauli ya Lindi- Bukoba kwenda na kurudi na mazaga zaga kwa wakwe ni maumivu

Nakubaliana nawe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom