ZINGATIA-Mnaoweka matangazo ya kazi humu

Papaa kama upo siliazi na kutafuta kazi basi inabidi ushukuru kwa kupewa link ni jukumu lako mwenyewe kutafuta, lipa hata buku uingie internet cafeee. Kwani unalaumu kwa uyo anaekusaidia kukupa linki wewe unamlipa nini na hata akujui kwanza then anakusaidia wewe unamlaumu.

Inaonekana hata ukipewa maswali ya mtihani wa kesho wewe utamlaumu aliekupa mbona ajakupa na majibu, tuweni waungwana wana jf
 
internet cafe bila hela wala kazi ndugu zangu! Si mtu unajikuta unatumia zaidi ya 5000 wkt kwenye simu ni bure, kumbuka watu wengi tunaosoma matangazo haya hatuna kazi wala kianzi. Tunaumizana wakuu mtoa mada yuko sahihi.
 
Habari Wana Jamii Forum,

Sisi ni ZoomTanzania.com. Kwa kupitia maoni yenu, tumeelewa kwa nini baadhi yenu mnaona ni kero na usumbufu kulazimika kubofya link ili kupata maelezo juu ya kazi. Tunaomba ushauri wenu tufanye nini juu ya jambo hili.

Siku zote tunajitahidi sana kuwaletea mkusanyiko mkubwa wa nafasi za kazi Tanzania nzima. Mara nyingi huwa tunawaletea kati ya nafasi mpya za kazi 25 mpaka 40.

Waajiri wengi wanapost kazi kwenye Website yetu kwa sababu kuu mbili:
  1. Tuna utaratibu mzuri wa kutunza Email Addresses zao. Jambo ambalo huzuia wasipate Spam kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
  2. Wanayo nafasi ya kupost maelezo kuhusu nafasi ya kazi kwa ku-upload MS Word au PDF.
Kinachotutatiza sisi ni kuwa kama tukiweka maelezo ya kazi, kwa kazi zote (25 – 40), post itakuwa ni ndefu sana na ngumu kusoma. Na inawezekana Wana Jamii Forums wengi wasifurahie ku-‘scroll’ sana ili kutafuta nafasi ya kazi inayoendana na taaluma yao.

Kinachotutatiza zaidi ni, kwa zile kazi ambazo Maelezo yake ya kazi yako kwenye MS Word au PDF, tuki-upload Maelezo hayo, itakuwa bado ni ngumu kwa wale wenye simu ndogo kudownload na kusoma.

Tunapenda sana kuendelea kutumia JamiiForums ili kuwataarifu juu ya nafasi mpya za kazi. Kwa sisi tunaopost kazi nyingi, tunaona utaratibu wa links, unasaidia Wana Jamii waone kazi za taaluma zao kwa Haraka na urahisi zaidi.

Tunaomba mtusaidie ili tuweze kuendelea kuwasaidia. Je ni bora tupost kazi mbili au tatu tu, na Maelezo Kamilifu na tuwaambie idadi tu ya kazi nyingine mpya? Au tuchague kazi moja tu ambayo tunaona ni moto moto zaidi, tuweke maelezo kamili na kisha tuweke links ya hizo kazi nyingine?

Tunakaribisha maoni yenu!
 
Habari Wana Jamii Forum,

Sisi ni ZoomTanzania.com. Kwa kupitia maoni yenu, tumeelewa kwa nini baadhi yenu mnaona ni kero na usumbufu kulazimika kubofya link ili kupata maelezo juu ya kazi. Tunaomba ushauri wenu tufanye nini juu ya jambo hili.

Siku zote tunajitahidi sana kuwaletea mkusanyiko mkubwa wa nafasi za kazi Tanzania nzima. Mara nyingi huwa tunawaletea kati ya nafasi mpya za kazi 25 mpaka 40.

Waajiri wengi wanapost kazi kwenye Website yetu kwa sababu kuu mbili:
  1. Tuna utaratibu mzuri wa kutunza Email Addresses zao. Jambo ambalo huzuia wasipate Spam kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
  2. Wanayo nafasi ya kupost maelezo kuhusu nafasi ya kazi kwa ku-upload MS Word au PDF.
Kinachotutatiza sisi ni kuwa kama tukiweka maelezo ya kazi, kwa kazi zote (25 – 40), post itakuwa ni ndefu sana na ngumu kusoma. Na inawezekana Wana Jamii Forums wengi wasifurahie ku-‘scroll' sana ili kutafuta nafasi ya kazi inayoendana na taaluma yao.

Kinachotutatiza zaidi ni, kwa zile kazi ambazo Maelezo yake ya kazi yako kwenye MS Word au PDF, tuki-upload Maelezo hayo, itakuwa bado ni ngumu kwa wale wenye simu ndogo kudownload na kusoma.

Tunapenda sana kuendelea kutumia JamiiForums ili kuwataarifu juu ya nafasi mpya za kazi. Kwa sisi tunaopost kazi nyingi, tunaona utaratibu wa links, unasaidia Wana Jamii waone kazi za taaluma zao kwa Haraka na urahisi zaidi.

Tunaomba mtusaidie ili tuweze kuendelea kuwasaidia. Je ni bora tupost kazi mbili au tatu tu, na Maelezo Kamilifu na tuwaambie idadi tu ya kazi nyingine mpya? Au tuchague kazi moja tu ambayo tunaona ni moto moto zaidi, tuweke maelezo kamili na kisha tuweke links ya hizo kazi nyingine?

Tunakaribisha maoni yenu!

Mkuu, Kuh Zoomtz nyie mnafanya kazi katika kiwango cha hali ya juu sana, kwanza mnaweka list ya kazi zote ktk ukurasa wa jf kisha link ya kila kazi, hii ina saidia mtu kujua kwa kuona mwenyewe kabla ya kuwa interested kufungua link, Pili Zootz ni website ya kisasa ambayo page yake sio nzito kiasi cha kufanya ishindwe kufunguka katika simu, tatu ktk link unaweza kuapload cv yako hata kwa kutumia mobile phone hivyo mpo juu sana.

Hawa Wenye Blogs ni kweli wanatusaidia sana lakini size za blogs ktk front pages ziko undefine hivyo kuipata kazi na ukaisoma vizuri ni taabu sana. Kwanza Page Inakuwa Kubwa Sana kufunguka, inatakiwa uscroll right left up down tena speed yake ni ndogo sana hivyo wenye cm za kichina huwezi kuona kitu tena bahati mbaya hakuna list ya kazi zenyewe ktk jf page hivyo tunazipotezea tu.

Jamani ni kweli hizi ni kazi za kujitolea lakini naamini Mungu atawalipa zaidi kama mtatafuta namna mzuri ya kuwakilisha hizi nafasi ili kuwafikia watu wengi zaidi maana wengine wapo mbali hivyo hawana access ya Pc Internet hivyo endeleeni kutusaidia ktk kiwango bora zaidi maana kazi yenu tunaikubali, tunaihitaji na tunaitegemea sana
 
ina maana hairuhusiwi mtu kuweka link?..mh akili masaburi hii
Acheni mambo ya ajabu,si mmeelekezwa na aliyetoa thread hii kuwa toa ufafanuzi ndipo uweke link.

Kama wewe ni mchovu wa kusoma walichoandika wenzako haina haja ya kuweka comment zako ambavyo si lazima sana.

jitahidini kusoma kwa kuelewa na sio kubisha na muwe tayari kusaidia na wengine ambao hawana access na computer kwani jf members sio wote wako mjini na wengi wanatumia simu ndogo tu.
 
maneno mengi watz huwa ni wavivu kusoma andika brief halafu link ili mwenye nia zaidi aingie..
 
kwa shida niliyonayo na ajira hata wasipo weka link nikiona tangazo tu ntagoogle ili nipate more info.
 
Ama kweli wabongo ni wazembe wa kutisha, Umepewa link bado unalalamika, simu gani inaweza kufungua internet then ishinwe kufungua hata link? Hebu jaribuni kuwa na shukrani walau kidogo tu.
 
Zoom nawakubali sana sana ila kuna fununu kuwa na typing error mchapaji awe makini zaidi pili ni ombi naomba wekeni e-mail addrs za kazi mnazoweka tafadhal mbna wao wanaweka kwenye magazeti?tafadhalin sana sio wote tunauwezo wakupata gazeti au hela zakupost barua so km zoom hamtajali tuwekeeni email adres za wanaotuma matangazo ya kazi
 
acheni ubahili kwanini tunataka kuwekeza bila gharama!?ingia net
 
Unapenda kutafuniwa kila kitu mchujo unaanzia hapo ukiona ugumu wa kuipata link ujue umeisha toka kwenye kinyang'anyiro acha wenye nguvu wapite.
 
S...type wewe unaona sisi tunaohangaika kuweka tunawawekea wenye simu??kweli wewe umekosa busara kama ng'ombe hata umpandishe ndege atakunya humo!!Mimi kuanzia leo siweki tena naweka hii ndo yamwisho tazama naweka link ya kazi za UN kama una tumia simu utajiju kama unataka kazi nenda cafe.
 
Wabongo kweli hamna shukrani khaaaa!!!
Thank you sana @ Baba Mkali.........haah huyu jamaa analalamika kupewa info za kazi duh! Yaani hataki hata ku-appreciate kwamba mtu kafanya iniatiative na muda wake kupost a job advert humu ndani....... I hate this

Plz tuwe na shukrani na kuwatia moyo wanaotupa hizi job adverts kwa sababu kuna wengi wanaona kwingineko na wala they never take a step kushare na sisi humu ndani.
 
Where necessary weka full info na link, ni haki na ni upendo na hekima ya great thinker kutambua tatizo na kulitambua, sio wote wenye uwezo wa kwenda cafe. Kwa hiyo kama inawezekana weka habari kamili ndugu zanguni.
 
Inakera unakuta tangazo la kazi, unafungua unakutana na link, hebu jiulize wewe unaeweka link mtu mwenye simu ndogo ataweza kuifungua kweli wakati mi-blogs yenu inatafuna mi-kb! Au mnataka tujue mnamiliki blogs!

Fanyeni copy & paste (MFANO MAX MELO) then kwa kutia naskshi unasema "for more info" then unatupia link.

Badilikeni jamani.......mjini shule!

Man! you have to change your thinking attitude. Dunia haiendi hivyo unavyofikiria. Unataka kua bosi hata katika vitu usivyo vimiliki. HIYO NDIO TABIA INAYO ITWA MASIKINI JEURI. UTABAKI MASIKINI NA UJEURI YAKO MILELE.
 
Dry,
nadhani hapa hauna elimu kidogo ya website."@Dry hakuna website yeyote duniani wakati wa ku browse isile bytes or any size.na hii inategemea sana Uzito wa website na pia wewe watumia ISP yupi kwenye simu yako?Then handset yake(device-simu yako).sasa kama wewe watumia Nokia tochi au hizo zingine huwezi kufungua hizo links."
Cha msingi nunua laptop,or pda device's eg.ipad 2,blackberry,samsung galux.

Usilaumu laumu tuu..use technology na akili pia ..kutafuta kazi ni gharama.
 
Hebu fikiria hata hiyo link umeipata ...kunasehemu tuliko sisi wananch hawana elimu ya Technohama,Mitandao yenyewe shida kushika...ikinyesha mvua mitandao inakuwa ishu sometimes,magazeti yanasomwa ya siku moja nyuma,fikiria huyo atajuaje kunakazi sehemu na kama wenye blog yao hawa wanatusaidia kuweka hizi link ili tutafute na ikiwa bahati yako upate.@dry wewe uko Dar waweza nunua gazeti tuliko sisi unasoma gazeti siko moja au 2 nyuma.

Ulichotakiwa ni kuwaomba wana blog wawe wanaweka full information ili ikupunguzie gharama ya ku visite link nyingi na kupunguza mahesabu ya vocha za mawazo.

By the way maisha yamebadilika no anything came straight and to get a job now it's like Mungu amekushushia neema..Najua uko affected kidogo na hali ya maisha haya ya job hunt.so be cool and waombe wadau na watakusikiliza lakini sio kutumia kauli mbaya kama hizo na kusema inakera.kama huwezi nunua magazeti yote ili uzione hizo full info za job advert..Kila la kheri bwana Dry.

very :A S embarassed:

Inakera unakuta tangazo la kazi, unafungua unakutana na link, hebu jiulize wewe unaeweka link mtu mwenye simu ndogo ataweza kuifungua kweli wakati mi-blogs yenu inatafuna mi-kb! Au mnataka tujue mnamiliki blogs!

Fanyeni copy & paste (MFANO MAX MELO) then kwa kutia naskshi unasema "for more info" then unatupia link.

Badilikeni jamani.......mjini shule!
 
@likwamba,
mimi nijuavyo maisha ya technohama no free na pia you supposed to pay each service unayo access kwa wakati huo.kama ameweza sign in kwenye blog,facebook,yahoo na myspace huyo anaweza mudu gharama za kucheki hizo link hata mia moja.

Mimi naomba muendelee na mnavyofanya na sio mtu mmoja anataka kufanya chombo kama chake.kama hawezi kubrowse basi aende cafe kwa maana gharama zinautofauti wa sh 100 au 50 tuu.so Mtafuta hachoki na akichoka ujue huyo hakuwa ametafuta au ameshapata.
*Technology is very expensive that people think.....kama atataka simu iweze kuwa na color nzuri na web browser lazima iweze meet technical specification means itamlazimu anunue simu zenye viwango au la awe mtu wa cafe.

Nawapa sana big up wenye blog hii kwa ku post hizi nafasi.kwa mimi nashukurubmaana nikiona simu haiwezi fungua link basi nitatoa 1000(ya dubai) ili nikacheki cafe au kumwomba wenye pc acheki na hapo ndo utakapojua unamarafiki wa namna gani.

See ya
 
Back
Top Bottom