Zingatio kwa wafanyabiashara ya Uber, bajaji na bodaboda

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,601
4,086
Wakuu,

Miongoni mwa biashara zinazozingua na kuwapa presha ya kupanda pamoja na vidonda vya tumbo wamiliki ni biashara ya vyombo vya usafiri (Uber, Bajaj & Bodaboda).

Hii ni kutokana na madereva wengi wanaokabidhiwa hivi vyombo kuwa na fikra za hovyo zinazopelekea tabia za hovyo:

- Hawa hufikiri kuwa mmiliki wa chombo ana hela nyingi na ameridhika. Hivyo ile hesabu ya chombo ni ya ziada au ya kujifurahisha tu.

- Pia huhisi kama si halali kumpa mmiliki pesa yake ya hesabu kama walivyokubaliana.

Yaani wanahisi kama vile wanampa hela ya bure akiwa amekaa tu bila kufanya kazi yoyote.

(Wanasahau kuwa huyu mtu alitoa Milioni zake kadhaa kununua hicho chombo, na pengine ni za mkopo unaomtesa kuurejesha).

- Wakishazoeleka na kupata connection ya wateja wengi, (baadhi yao) huingiwa na kiburi na kuona kuwa wanaweza kupata pesa kirahisi tu na hivyo nafasi ya mmiliki mwenye kile chombo haina tija.

- Wanasahau kuwa walikuja kwa upole, mikono nyuma, kuomba kibarua cha kukabidhiwa chombo waendeshe na kutoa ahadi ya kutekeleza makubaliano yote bila purukushani zozote.

Kwa fikra na tabia hizo hapo juu,

- Hawapeleki hela kwa mmiliki kama walivyokubaliana

- Hawakitunzi chombo, wanakitumia bila uangalifu wowote.

- Wanaweza kuingia makubaliano na vibaka na kujifanya wameporwa chombo kwa kugawana nao asilimia kadhaa.

Hivyo, watu hawa hupelekea taharuki, majuto na vilio vingi sana kwa wamiliki wengi wa vyombo vya usafiri (hasa wale wenye mitaji midogo)

Zingatio:
Najua humu kuna watu ambao wanafanya biashara, wengine wana mikakati ya kuifanya, wengine wamefanikiwa na wengine ni waathirika wa biashara hii na hawataki hata kuisikia
(Mimi sipo kwenye kundi lolote miongoni mwa hayo).

Kwa wale wanaotaka kuielekew hii biashara zingatia haya machache:

1) Usimkabidhi mtu chombo kwa makubaliano ya kienyeji, pasipo na maandishi ya kisheria.

Mkabidhi kwa mkataba maalum,
Tena mkataba uandikwe, kushuhudiwa na kusainiwa na mwanasheria,

Una uwe na vipengele vya kuwa favour nyote bila kumuumiza yeyote,
Na vipengele vya kum'bana yeyote atayekiuka makubaliano.

Tena ikiwezekana uprintiwe kwenye legal paper.

Usione shida kumpa mwanasheia 20,000/= ikiwa chombo chako ni cha Milioni kadhaa.

(Hii sio kinga ya 100%, ila inaweza kuwa defense kwa kiasi kikubwa).

2. Mpe chombo mtu mzima mwenye familia yake, ambaye atakitumia kama sehemu yake ya kazi ili kuikimu familia yake.
Ila hakikisha anakuwa na mdhamini anayeaminika.

Usimpe chombo msela tu ambaye popote kambi na hana cha kupoteza,

Hawa hawashindwi kufanya mambo ya hovyo muda wowote.

3. USIMPE CHOMBO MTU ANAYENYOA KIDUKU NA KUVUTA BANGI-
UTALIA KILIO CHA FISI MWENYE BUSHA.

Nimeandika kwa herufi kubwa hapo ili twende sawa wakuu.

Mengine watamalizia wadau.

Hii Nchi ni Yetu Sote na Maendeleo Hayana Chama.
 
Seneta Wa Mtwiz, Professional advice... mimi sina cha kuongezea maana umepita mulemule anayetaka kufanya hii biashara akifuata hizi nondo atapunguza risk kwa % kubwa sana japo risk ni usually kwenye biashara ila kwa thread hii itasaidia sana
 
Mm nataka niingie nifanye mwenyewe kwa kugawana muda na mwajiri wangu (kazi nyingne).

Una lipi la kunishauri?
 
Back
Top Bottom