Zinduna Talk Show: Leo mjengoni nipo na Aunt Lizzy~~~~!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Samahani wasomaji wa JF, jana kipindi hakikuruka hewani kwa sababu ya kupisha mkutano wa Jangwani.
Leo mjengoni nipo na Aunt Lizzy, ambaye kwa kweli amenipa ushirikiano wa hali ya juu. Yeye hakujivuta vuta saana kukubali mwaliko wangu kama Mzee wa Mapouzi Bishanga. Mahojiano yangu na Aunt Lizzy yatasawiri zaidi kwenye maisha yake binafsi na kazi zake za mapema.

Line za ku-post Comments ziko wazi, Mwana JF yeyote anaweza kutumia fursa hii kumuuliza Aunt Lizzy swali lolote na yeye bila shaka atayajibu maswali yenu kwa kadiri atakavyopata muda.

Kwa kuanza ninayo maswali kumi ambayo ningependa kumuuliza Aunt Lizzy:

1. Je umezaliwa msimu gani?
2. Je Ulishawahi kucheza mchezo wa baba na mama na kupika pika utotoni?
3. Je umeolewa? Kama umeolewa, Je una watoto wangapi, na kama hujaolewa, ina maana huna hata wa kuchombeza?
4. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
5. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana
6. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
7. Je unapenda chakula cha aina gani?
8. Ukipata fursa ya kupata staftahi na mheshimiwa Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa Chadema jimbo la Arusha, utamshauri nini?
9. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
10. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show…….

Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Aunt Lizzy atakuja kuyajibu maswali yenu.

Karibuni sana
 
1.je ulishawai kutokewa na mume wa mtu na kama ndio ulikipingaje iko kishawishi???
2.ulishawahi kufaminia ama kufumaniwa??
3.unapenda mwanaume mwenye sifa gani??
4.je ukiwa kama mwanamke unawashauri nini wanawake wenzako kuhusu kujituma na kuachana na mawazo ya kuwezeshwa ama kutegemea wanaume ili watoke ktk maisha???
 
Ahsante CUTE kwa maswali yako mazuri.
Samahani, huenda maswali yenu yasijibiwe haraka kwa sababu Aunt Lizzy ndio amefika na sasa anajipodoa kwa mapouda nyuma ya pazia kabla hajauza sura hapa mjengoni ....
Labda niwafahamishe tu kwamba nimelazimika kusafiri hadi Arusha UNGA LIMITED kwa ajili ya kufanikisha mahojiano haya ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu na wadau hapa JF...........
Pia ningependa kuwaomba radhi wapenzi wa kipindi hiki cha Zinduna Talk Show kwamba niliahidi kuwa na Mwana JF machahari Kipipi , lakini kwa bahati mbaya aliomba udhuru na kwa sababu amesafiri kikazi kwenda visiwa vya Mayotte na hivyo nikaona ni vyema nifanya mahojiano na Aunt Lizzy wiki hii~~~

Wiki ijayo nitakuwa na Bwana Mkubwa Erickb52 ~~~~Stay tune
 
Last edited by a moderator:
1. Ulishawahi fanya masterbation?
2. Kama ni amri yako, ungetoka na mkaka gani wa JF (ur secret admire)?
3. Can you give up ur carier n be a house wife for any reason
 
1. Ulishawahi fanya masterbation?
2. Kama ni amri yako, ungetoka na mkaka gani wa JF (ur secret admire)?
3. Can you give up ur carier n be a house wife for any reason
Kaunga napenda kuutambua uwepo wapo katika kipindi hiki siku ya leo
Ahsante sana kwa maswali yako mazuri na yenye mashiko, vuta subira Aunt Lizzy atakuja hivi punde kujibu maswali yenu
 
Last edited by a moderator:
Maskini, my wi Lizzy hajaonekana jamvini kwa muda sasa, sijui yuko wapi.

Ikifika saa 15:00 hajaja naanza kumjibia maana mie na wifi yangu hatufichani.
 
Last edited by a moderator:
Bi Zinduna asante sana kwa kunikaribisha kwenye kipindi, na naomba radhi sana kwa kuchelewa maana kipindi kilianza bila mie kuwa nimewasili. Sasa maana muda umeenda naomba nijibu maswali yako haraka haraka kama watazamaji hawajahamia TiBiSii.

Koh koh. . .
Kwa kuanza ninayo maswali kumi ambayo ningependa kumuuliza Aunt Lizzy:

1. Je umezaliwa msimu gani?
. . . . HEHEHE. . msimu nlozaliwa mie kiangazi, ndo maana watu hawaishi kulalamika Lizzy majibu yake DRY!!Jamani. . I can't help it.

2. Je Ulishawahi kucheza mchezo wa baba na mama na kupika pika utotoni?
. . .Khaa, kuna aliyeishi uswahilini akapitwa kweli? Ila tu niseme sie hatukua tunafanya matusi kama ambavyo nasikia wengine walikua wakifanya.

3. Je umeolewa? Kama umeolewa, Je una watoto wangapi, na kama hujaolewa, ina maana huna hata wa kuchombeza?
. . . Mara ya tatu hii.Niliwahi kuwa mama mchungaji, nikawa 'firstlady' wa mwenyekiti wa mtaa, na sasa hivi nimetulia kwa balozi wa wabeba box.

. . . Kila ndoa imenibariki watoto wawili, kwahiyo nnao sita mpaka sasa.

4. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
Kifo cha mwanaJF mwenzetu Regia na Chentutu.

5. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana
Ushindi wa MMU Queen. . .japo Superman mpaka leo hajanipa zawadi yangu.

6. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
Vimini na jeans tight. . .ndio maana u'mama mchungaji ulinishinda.

7. Je unapenda chakula cha aina gani?
Kwanzia wali wa maharage mseto, ugali wa dagaa mpaka ndizi. machalari tunazopika sana kule kwetu Machame.

8. Ukipata fursa ya kupata staftahi na mheshimiwa Godbless Lema aliyekuwa Mbunge wa Chadema jimbo la Arusha, utamshauri nini?
Asife moyo. . .yeye ni wa watu wa Arusha na watu wa Arusha ni wake.

9. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
. . . Nalipa kodi. . .japo inaishia kwa mafisadi ila na mie nimejaribu.
10. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show…….
. . .Huu ntakupa pembeni usije ukaacha kunikaribisha tena kwenye kipindi.

Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Aunt Lizzy atakuja kuyajibu maswali yenu.

Karibuni sana
 
Last edited by a moderator:
na nilitaka kukujibia, ungenitambua.

Zile siri zote ningezianika hadharani.

Bi Zinduna asante sana kwa kunikaribisha kwenye kipindi, na naomba radhi sana kwa kuchelewa maana kipindi kilianza bila mie kuwa nimewasili. Sasa maana muda umeenda naomba nijibu maswali yako haraka haraka kama watazamaji hawajahamia TiBiSii.

Koh koh. . .
 
1.je ulishawai kutokewa na mume wa mtu na kama ndio ulikipingaje iko kishawishi???
2.ulishawahi kufaminia ama kufumaniwa??
3.unapenda mwanaume mwenye sifa gani??
4.je ukiwa kama mwanamke unawashauri nini wanawake wenzako kuhusu kujituma na kuachana na mawazo ya kuwezeshwa ama kutegemea wanaume ili watoke ktk maisha???

CUTE asante kwa maswali mpenzi. . .
1. NDIO. . . HAPANA yangu ilitosha kumjulisha siwezi kuwa nyumba ndogo wakati hata mie nna sifa za kuwa kubwa.

2. Heheheheh. . .hapana kwa yote. Kufumania labda kama ningekubaligi propasal ya Bishanga.

3. Kinyume na alizo nazo Bishanga . . . .
Yani asiwe na jitambi, majigambo wakati hata sura hailipi, asijione msomi kwakua tu anaongea kiingereza cha dikshenari, asijione tajiri kwa pesa za urithi n.k

4. Wajitume, waache uvivu na utegemezi na wivu wa kijinga watupe kuleee. Wivu wa kimaendeleo ndio wakuendekeza.

Enheeee. . .
 
Last edited by a moderator:
1. Ulishawahi fanya masterbation?
2. Kama ni amri yako, ungetoka na mkaka gani wa JF (ur secret admire)?
3. Can you give up ur carier n be a house wife for any reason

Kaunga heheheh. . .mbona mchokonozi hivyo? Haya maswali usikute kakupa Bishanga. . . lolz

Nwy. . .
1. HAPANA!!!

2. Hehehe. . .nanii, umhhhh jina lake linaanza na herufi nanii.

3. Aisee labda kwaajili ya watoto tu. . .na mpaka hapo niwe nimehakikisha pamoja na kuwa nyumbani haitokuwa mwisho wa mimi kutengeneza pesa.
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom