Zimwi la Richmond bado lamuandama Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zimwi la Richmond bado lamuandama Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 12, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  [h=1]Zimwi la Richmond bado lamuandama Lowassa[/h][HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Jacob Daffi - Imechapwa 02 November 2011


  [​IMG][​IMG][​IMG]


  VIONGOZI waliokuwa serikalini wakati wa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharula wa Richmond bado wanaendelea kung’ang’aniwa kwenye kashifa ya kushiriki kwenye ufisadi wa mkataba huo, MwanaHALISI limeelezwa.

  Wanaotajwa kushiriki kikamilifu, ni Edward Lowassa aliyekuwa waziri mkuu. Wengine waliokuwa mawaziri kwa nyakati tofauti katika wizara ya nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

  Taarifa zinasema mipango ya siri ndani ya serikali ndiyo ilifanikisha mradi wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

  “Siyo bure,” ameeleza mwanasheria mmoja jijini Dar es Salaam. “Walikuwa wanawekeza; na sasa wanavuna kwa kuchekelea.”

  Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya serikali, mambo kadhaa yalifanywa na serikali “kwa makusudi; bila shaka kwa manufaa ya baadaye.”

  Kwanza, kupinga na kukataa maamuzi halali ya bodi ya tenda ya TANESCO ambayo ilikataa maelezo na vitambulisho vya Richmond vya kuombea mkataba wa kuzalisha umeme nchini.

  Bodi ya TANESCO ilikatataa maombi ya Richmond mara tatu. Baada ya kuonyesa ujasiri huo, ndipo serikali ilinyakua madaraka ya Bodi na kuyatumia ilivyotaka kwa kuipa mkataba Richmond.

  Pili, Serikali iliamuru na kushinikza TANESCO kukubali mkataba kati yake na kampuni ambayo tayari waliishaikatalia mara tatu.

  Tatu, Serikali ilivunja sheria yake yenyewe (Sheria ya Ununuzi ya umma ya mwaka 2004) kwa kukalia nafasi ya muhitaji anayepaswa kuamua iwapo kinachohitajika kununuliwa kina manufaa kwake na kinahitajika kwa wakati huo.

  Nne, serikali kwa ushirikiano na wanasheria ilikubali suala la uvunjwaji wa sheria ya ununuzi wa bidhaa lijadiliwe katika mahakama ya usuluhishi ya kigeni badala ya kwanza kumaliza sula hilo katika mahakama za Tanzania.

  Hii ndiyo maana hukumu ya Jaji Emilian Mushi wa mahakama kuu, kanda ya Dar es Salaam, inasema mawakili wa TANESCO na serikali waliruhusu, kinyume cha utaratibu, mahakama ya upatanishi ya kimataifa (ICC) kutafsiri sheria za Tanzania.

  Anasema hatua ya mawakili hao, ndiyo sababu ya mahakama yake “kufungwa mikono” kwenye shauri lililofunguwa na asasi za kiraia kupinga malipo ya Sh. 111 bilioni kwa kampuni ya Dowans.

  “Katika suala hili,” anasema Jaji Mushi, “hoja muhimu ya kisheria iliyostahili kuletwa hapa mahakamani, ni juu ya hatua ya serikali kuipora bodi ya zabuni ya TANESCO, kazi ya kutafuta mzabuni, badala yake kazi hiyo ikafanywa na serikali yenyewe.

  Anasema kitendo hicho kilipaswa kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi na mahakama za hapa nchini kwanza, kabla ya shauri hilo kusikilizwa kwenye mahakama ya usuluhishi.

  Jaji anasema na kurejea taratibu kuwa “tathimini ya utoaji zabuni hufanywa na bodi ya zabuni ya TANESCO, sio serikali wala wizara ya nishati na madini.”

  Hayo yamo katika hukumu ya Jaji Mushi ya kurasa 89 ambayo gazeti hili linayo.

  Kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma, kifungu cha 31, siyo serikali wala wizara ya nishati na madini, aliyekuwa na mamlaka ya kutoa zabuni ya kufua umeme.

  Anasema kwa kuzingatia sheria hiyo, mahakama yake imehuzunishwa na kitendo cha serikali kujipa mamlaka yasiyoihusu.

  Hatua ya serikali kuipora kazi ya kutoa zabuni bodi ya Tenda ya TANESCO ilikwenda sambasamba na kurejeshwa kundini kampuni ya Richmond, ambayo bodi ya tenda ya TANESCO tayari ilishaindoa.

  Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku baadhi ya walioshiriki kuangamiza nchi kwenye mkataba huo wakihaha kujisafisha; huku Jaji Mushi akisema, “Kama siyo serikali kujiingiza katika mchakato wa zabuni, kusingekuwa na kashifa.

  Jaji Mushi anasema, “Jambo la kushangaza ni pale terehe 4 Aprili 2006, serikali ilipoitaka TANESCO kuziita kampuni nane ambazo awali ziliomba kupewa zabuni na kuzifanyia tathmini upya ikiwamo Richmond, ambayo tayari ilithibitika kutokuwa na uwezo wa kutekeleza mradi huo.”

  Mara baada ya serikali kupora mamlaka ya bodi ya zabuni, 30 Machi 2006, iliamua kutangaza upya zabuni hiyo kwa njia ya “International shopping procurement.”

  Jaji anasema, “…kwa kutathmini uhalisia na historia ya maombi haya, ukweli ni kuwa jambo hili ni gumu na linaumiza sana. Ugumu wa jambo hili ni kwamba, Richmond haikuwa na zana za kazi, wafanyakazi na uzoefu wowote katika miradi kama hiyo.”

  Anasema, “Ni jambo la kushangaza, serikali na mawikili wake wanakubali jambo hili la kuvunjwa kwa sheria ya manunuzi ya umma kwa kufanya lijadiliwe kwenye mahakama ya usuluhishi.”

  “Hatua ya mawakili wa serikali kuridhia mawakili wa Uingereza kujifungia kwenye hoteli ya Kilimanjaro-Kempinsk kutafasri sheria za Tanzania, ndiyo msingi wa kesi iliyofunguliwa na wanaharakati kupinga kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans kugonga mwamba,” ameeleza mwanasheria mmoja jijini Dar es Salaam.

  Ushahidi ulioletwa mahakamani, anasema Jaji, umethibitisha kwamba bodi ya zabuni ya TANESCO ilikataa kutekeleza maelekezo ya serikali ya “kuziita tena kampuni ambazo awali hazikupitishwa ikiwamo Richmond.”

  Katika uamuzi wake, Jaji Mushi ametupilia mbali maombi yaliyowasilishwa tarehe 27 Augosti 2011 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupinga malipo kwa kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Ltd.

  Maombi hayo yalikuwa ni ya kupinga maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi katika kitengo cha biashara ambayo iliamuru makampuni ya Dowans kulipwa fidia ya Sh. 94 bilioni na TANESCO kutokana na hatua ya kuvunja mkataba wake.

  Baada ya kuvunjwa kwa mkataba huo, 14 Septemba 2008 kampuni ya Dowans ilifungua shauri la madai katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiahara (ICC), kupinga kuvunjwa kwa mkataba kati ya kampuni ya Richmond Development Company (LLC) na TANESCO.

  Kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya mkataba wa TANESCO na Dowans wa 23 Juni 2006, pande hizo mbili zilikubaliana kutumia sheria za mahakama ya ICC, pale panapotokea migogoro ya kisheria; kuheshimu maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo na maamuzi hayo ndiyo yatakuwa ya mwisho.

  Kulingana na kifungu cha 28 (6) cha kanuni ya mahakama hiyo, maamuzi ambayo yatatolewa na mahakama hiyo yatakuwa ni ya mwisho na yatazifunga pande hizo na hayatakatiwa rufaa.

  Wakati hayo yakiendelea, MwanaHALISI limeelezwa kuna uwezekano mkubwa wa Dowans kuwa tayari imeshalipwa sehemu ya fedha inayodai.

  Kiasi kinachoelezwa kwamba kinaweza kuwa kimelipwa ni dola za Marekani 5.1 milioni (karibu Sh. 8. bilioni) ambazo ziliwekwa dhamana kwenye mahakama ya Uingereza.

  Mwanasheria mashuhuri nchini, Tundu Lissu amesema, “Kama serikali imeweka fedha hizo kama dhamana kwenye mahakama ya Uingereza, basi hakuna kinachoweza kuwazuia Dowans kulipwa fedha hizo.”

  Lissu alikuwa akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili aliyetaka kujua iwapo “fedha iliyowekwa dhamana na Tanessco yaweza sasa kuchukuliwa na Dowans kwa kuwa shauri limemalizika mahakama kuu ya Tanzania.”

  Amesema, “Kama fedha hizo ziliwekwa kama dhamana, basi hakuna njia ambayo TANESCO wanaweza kuzuia kuchukuliwa. Hapa labda kama kuna shauri jingine limefunguliwa Uingereza. Lakini kama shauri lenyewe ndiyo hilo la Dar es Salaam, mhh, hiyo hela kaka imeshakwenda.”

  Mahakama ya ICC iliamua kutoa tuzo kwa Dowans kwa kigezo kwamba pande hizo mbili zilijifunga kisheria kutatua matatizo ya kisheria kupitia mpatanishi chini ya mahakama hiyo.

  Kwa upande mwingine, Jaji Mushi anasema rekodi zilizopo zinamuonyesha Rostam Aziz, mfanyabiashara na swahiba wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete kuwa “anahusika katika kampuni ya Richmond.”

  Rostam alisafiri hadi Houston, Texas Marekani, tarehe 7 Oktoba 2006 kukutana na wawakilishi wa kampuni ya Richmond ambapo makubaliano yalifanyika ya kuidhamini kampuni hiyo.

  Ni Rostam Aziz, Jaji Mushi anasema aliyetumia madaraka yake kushinikiza uhamishwaji wa mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans; jambo ambalo lilithibitishwa kwenye mahakama ya ICC na mmoja wa mashahidi wa Dowans.
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ukisoma habari kama hyo (nilishaisoma kwenye Mwanahalisi) mwili unasisimka, hasa ukichek ubusy wa EL katika harakati zake za kuitaka nchi.
  Natamani kuwa na mengi kweli ya kusema ila pozi linaniisha nkichek koment za Tundu Lisu hapo kwamba hatuambulii hata "jiti"...
  Hapo kweli Mkuu Bubu lazima Utake Kusema lol
   
 3. Kaveli

  Kaveli JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 3,233
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Mkuu BAK, vipi hili zimwi la Richmond... bado linamuandama mh wetu ?

  -Kaveli-
   
 4. RingaRinga

  RingaRinga JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2016
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 970
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 80
  Kwani huzijui sifa za nyumbu mkuu
   
 5. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2016
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,095
  Likes Received: 11,582
  Trophy Points: 280
  HAKIKA PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA........
  Ni vigumu kuamini kuwa makamanda leo hii wanasema kuwa huyo jamaa alikuwa anasingiziwa na tena bila soni wanasema kuwa mwenye ushahidi apeleke mahakamani......
   
 6. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2016
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,163
  Likes Received: 4,192
  Trophy Points: 280
  Hili ndilo liliomuangusha na litakaloendelea kumuangusha Ngoyai
   
 7. Kaveli

  Kaveli JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 3,233
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280

  hahahaa mkuu, nimependa hayo maandishi yako in kapito: ''PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA''

  Kuna mdau mwingine humu alinifurahisha sana, yeye alisema hivi: ''HAKUNA SHUJAA KWENYE NJAA, yaweza mfanya mtu akala matapishi yake''

  Niwe muwazi tu... baada ya akadabla ya 'KUBADILI GIA ANGANI', binafsi ndipo nilihitimisha kuwa nchi hii bado hatuna upinzani wa kweli. Ni wachumia tumbo tu, na wajasiriamali.

  -Kaveli-
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2016
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  UKAWA, wazee wa kubadili na kuhamisha magoli.
   
 9. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2016
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 8,613
  Likes Received: 4,758
  Trophy Points: 280
  Duniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!E Mungu tusaidie.UNAFIKI,UNAFIKI,UNAFIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2016
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  Mungu akusaidie kwenye lipi wewe usiyejua maana ya unafiki!? Hebu thibitisha huo unafiki kwenye huo uliouita unafiki.

   
 11. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2016
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,378
  Likes Received: 6,559
  Trophy Points: 280
  Ukawa ni ajabu la nane la dunia
   
 12. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2016
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,163
  Likes Received: 4,192
  Trophy Points: 280
  BAK naomba kujua msimamo wako juu ya Waziri mkuu aliyejiuzulu.....
   
 13. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2016
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,095
  Likes Received: 11,582
  Trophy Points: 280
  Wewe ni miongoni mwa watu wachache wanaotumia akili zao vyema....bila ya kuyumbishwa na porojo za wafanyabiasiasa.......
   
 14. Kaveli

  Kaveli JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 3,233
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280

  Huwa nazikubali sana busara zako mkuu. SIASA ni biashara, followers wawe makini sana kwenye hiyo bizna.

  -Kaveli-
   
 15. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2016
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,753
  Trophy Points: 280
  hahahahahaha
   
 16. Ladyfirst

  Ladyfirst Member

  #16
  Aug 4, 2016
  Joined: Jul 26, 2016
  Messages: 42
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 40
  Naunga mkono hoja yako 100℅ hatuna wapinzani wenye msimamo, njaa na unafiki ndio siasa yetu pekee.
   
 17. Kaveli

  Kaveli JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 3,233
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280

  Mrembo nimekupenda buuuure kwa hayo maneno kuntu.

  -Kaveli-
   
 18. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2016
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,911
  Likes Received: 12,091
  Trophy Points: 280
  Tanzania kuna vituko!
   
 19. Kaveli

  Kaveli JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 3,233
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280

  Ni zaidi ya vituko.

  -Kaveli-
   
 20. Kaveli

  Kaveli JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 3,233
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280

  Huyo tumbo lake linampelekesha mpaka anashindwa kutumia ubongo.

  Ukiendekeza tumbo huwezi kuwa na msimamo ktk maisha.

  -Kaveli-
   
Loading...