Zipi ni Spark Plug sahihi kwa gari lako?

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
images (42).jpeg


Zipo spark plug za aina nyingi sana. Yapo mambo mengi sana yanayoweza kutofautisha spark plug za gari na gari jingine.

Mambo hayo ni

1.Material yaliyotengeneza hizo plug (iridium copper n.k)

2. Urefu wa thread (nyingine zinakuwa na thread ndefu nyingine fupi)

3. Gap (nyingi zina gap la 1.1mm lakini linaweza kuongezeka au kupungua na hawashauri kuliadjust)

4. Idadi ya pini ( pin1, pin 2, pin 3 n.k.

5. Material ya tip (platnum tipped, nickel tipped n.k.)

6. Ncha ya tip (Nyingine ni sindano na nyingine zipo kawaida)

Kwa kifupi hakuna plug ambayo ni best kwa kila gari. Ndio maana, kila engine ina plug zake ambazo ni OEM ameshauri zifungwe.

Kwa baadhi ya engine ukifunga plug ambazo si sahihi matokeo yake inakuwa ni sawa tu na gari ambayo plug zake zimechoka.

Plug zilizochoka zinaweza kuwa na dalili hizi.

1. Kutetemeka engine

2. Gari kuwaka kwa shida.

3. Gari kuzima yenyewe muda mwingine.

4. Matumizi makubwa ya mafuta.

5. Gari kuchelewa kuchanganya. (Poor acceleration).

6. Pia taa ya check engine inaweza kuwaka na kutrigger code namba p0171 system is too lean. Japo hii code inaweza kuletwa na mambo mengi.

Gari yako ina engine gani? Comment model code ya gari lako nikuambie plug sahihi za kufunga.

*******######**********

1. Pia kama unahitaji Diagnosis na marekebisho kwa gari lako karibu Magomeni Mwembechai Dar.

SIMU: 0621 221 606

WHATSAPP: +255 621 221 606

images (41).jpeg
 
Back
Top Bottom