Zingatia haya kwenye safari yako

Zingatia haya kwenye safari yako

Marmeid

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2024
Posts
523
Reaction score
1,204
Maisha ya kijana ni safari ya kujitafuta.
Ni kipindi cha ndoto, nguvu, hamu, makosa, maumivu na maamuzi makubwa.

Wengi huingia hatua hii wakiwa na matarajio makubwa—lakini hukutana na uhalisia mgumu kuachwa, kukataliwa, kukosa ajira, kukosa fedha, presha za marafiki na tamaa za mwili.
Ndipo neno acceptance (kukubali uhalisia) linapokuwa muhimu sana.

NB:
Acceptance siyo udhaifu.
Acceptance ni hekima.

1. ACCEPTANCE BAADA YA KUUMIZWA AU KUACHWA

Kama umeachwa au umeumizwa, ukweli wa kwanza ni huu: maumivu ni halali. Usijilazimishe kuwa na furaha bandia. Usikimbilie kujaza pengo kwa mtu mwingine.

Kwa nini acceptance ni muhimu baada ya kuachwa?
Inazuia chuki kukaa moyoni, inazuia kulipiza kisasi kwa kuingia kwenye mahusiano ya pupa.

Inakuwezesha kujifunza badala ya kuumia milele kijana wengi wakiumizwa hukimbilia

.Ngono za kulipiza.
.Mahusiano mengi ili kuthibitisha thamani.
.Pombe au starehe kupitiliza.

Lakini ukweli ni huu:

Unapokimbia maumivu, unayapa nguvu zaidi.
Acceptance inamaanisha,
Nimeumia, lakini sitaruhusu maumivu ya leo yaharibu kesho yangu.”
Unajipa muda wa kupona.
Unatafakari ulipojifunza.
Unaendelea mbele bila kujichukia.

2. ACCEPTANCE KWENYE MAISHA MAGUMU

Maisha siyo laini kila wakati. Kuna wakati huna pesa
Wenzako wanafanikiwa zaidi, familia inakutegemea ndoto zinaonekana mbali acceptance hapa haimaanishi kukaa chini inamaanisha kukubali ukweli wa sasa ili uweze kupanga kesho vizuri.

Ukikataa hali yako utajilinganisha utapata presha utafanya maamuzi ya haraka lakini ukikubali hali yako unaweka mikakati unasonga hatua kwa hatua unajenga kwa utulivu maisha magumu siyo laana Mara nyingi ni darasa.

3. NGONO ZEMBE HATARI KWA AFYA NA NDOTO

Katika kipindi cha maumivu au msongo, ngono zembe huwa jaribu kubwa.
Lakini kijana mwenye maono lazima awe na nidhamu.

1️⃣ Hatari za kiafya

Dunia imejaa magonjwa ya zinaa kama:
.HIV/AIDS
.Gonorrhea
.Syphilis

.Human Papillomavirus.

Baadhi ya magonjwa haya hayana dalili mapema yanadumu maisha yote.
Yanaweza kuharibu afya, ndoa na ndoto.
Dakika chache za tamaa zinaweza kubeba mzigo wa maisha yote.

2️⃣ Hatari kwa ndoto
Ngono zembe inaweza kusababisha

.Mimba zisizotarajiwa.
.Migogoro ya kihisia.
.Kuvurugika kwa masomo au kazi.

.Kumpoteza focus.

Kijana asiyejijenga akifungwa na majukumu ya ghafla, ndoto nyingi hufifia kabla hazijachanua.

Swali la kujiuliza

(Hii raha ya muda mfupi ina thamani kuliko mustakabali wangu?)

4. MOVE ONE STEP AT A TIME

Kosa kubwa la vijana wengi ni kutaka kila kitu kwa wakati mmoja mafanikio haraka mapenzi makubwa haraka pesa nyingi haraka lakini maisha yanajengwa kwa hatua.

Hatua ya kwanza: Jitambue
Jua wewe ni nani, una maadili gani, una maono gani.

Hatua ya pili: Jidhibiti
Uwe na mipaka. Siyo kila mwaliko unakubali.
Siyo kila mtu ana nafasi kwenye maisha yako.

Hatua ya tatu: Jenga msingi
Elimu au ujuzi.
Nidhamu ya kifedha.
Afya ya mwili na akili.

Hatua ya nne: Subira
Mti hauoti leo ukavuna kesho.
Ndoto zinahitaji muda.

5. NGUVU YA KUJIZUIA

Kujizuia siyo kupoteza ujana.
Ni kuwekeza ujana kijana anayeweza kusema
Nitaweka mipaka mpaka niwe tayari,” anaonyesha ukomavu mkubwa kuliko anayefanya kila kitu kwa sababu “wote wanafanya”.
Tamaa ni ya muda heshima ya maisha ni ya kudumu.

6. KUWA NA AMANI NDANI YAKO

Acceptance inakupa amani unajua hujakamilika, lakini uko safarini.
Umeumizwa, lakini hujavunjika maisha ni magumu, lakini hujakata tamaa.

Kijana mwenye acceptance hafanyi maamuzi kwa hasira hafanyi maamuzi kwa presha hafanyi maamuzi kwa tamaa anafanya maamuzi kwa maono.

HITIMISHO

Kijana, unaweza kuumizwa lakini usijiharibu.
Unaweza kuachwa lakini usipoteze mwelekeo.
Unaweza kukosa leo lakini usiache kuota.
Epuka ngono zembe. Linda afya yako. Linda afya yako ya akili
 
Subscribed
 
Hivi ni mimi tu au mpaka wengine...
Kama kijana mpambanaji na unaona mambo yanenda dilemma hiyo hamu ya ngono unatolea wapi..

Ngoja niwape sili vijana wenzangu
Utajiri na nguvu za kiume ni vitu viwili tofauti na havikai pamoja...
Hilo jambo ukifatilia utaona matajiri wengi hawana nguvu za kiume.
Tafuta tajiri yoyote hapa nchini kama ana nguvu za kiume njoo hapa niambie ,""

Hivo ndugu zangu katika mada za kijana kujitafuta toeni mambo ya ngono...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom