Zimebaki siku 30 Diamond Platinumz na Zari kulitikisa jiji la Dar es Salaam na nchi nzima

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,212
42,076
Wasalaam wana jamvi....

Wachumba wa Zamani Diamond Platinumz na Zari wanatarajia kuandika historia nyingine kama ilivyo kawaida yao pale uwanja wa uhuru ambapo kutakuwa na matukio mengi sana ikiwemo album ya mwanamuzi Diamond Platinumz " A boy from Tandale" ambayo kwa tukio la kuzindua inataraji kuuza nakala 30,000 za mwanzo huku kukiwa na kiingilio kuwaona wasafi wote wakiongozwa na Diamond Platinumz.

Hata hivyo waandaaji wa tukio hili walishaomba uwanja wa taifa lakini wameambiwa utakuwa na matumizi hivyo wamepewa uwanja wa uhuru kwani kwa makisio yao waliona uwanja wa uhuru hautotosha kabisa lakini Plan imekuwa ni kufanya tukio hilo kila mkoa kwa kiingilio ambacho hakitasababisha watu kushindwa kupumua uwanjani.....

Katika siku hiyo kutakuwa na tukio lingine kubwa zaidi ambalo sitaliweka hapa kwa sababu za kibiashara lakini joto la tukio hilo litapanda zaidi ikifika march kwani kuna mengi zaidi yatatangazwa kuhusu Diamond na kuwaacha wengi midomo wazi....

Kikubwa zaidi ni kuwa tamasha hili hadi sasa linagombewa na kampuni kubwa mbili ambazo zinataka kuweka matangazo mule ndani ya uwanja siku ya tamasha ambalo bila shaka litaweka historia......

Wana jamvi kwa leo nawajuza haya tuu lakini mkumbuke kuwaona Diamond na Zari safari hii ni kwa pesa si bure tena......

Wasalaam
 
SIFA KUU YA MAFISIEM NI UNOKO, ROHO MBAYA, UMBEA MBEA ,MAONGO YAANI MANAFKI YA AJABU
Kuna bavicha wako very partisan ila nawakubali, wanajua kutofautisha majukwaa. Kwenye burudani mnaweza kuwa na mtazamo mmoja nao na maisha yakaendelea kama watu wenye mlengo mmoja ktk eneo hilo.
Wewe nakushangaa kwenye burudani unaleta siasa, wewe ni mtu mzima ila bado "mtoto", grow up na jifunze kutofautisha vitu na nini cha kusema ktk wakati gani na eneo gani.

Ruksa kunijibu kwa njia yoyote utakayo, nakuruhusu utoe povu lako looote kwenye matundu yako yote ya mwilini mwako, na mwenzako yeyoye atakayejisikia uko nae timu moja nae ruksa, atoe nyongo yake hapa ili maisha yake yaendelee salama.

Anzia hapa!
 
SIFA KUU YA MAFISIEM NI UNOKO, ROHO MBAYA, UMBEA MBEA ,MAONGO YAANI MANAFKI YA AJABU
nmecheka kwa nguvu hadi wachawi huko nje naskia wanataka niwashirikishe furaha yangu ili leo wasinipeleke kulima mashamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…